
Na Elizabeth John
MKALI wa muziki wa kizazi kipya nchini, Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ amesema hakutegemea kama kuna siku video yake itakuwa inachezwa mara kwa mara katika televisheni kubwa barani Afrika.
Akizungumza jijini Dar es Salaam juzi, Dimpoz alisema, kwasasa amepata jibu kwanini kuwekeza na kufanya video nzuri kunafaida kubwa kwa wasanii wakubwa Duniani.
Alisema kutengeneza video ya wimbo wake mpya wa ‘Ndagushima’ ambayo inafanya vizuri hivi sasa ametumia zaidi ya milioni 30 ambapo kwasasa anakula matunda yake.
“Nilikuwa sijui kwanini wasanii wenzetu wanatumia gharama kubwa kutengeneza video zao, lakini kwasasa nimeju na namshukuru Mungu kanisaidia kazi hii inafanya vizuri na inapigwa katika televisheni zote za Afrika,” alisema.
Alisema baada ya kusambaza video hiyo, amepata mialiko mingi ya nchi za Kenya, Afrika Kusini na Nigeria.
Dimpozi kwasasa anatamba na ngoma yake ya ‘Ndagushima’ yenye maana kwamba ‘mrembo’ licha ya kuwa ananyimbo zingine zinazofanya vizuri kama Baadae, Me and You, Nai nai na nyinginezo.