Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Article 1

$
0
0
KAMPENI ZA UCHAGUZI KALENGA ZAFIKIA TAMATI
 Badhi ya wananchi wa kijiji cha Sadani, wakifurahia baada ya kuwasili kwa mgombea ubunge wa jimbo la Kalenga kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Grace Tendega, ambaye aliambatana na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe ambako walifanya mkutano wa kampeni juzi. (Picha zote na Joseph Senga)
 Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Sadani wakiitikia kibwagizo cha People's Power cha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wakati wa mkutano wa kampeni za mgombea ubunge wa jimbo la Kalenga kupitia chama hicho, uliofanyika katika kijiji hicho juzi.
Baadhi ya viongozi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), wakiwa katika mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani), kuelezea hatua za mwisho za taratibu na sheria za uchaguzi, uliofanyika mjini Iringa jana. Kutoka kulia ni Makamu Mwenyekiti, Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar, Hemed Mahamoud Hamid, Prf. Amon Chaliga (Mjumbe) na Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu, John Mkwawa.
 Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akiongozana na mgombea ubunge wa jimbo la Kalenga kupitia chama hicho, Grace Tendega baada ya mkutano wa mwisho wa kampeni uliofanyika katika kijiji cha Ifunda.
Mgombea ubunge katika jimbo la Kalenga kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Grace Tendega akiwahutubia kwenye mkutano wa mwisho wa kampeni, katika kijiji cha Ifunda.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>