Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

YANGA YAIZIMA EXPRESS YA UGANDA KWA BAO 1-0

$
0
0
 Mrisho Ngassa (kulia) na Andrey Countinho waniwania mpira.
Mashabiki wa Yanga wakifuatilia mchezo huo.
 Hekaheka.
 Salvatory Edward.
Kocha Msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa.
Nizar Khalfan akipiga shuti.
Oscar Joshua (kulia) akimiliki mpira mbele ya beki wa Express ya Uganda, Waswa Hassan.
 Golikipa wa Express, Kigundu Ali akidaka mpira miguuni mwa Nizar Khalfan.
 Nizar Khalfan akiwatoka wachezaji wa Express.
 Ogwawa Julius akimiliki mpira huku akizongwa na Oscar Joshua.
 Haruna Niyonzima akimiliki mpira.
 Hamis Kiiza akichuana na Lwanga Tadeo.
 Simon Msuva akimiliki mpira.
 Juma Abdul wa Yanga akipambana na mchezaji Express, Kasozi Bob.
 Moja ya heka heka zilizotokea katika lango la Express.
 Hamis Kiiza akiwatoka wachezaji wa Express.
 Hamis Kiiza akimbusu Simon Msuva kama ishara ya furaha baada ya kuifungia timu yake bao pekee katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki wakati ilipopambana na Express ya Uganda.
 Furaha ya ushindi.
Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao pekee la timu hiyo lililofungwa na Hamis Kiiza katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya The Express.
 Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao pekee la mshambuliaji, Hamis Kiiza.
 Hamis Kiiza (kulia) akishangilia bao aliloifiungia timu yake, katikati ni Mbuyu Twite.
Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao pekee la timu hiyo lililofungwa na Hamis Kiiza katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya The Express uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu

TIMU ya Yanga leo imeibuka na ushindi wa 1-0 baada ya kuwachapa Express ya Uganda katika mechi ya kirafiki ya kimataifa iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Katika mechi hiyo iliyokuwa yenye ushindani na ufundi mwingi kwa kila timu, licha ya timu hizo kufanya mashambulizi makali hasa Yanga, bado zilimaliza dakika 45 bila bao.
Hata hivyo, kilichowakera wapenzi na mashabiki wa Yanga katika mechi ya jana, ni kitendo cha Kocha Mkuu, Mbrazil Marcio Maximo kutompanga nyota mpya, Emerson de Oliveira Neves Roque.
Kitendo hicho kiliwakera mashabiki wengi ambao walilipa kiingilio kwa ajili ya kumuona kiungo huyo mpya ambaye tangu atue Jangwani, hajawahi kuonekana akicheza.

Hata hivyo, ukweli ni kwamba nyota hao wamewekwa ‘akiba’ kuelekea mechi ya Nani Mtani Jembe baina ya timu za Simba na Yanga itakayochezwa Desemba 13, kwenye Uwanja wa Taifa.
Kipindi cha pili, kiliendelea kuwa kizuri kwa upande wa Yanga ambapo dakika ya 71, Nadir Haroub Cannavaro alishindwa kuitendea haki pasi murua aliyotengewa na Mbuyu Twite.
Cannavaro alishindwa kufunga licha ya lango kuwa wazi, baada ya kipa wa Express ya Uganda kutoka langoni katika hekaheka ya kukabiliana na shambulizi hilo la nguvu la Yanga.
Dakika ya 90, nyota wa kimataifa wa Uganda, Hamis Kiiza akitokea benchi aliwainua mashabiki wa Yanga, baada ya kuifungia bao timu yake akiunganisha krosi murua ya Simon Msuva.
Msuva alikuwa ameitendea haki pasi ambayo ilitokana na mpira wa kurushwa na Juma Abdul na kumkuta Kiiza aliyeukwamisha wavuni na kuifanya Yanga kuondoka na ushindi wa bao 1-0.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>