![]() |
Eng.Philbert Rweyemamu akifafanua jambo katika moja ya mabanda ya maonyesho kwa baadhi ya maafisa wa uhamiaji walipokuwa wakitembelea mabanda ya maonyesho. |
![]() |
Michel Ash-Afisa Mkuu wa Masuala ya uendeshaji wa kampuni ya Acacia akizungumza na familia pamoja na wafanyakazi wa mgodi wa Buzwagi |
![]() |
Kikundi hiki cha Ngoma kutoka Shinyanga kilitia fola kwa burudani safi ya Ngoma waliyoitoa. |
![]() |
Baadhi ya maafisa wakuu wa kampuni ya Acacia wakifuatilia burudani ya ngoma |
![]() |
Baadhi ya maafisa wa idara ya ufanisi wa Mgodi wa Buzwagi wakiwa katika picha ya pamoja katika banda lao wakati wa maonyesho |
![]() |
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi mwenye shati la bluu akiongozwa na mkuu wa kitengo cha ulinzi Jamal Rwambol kutembelea mabanda ya maonyesho |
![]() |
Azael Kitange-Mkufunzi wa idara ya ufanisi wa kampuni akitoa maelezo kwa wageni walipotembelea banda la idara ya Ufanisi katika kitengo cha Mafunzo. |
![]() |
Wataalamu wa miamba wakionyesha aina mbalimbali za miamba yenye dhahabu na namna wanavyotumia vifaa vya kisasa kuitafuta dhahabu. |
![]() |
Kikundi cha Ngoma cha kabila la wasukuma kikitoa burudani ya ngoma wakati wa maadhimisho ya siku ya familia kwa wafanyakazi wa mgodi wa Buzwagi |
![]() |
Baadhi ya wanafamilia wa wafanyakazi wa mgodi wa Buzwagi. |
Baadhi ya maafisa kutoka Mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu wakifurahia moja ya burudani wakati wa sherehe hizo.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Eng. Philbert Rweyemamu (katikati) na Meneja wa Biashara wa Mgodi huo wakifuatilia kwa makini burudani zilizokuwa zikiendelea wakati wa sherehe hizo, kushoto kwao ni mwakilishi wa Mkuu wa wilaya ya Kahama.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii aliyekuwa Kahama
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii aliyekuwa Kahama
Buzwagi imeanzisha mkakati wa kukuza na kuboresha hali ya utendaji kazi kwa wafanyakazi wake kwa kuanzisha utaratibu wa kuwakutanisha wafanyakazi wa mgodi huo na familia zao mara moja kwa mwaka katika siku maalumu ya familia ambayo hutoa fursa kwa familia za wafanyakazi wa mgodi huo kuweza kujionea namna ambavyo shughuli za uchimbaji wa madini hufanyika na hivyo kuwa mabalozi wazuri wa kampuni kwa ujumla.
Mwaka huu wafanyakazi wa kampuni hiyo wamepata fursa ya kukutana na kujionea shughuli mbalimbali ambazo zimekuwa zikifanyika mgodi hapo. Pamoja na mambo mengine wafanyakazi hao pia walipata fursa ya kutembelea eneo ambapo shughuli za uchimbaji zinafanyika.
Sherehe hizo zilihudhuliwa na Afisa mkuu wa masuala ya uendeshaji Michelle Ash, Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulur-Graham Crew na meneja mkuu wa masuala ya ufanisi wa kampuni Janet Ruben pamoja na meneja mahusiano na mawasiliano wa Acacia Nector Foya, pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali..