Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

FID Q AWAPA CHANGAMOTO WAANDAAJI WA KILI MUSIC

$
0
0

Na Elizabeth John
MKALI wa muziki wa hip hop nchini, Farid Kubanda ‘Fid Q’ amesema tuzo za mwaka huu zilikuwa za mwisho kushiriki endapo waandaaji wa tuzo hizo wasingetambua mchango wake tangu mwaka 2004.

Akizungumza jijini Dar es Salaam juzi, Fid Q alisema miaka mingi amekuwa akishiriki tuzo hizo bila mafanikio yeyote tangu alivyopata mwaka 2004 hajawahi kupewa tena wakati kazi alikuwa anafanya na kuambulia kushiriki tu.

“Sijawahi kumwambia mtu, nilikuwa nasema mwenyewe moyoni na ndio maana hata siku ile nilishindwa kuongea nilipotakiwa kuongea nilitaka kuwauliza, leo saa mbovu imepata majira? lakini nikaona kwasababu wenyewe wamejiongeza na kuona mchango wangu basi niwaache tu,” alisema Fid Q.

Aidha, Fid Q alisema kutokana na upinzani uliopo katika soko la muziki kwasasa wasanii wengi wamekuwa hawapendani, yeye hana mpango wa kugombana na mtu na anayemchukia yeye hana mpango nae.

“Sijawahi kugombana na msanii yeyote, mimi kila msanii ni mshikaji wangu, ambaye ataona ana chuki na mimi kwa mambo yake binafsi mimi sijali mimi kila msanii ni ndugu yangu,” alisema Fid Q.

Fid Q mwaka huu amechukua tuzo mbili za msanii bora wa kiume hip hop na mtunzi bora wa mashairi ya hip hop.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>