Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Article 4

$
0
0
Mandela ni Kioo cha Ma-Rais na Viongozi wote duniani

Na Bryceson Mathias

MA-RAIS na Viongozi wote duniani, hivi leo wakitaka kupima na kujitazama mwenendo na Sura ya Utawala walionao, basi wanatakiwa kujipima ma kujifunza kwa kujiangalia kwa Mwanga wa Afrika, Nelson Mandera, ambaye Hakika ni kioo Chao.

Mandela ambaye ni Udongo wenye rutuba halisi ya Afrika, Mpiganai Uhuru wa Kweli, Mfungwa wa Kisiasa Mwenye Ushindi, Mwafrika wa kwanza kuwa Rais wa Afrika kusini, na Kiongozi pekee mwenye kusamehe na kusahau, anayefananishwa na Yesu Kristo.

 Napata Shaka kibinadamu, Iwapo Mungu ataruhusu azaliwe mtu mwingine kama Mandela, ambaye anaweza kuwa Kioo na ‘Tape Recorder’ ambapo watu wakitaka kuwatendea mema wananchi wao, wanatakiwa kujitazama na kusikiliza ili wajirekebishe udhaifu wao.

“Hivi yuko Rais au Kiongozi duniani anayethubutu kujigamba akijifananisha na Mandela? Hakunaaa! Na hatatokeaa labda Mungu mwenyewe apende kumleta tena Mtu wa namna hiyo kwa lengo maalum ili watu wajifunze tena, Ingawa fundisho hilo limepita hawajaelimika”. alisema Mama mmoja wa Mazimbu Morogoro aliyeomba asitajwe.

Mama huyo aliongeza kusema, Kama kuna mtu aliyekuwa Mwana Demokrasia wa kweli kwa Mawazo, Maneno na Vitendo,dunia, basi ni Mandela.  Wengine wanaojifananisha ati wanaenzi Demokrasia ni Vivuli tu (Photocopy).

“Je viongozi wetu leo wako tayari kujitazama kwa Mandela?”.aliuliza?

Tunafahamu kwa kusoma na kuamini kwamba,  mwenye kusamehe dhambi akasahau kidini, alikuwa Yesu Kristo (Issa Bin Mariam). Kama ilikuwa kwa Mitume waliopata neema ya kufanya sehemu ya kazi za Yesu, basi na Mandela ni miongoni mwa Sura na Utashi wa Yesu.

Yesu aliwasamehe watu wote waliomtukana, Waliompiga na Kumtesa, Waliomtemea Mate, Waliomnyanga’anya Mavazi, Waliomchoma MKuki, Waliomdharau, Waliomvisha Taji ya Miiba na Kumpigilia Misumari Msalabani akasema, “Baba Wasamehe maana hawajui walitendalo”.

Kama Yesu, Mandela naye aliwasamehe Makaburu na Makaburu Weusi wa Ki-Afrika waliobambikizwa Uzungu kama Ndevu za Maagizo tangu alipokuwa na alipotoka Gerezani, na akawaunganisha kuijenga Afrika Kusini Mpya akiwa Rais. Je nani katika nchi zetu anaweza?

Kama Viongozi wetu wa Ki-Afrika mara wanapopata Uongozi cha kwanza wanafikiria kurudisha Kisasi, Watawafunga Mahasimu wao Maisha, Watawanyonga, wataweza kuenzi yale aliyofanya Mandela kiasi cha kuachia Uongozi wakati bado unanoga?

Kama kwa Uhasimu huu tu! Viongozi au watu wanaweza kudiriki kufanya Ukatili wa kuwamwagia watu Tindikali, Kutoboa watu Macho na Kuua Wandishi na Viongozi wa Dini, kuwatoa watu Kucha, Kuua Albino, Kupiga watu wanaodai haki Mabomu, Kusalitiana, Kuvunja Watoto Miguu, Kufyeka Mapanga Mtoto aliyechuma Pera. Tuwafananishe na Mandela?

La Hasha, hao hatuwezi kuwalinganisha naye hata kidogo, bali hao tutawaita Maadui na Wauaji wa Demokrasia, Waasi, Wauaji, Dhulumati, Mafisadi wa Mali, Miili na Uchumi wa Umma wa Taifa hilo.

Huwezi kuwa na Majeshi yanayofunzwa Porini kwa ajili ya kuwadhulu, kuwajeruhi, Kuwapa Vilema vya Kudumu, Kuwaua Mahasimu wako, Kuwapandishia Bei za Bidhaa wananchi ovyo,   halafu katika nchi hiyo ya Ki-Afrika tukuite eti unafanana na Madiba mwenye kusamehe bure! Aaa!

Hapo, ndipo tunaposema kifua mbele, Mandela ni Kioo cha Ma-Rais na Viongozi wote duniani, anayetaka kufikia hapo basi ajikane, ajitwike Msalaba amfuate. Hapo tutakuwa na sababu ya kumuenzi na badala ya kulia, tutaimba kwa furaha kushangilia kama Wananchi wa Afrika Kusini walivyofanya. Jione kwa Mandela!.


0715933308   

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>