
Na Elizabeth John
STAA wa filamu za Bongo, Wema Sepetu amesema filamu nyingi za Bongo ni filamu za makochi na juisi hivyo kwasasa ameamua kuja tofauti.
Akizungumza jijini Dar es Salaam juzi, Wema alisema, stori nyingi za filamu huwa zinajirudia sana, utakuta mke hazai au kwa waganga kila siku hizo hizo wasanii wengi ni wavivu wa kufikiria na kujaribu kubadilisha mazingira.
“Filamu mpya ambayo natarajia kuingiza sokoni itakuwa na utofauti mkubwa wsana nimejaribu kufanya uchunguzi wa filamu nyingi hakuna msanii anaekwenda mbali zaidi hii itakuwa ni bonge la kazi,” alisema.
Wema ambaye aliwahi kuwa Miss Tanzania mwaka 2006, alisema kazi hiyo inajulikana kwa jila la ‘Family’ amecheza na rafiki yake, Aunt Ezekiel na hadithi hiyo itawavuta mashabiki wengi kutokana na kuonesha uhalisia wa maisha ya binadamu na sio kuigiza.
“Kuna kipindi nilinyoa kipara, wengi walijiuliza ni kwanini nimeamua hivyo, nimecheza kama mgonjwa wa kansa lengo langu ilikuwa ni kucheza kitu kiuhalisia,” alisema mwanadada huyo.