Quantcast
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Idris azoa Mil 500/- za BBA

 Mshindi wa shindano la Big Brother Africa msimu wa tisa, Idrisa Sultan ambaye ni Mtanzania (kushoto) akifurahia mara baada ya kutangazwa mshindi.
 Mshindi wa shindano la Big Brother Africa msimu wa tisa, Idrisa Sultan ambaye ni Mtanzania akifurahia mara baada ya kutangazwa mshindi.
 Mshindi wa shindano la Big Brother Africa msimu wa tisa, Idrisa Sultan ambaye ni Mtanzania akifurahia mara baada ya kutangazwa mshindi.
Mshindi wa shindano la Big Brother Africa msimu wa tisa, Idrisa Sultan ambaye ni Mtanzania (kushoto), akipokea mfano wa hundi ya dola za kimarekani 300,000 kutoka kwa Mkurugenzi wa M-Net Africa, Wangi Mba-Uzoukwu katika hafla iliyofanyika nchini Africa Kusini juzi usiku.

NA ANDREW CHALE

MSHIRIKI  wa Tanzania katika shindano la Big Brother Africa Hotshots, Idris Sultan amefanikiwa kushinda kitita cha dola 300,000, akiwabwaga washiriki wenzake kutoka nchi nane.

Katika fainali ya shindano hilo la msimu wa tisa ililofanyika juzi usiku nchini Afrika Kusini, Idris aliweza kuwambwaga wengine saba waliofika hadi hatua ya mwisho ya fainali.

Mshiriki huyo kutoka jijini Arusha, alipata ushindi huo kutokana na kupigiwa kura nyingi kutoka nchi tano tofauti, hivyo kuwazidi wenzake ambao waliishia kura tatu, mbili , moja huku wengine wakikosa kabisa.  

Idris anakuwa Mtanzania wa pili kunyakua taji hilo, akitanguliwa na Richard Bezuidenhout ambaye alishinda katika msimu wa pili, akifuata nyayo za Mwisho Mwampamba aliyeshika nafasi ya pili katika msimu kwanza.

Mwampamba pia alipata nafasi ya kushiriki pia msimu wa tano wa shindano hilo na kufanikiwa kuingia fainali, akiishia nafasi ya tano.
Kwa ushindi huo, Idris ameibuka na kitita cha dola 300,000 za Marekani sawa na sh. mil 500 za Tanzania.

Akizungumzia ushindi huo, Ofisa Mahusiano Mkuu wa kampuni ya Multchoice Tanzania ambao ni  wasambazaji wa visambusi vya Dstv, Barbra Kambogi, alisema ni faraja kubwa kwa Watanzania.

“Tunampongeza Idris kwa kutuwakilisha vema Tanzania. Tuna kila furaha na kwa sasa tupo katika mipango ya kumpokea ambapo tutawatangazia watanzania wote siku hiyo ya kumpokea,” alisema Barbra.

Shindano hilo ambalo lilifikia tamati juzi usiku, limedumu kwa miezi miwili sawa na siku 61, awali lilikuwa na washiriki 26 kutoka nchi mbalimbali za Afrika kabla ya kuchujwa mmoja hadi mwingine hadi kubaki nane.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>