Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Kibaden: Sijafa jamani, .awapa pole waliomzushia kifo

$
0
0
Na Mwandishi Wetu
KOCHA maarufu nchini na nyota wa zamani wa Klabu ya Simba, Majimaaji na  timu ya soka ya  Tanzania, Taifa Stars, Abdallah ‘King Mputa’ Kibaden, ameibuka na kusema hajafa na kwamba yu mzima wa afya.
Kibadeni aliyasema hayo baada ya kutafutwa kwa njia ya simu kupata uhakika kama yu hai kweli, kwani baadhi ya mitandao ya kijamii ilikuwa imeripoti kuwa nguli huyo wa soka nchini  amefariki.
Baada ya kupokea simu, Kibaden alitoa pole kwa wote waliopata taarifa za kifo chake na kushtuka kwani yeye yu umzima wa afya.
Kibaden alionyeshwa kushangazwa na kitendo hicho cha kuzushiwa kifo akisema ni dalili za baadhi ya watu kumtakia mabaya.
Alisema kutokana na taarifa hizo za kifo feki kisambaa kama moto wa nyika, kwa kutwa ya jana alipata usumbufgu mkubwa wa kupokea simu kutoka kwa ndugu, jamaa, marafiki na watanzania wanaomfahamu.
 "Mimi nipo nyumbani nikiwa mzima wa afya. Nashangazwa na habari kuwa nimefariki dunia. Nina wapa pole wale wote waliopata mshtuko kwa ajili yangu.
“Kuna wengine wananipigia, wakisikia sauti yangu, wanapatwa na mshituko... wapo waliomwaga machozi," alisema Kibaden kwa utulivu.
Kibadeni alisema, siku ya jana haikuwa usumbufu mkubwa kwake tu, bali hata kwa familia yake ambayo ilipokea simu nyingi za watu wakiwapa pole juu ya kifo changu.
Hata hivyo, Kibadeni alishukuru kwa baadhi ya vyombo vya habari vilivyomtafuta kwa simu kupata uhakika akimini vitasaidia kufikisha ujumbe kwamba ni uzushi.
“Ni vizuri mlivyonipigia simu, naamini mmetaka kupata ukweli wa taarifa hizo mbaya dhidi yangu. Mimi ni mzima wa afya,” alisema na kuongeza:
"Kutwa ya leo (jana) mimi na familia yangu tumepata mshtuko mkubwa. Jamani si kweli, mimi ni mzima wa afya niwape pole wote waliopata usumbufu kutokana na taarifa hizi za uzushi. Sijui mtu kazipata wapi?
Aidha, Kibaden alisema pamoja na kwamba hakuna mwanadamu atakayeishi milele, lakini anamshukuru Mungu bado yu hai hadi pale muumba wake atakapoamua.
Tanzania Daima  ilipowasiliana na mtandao wa  Taarifa.com,  simu yao ya kiganjani iliita bila kupokelewa.
Hivi karibuni Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imekuwa ikionya juu ya mitandao ya kijamii kuandika ama kutoa taarifa ambazo si sahihi.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>