Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

LHRC YAADHIMISHA MIAKA 20 TANGU KUANZISHWA KWAKE

$
0
0
 Mgeni rasmi katika Maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Septemba 26,1995, Jaji Mstaafu Osebia Munuo (katikati), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kitabu cha maadhimisho ya miaka 20 cha LHRC yaliyofanyika Makao Makuu ya LHRC Kijitonyama Dar es Salaam jana. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya LHRC, Geoffrey Mmari na Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Dk.Helen Kijo-Bisimba.
  Mgeni rasmi katika Maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Jaji Mstaafu Osebia Munuo (kushoto), akikata keki maalumu ya Maadhimisho ya miaka 20 cha LHRC yaliyofanyika Makao Makuu ya LHRC Kijitonyama Dar es Salaam jana. Anayeshuhudia kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya LHRC, Geoffrey Mmari na Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Dk.Helen Kijo-Bisimba.
 Wimbo wa taifa ukiimbwa kabla ya kuanza maadhimisho hayo.
 Waimbaji wa Kwaya ya LHRC ya Mwalusanya wakiimba wa wimbo wa Taifa.
 Wimbo wa Taifa ukiimbwa.

 Kwaya ya LHRC ya Mwalusanya ikifanya vitu vyake katika maadhimisho hayo.
 Hapa ni Kwaya ya Mwalusanya ikiserebuka kwa kwenda mbele. 'Jamaa wa mbele kushoto yupo vizuri kiuchezaji chezea maadhimisho ya miaka 20 ya LHRC wewe'
 Mwenyekiti wa Bodi ya LHRC, Geoffrey Mmari (katikati), akitoa hutuba fupi katika maadhimisho hayo. Kulia ni Mwakilishi kutoka Tume ya Taifa ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Rehema Ntimizi na kushoto ni Mgeni rasmi wa hafla hiyo, Jaji Mstaafu, Osebia Munuo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Dk.Helen Kijo-Bisimba (katikati), akisoma hutuba yake ya maadhimisho hayo. Kushoto ni Mjumbe wa LHRC, Emeliana Mboye.
 Meza Kuu ikionesha Kitabu cha Maadhimisho ya Miaka 20 tangu kuanzishwa LHRC baada ya kuzinduliwa kwenye hafla hiyo. Kutoka kushoto ni Mdau wa LHRC, Profesa Chris Peter,  Mjumbe wa LHRC, Emeliana Mboye, Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Dk.Helen Kijo-Bisimba, Mgeni rasmi wa hafla hiyo, Jaji mstaafu, Osebia Munuo, Mwenyekiti wa Bodi LHRC, Geoffrey Mmari na Mwakilishi kutoka Tume ya Taifa ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Rehema Ntimizi.
 Mgeni rasmi Jaji Osebia Munuo akisoma hutuba yake.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>