Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Wazazi watunza ndani Mtoto Mlemavu miaka 9, bila kutoka Nje.

$
0
0
Mtoto, Daniel Julius Mushi  (12), mlemavu asiyetembea
anayetunzwa ndani  kwa miaka 9 bila kutoka nje tangu 2005.
(Picha na Bryceson Mathias)

Na Bryceson Mathias, Kikuyu


WAZAZI wa Mtoto, Daniel Julius Mushi (12), Julius Mushi na Ester Kwayu, ambao ni Waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Iringa Road, Dayosisi ya  Dodoma, wamemtunza ndani ya Nyumba Mtoto wao Mlemavu miaka Tisa (9) bila kutoka nje.

Wakizungumza nyumbani kwao baada ya Ibada ya Jumuia yao ya Mtaa wa Kikuyu Jumamosi 6, Mwaka huu, Wazazi hao kwa pamoja walisema, wamechukua hatua hiyo kutokana na kukosa Vifaa Tiba - Baiskeli ya kuwasaidia kumbeba atoke nje na kurudi ndani.

Wamewaomba Watanzania na Waumini wa Dini zote wenye Mapenzi Mema, wawasaidie ili mtoto wao apate Matibabu na Baiskeli ya kuwasaidia kumtoa nje na kumrudisha ndani, ikibidi aweze kusoma shule za Walemavu wasiojiweza, waweze kuondokana na kumtunza ndani.

Mtoto huyo ambaye awezi kuongea, atembei, isipokuwa kukaa, kucheka na kutoa Udenda tu, huku miguu yake ikiwa imelemaa tangu alipokuwa na umri wa miaka Miwili (2), hali ambayo Mama yake anabainisha ilimuanza kwa kuwashwa puani, na alipojikuna hali hiyo ilitokea.

“Nikiwa na Shughuli namuacha ndani akiwa amelala au amekaa kwenye Kochi kama alivyo hapo (pichani), sana sana atajigeuza geuza tu, na ndiyo maana tunaona ni afadhali alale ndani kwa sababu kwenye Kochi anaweza akaangka na kuumia”.alisema Mama yake Kwayu!.

Alisema, watoto wenye umri wake waliozaliwa pamoja, hivi sasa wenzie wako Darasa la Sita, na mwaka huu wataingia darasa la Saba, lakini yeye bado anaendelea kuteseka kwa Masahiba  hayo huku tukichua Jukumu la kumsaidia kwa kila huduma ya Maliwato na Chakula.

Baba yake Mtoto huyo Julius alisema, wanawaomba watu wema wote wenye Ushauri na niya ya   kuwasaidia Ki-Matibabu, Baiskeli na Msaada wa Masomo ya Watoto kama Mtoto wao alivyo, wawasiliane nao kwa Namba yake 0755-091656, na ya Mke wake ni 0754-826419.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>