Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

PNC ATAKA KUIMBA NA P SQUARE

$
0
0

Na Elizabeth John



MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini kutoka kundi la Mtanashati Entertainment, Pancras Ndaki ‘PNC’ ameachia video ya ngoma yake mpya inayofahamika kwa jina la ‘Habari ya Mjini’.

Akizungumza jijini Dar es Salaam juzi, PNC alisema kazi hiyo kaisambaza wiki iliyopita katika vituo mbalimbali vya televisheni na anaomba sapoti kwa mashabiki wa muziki wa bongo fleva.

“Naomba wapenzi wa kazi zangu wanipokee vizuri na video ya kazi hii ambayo audio yake imefanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio kutokana na maudhui ya wimbo wenyewe, naomba sapoti ili niendelee kutoa burudani kwa mashabiki wangu,” alisema.

Alisema kwasasa anajipanga kufanya kazi na wasanii wakubwa ambao wanatambulika kimataifa wa hapa nyumbani na nchi za jirani kwa lengo la kukuza kipaji chake pamoja na kujitengenezea soko katika nchi mbalimbali kupitia kipaji chake.


“Naimani kwa kufanya hivyo nitakuwa mmoja wa wasanii wakubwa hapa nchini kutokana na kulitangaza jina langu vizuri, mungu akipenda nafikiria kufanya kazi na P Square katika moja ya nyimbo zangu,” alisema PNC.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>