Na Mwandishi Wetu
MSHAURI wa ufundi wa kamati ya maandalizi mbio za Tabora Marathon Tullo Chambo, ameishukuru kampuni ya simu ya vodacom kwa msaada wa fulani 100 zilizotolewa jana jijini Dar es salaam.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake alisema kuwa Vodacom imekuwa msaada mkubwa kwao kwa kuwezesha upatikanaji wa fulana hizo ambazo zitatumika siku ya tukio juni 22.
“Tunaishukuru kampuni ya mawasiliano ya simu ya vodacom ingawa waliweza kutupatia fulana hizo kkwenye hatua za mwisho lakini tunatambua mchango wao katika suala zima la michezo hapa nchini na tuna omba waendelee na moyo huo”alisema Chambo
Akielezea maandalizi ya mbio hizo zitakazofanyika mwishoni mwa wiki hii,Chambo alisema kuwa hivi sasa wako kwenye hatua za mwisho ambapo mbio hizo zitakuwa ni za kilometa 21 kwa wanaume,16 kwa wanawake pamoja na kilometa 5 kwa watoto na watu wa umri wa kati.
Akikabidhi fulana hizo kwa niaba ya kampuni yake Matina Nkurlu ambaye ni meneja mahusiano alisema kwa kutambua umuhimu wa michezo nchini ndiyo sababu kubwa iliyowasukuma kutoa udhamini wa fulana 100 kwaajili ya mashindano hayo .
“Vodacom Tanzania itaendelea kudhamini na kuboresha michezo hapa nchini ikiwa ni wadhamini wa ligi kuu Tanzania bara na pia jamii inapaswa kutambua kuwa kampuni hii ni kwaajili ya watanzania”Alisema Nkurlu
Mbio za tabora marathon zinatarajiwa kufanyika mkoani Tabora Jumamosi ya juni 22 ambapo Vodacom ni kati ya wadhamini wa mbio hizo ,Filbert Bay foundation ,NGF Company limited, kampuni ya mabasi ya NBS,Emmanuel Mwakaataka pamoja na Sarah Ramadhani ambaye ni makamu mstaafu wa Rais Chama cha riadha Nchini.