WABUNGE wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wakiongozwa na Grace Kiwelu (Viti Maalum) na Godbless Lema (Arusha Mjini) wakiwa wamebeba mwili wa aliyekuwa Katibu wa CHADEMA Kata ya Sokoni One, marehemu Judith William Moshi, aliyeuwawa kwa bomu kwenye mkutano wa kampeni za chama hicho, Jumamosi iliyopita, Juni 15, 2013. Judith alizikwa jana kwenye makaburi ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Sokoni one, mjini Arusha.
↧