Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

PHD AWATAYARISHA MASHABIKI

$
0
0

Na Elizabeth John


STAA wa filamu na muziki wa kizazi kipya nchini, Hemed Suleiman ‘PHD’ amesema kabla ya mwaka haujaisha atakuwa amesambaza video kali sita za nyimbo zake mpya.

PHD ni kati ya mastaa ambao wanafanya vizuri katika tasnia hizo kutokana na ubora wa kazi zake na kukubalika katika jamii.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, PHD alisema, anaomba Mungu ampe uzima na akamilishe ratiba hiyo ambayo amejipangia kwa mwaka mzima.

“Nawashukuru mashabiki kwa kunikubali kwanza kwani bila wao mimi sio msanii, nimejiwekea ratiba yangu naomba uzima ili kuikamilisha siwezi kusema kama nitakamilisha kikubwa ni maombi yenu,” alisema.


Alisema hataki kutaja majina ya kazi zake kwa kuhofia kuondoa radha na maana ya wimbo mapema kabla hajatoa, anapotaka kutoa kazi ndio anatangaza jina.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>