Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

YOUNG KILLER ANUSURIKA KURUSHWA KICHURA MWANZA

$
0
0

Na Elizabeth John
KINDA wa muziki wa kizazi kipya nchini kutoka Mwanza, Erick Msodoki ‘Young Killer’ amenusurika kurushwa kichura na wanajeshi baada ya kukatiza katika kambi yao akiwa amevaa pensi inayofanana na sare ya jeshi.

Akihojiwa na redio Clouds, Young Killer alisema, alikuwa anakatiza kambini hapo huku amevaa pensi yenye rangi za jeshi, wanajeshi walimuita na kumtaka aivue na kuwakabidhi.

“Mimi nilikuwa nishajisahau kama nimevaa nguo ya jeshi, nikashtukia tu we dogo njoo hapa alikuwa mbali ila nilishindwa kukimbia ikanibidi niende akanambia nivue nimpe sema bahati nzuri nilikuwa na kaka yangu alikimbia nyumbani kunichukulia pensi nyingine ndio nikabadilisha,”.

“Yani kwa bahati nzuri nilikuwa na kaka yangu vinginenyo ningehaibika, na tulikuwa karibu na nyumbani wanajeshi hawana huruma hata kidogo,” alisema Young Killer.

Young Killer alishawahi kutamba na ngoma zake kama ‘Jana na Leo’, ‘Dear Gambe’ ‘Message to God’, ‘Mrs Superstar’ na nyinginezo ambazo zinafanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio na televisheni.

  




Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>