Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promitions, Alex Msama akiwaonesha wahariri wa michezo kutoka vyombo mbambali vya habari jijini Dar es Salaam jana, namna wananchi wanavyopiga kura kuchagua waimbaji, mikoa na mgeni rasmi wa tamasha la Pasaka 2014 kwa njia ya ujumbe mfupi ‘SMS’
ZOEZI la upigaji kura kupendekeza Mgeni rasmi katika Tamasha la Pasaka limezidi kupamba moto huku viongozi mbalimbali wakipendekezwa na wananchi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam jana, wakati wa kuwaonesha namna zoezi hilo linavyofanyika, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi, Alex Msama, alisema zoezi hilo linaratibiwa na kampuni ya Bofya Limited na kwamba, majina ya Rais Jakaya Kikwete, Kiongozi wa Upinzani Bungeni,
Freeman Mbowe na Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa yamependekezwa na wananchi wengi.
Alisema ili kupendekeza mgeni rasmi katika tamasha hilo , unatakiwa kutuma jumbe mfupi wa maneno kwa kuandika Mgeni rasmi Pasaka unaacha nafasi kisha jina la mgeni rasmi kwenda 15327.