![]() |
![]() |
Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wanachama wa CCM pamoja na wananchi wa Jimbo la Kilindi kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni Mkoa wa Tanga. Miongoni mwa ahadi aliyoitoa kwa wanaKilindi ni kulishughulikia suala la upatikanaji wa huduma za maji safi na salama pamoja na ujenzi wa barabara ya kuingia na kutoka katika Wilaya hiyo.
![]() |
Kutoka kulia ni mgombea ubunge wa Jimbo la Kilindi, Mboni Muhita akiserebuka na baadhi ya viongozi na makada wa CCM walioongozana kwenye kampeni za mgombea mwenza Wilaya ya Kilindi. |
![]() |
Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan akimtambulisha mmoja wa wagombea wa udiwani CCM katika mkutano wa hadhara Jimbo la Kilindi. |
![]() |
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kampeni za CCM Taifa, Ummy Mwalimu (kushoto) na Mahadhi Juma wakijadili jambo kwenye moja ya mikutano ya kampeni ya mgombea mwenza. |
![]() |
Aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Nkenge, Asumpta Mshama akizungumza na wanaCCM na wananchi katika mkutano wa hadhara Jimbo la Kilindi kunadi ilani ya CCM. |
![]() |
Baadhi ya wananchi wakiwa wamesimama juu ya kisiki kuweza kumshuhudia mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akiwasili Jimbo la Kilindi. |
![]() |
Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika ofisi za CCM Wilaya ya Kiteto kabla ya kuanzamikutano ya kampeni kunadi ilani ya CCM. |
![]() |
Mgombea ubunge wa CCM Jimbo la Kiteto, Emmanuel Papian John (kushoto) akitambulishwa kwa wananchi na WanaCCM na Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan. |
![]() |
Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwenye mkutano wa hadhara Jimbo la Chemba. |