Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all 19659 articles
Browse latest View live

  WATANZANIA TUTUNZE RASILIMALI ZA MISITU-MAJALIWA

$
0
0
Akabidhi hundi mbili zenye thamani ya shilingi bilioni 4.27 zilizotokana na hewa ukaa

 

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Watanzania watunze rasilimali za misitu kwa kuwa zinafaida kubwa kwa Dunia, Taifa na mwananchi mmoja mmoja.

 

Amesema kuwa katika vipindi tofauti Rais Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa akisisitiza juu ya umuhimu wa kuhifadhi misitu nchini, hivyo kila mmoja ahakikishe anazingatia suala hilo. 

 

Ameyasema hayo leo (Jumatatu, Desemba 12, 2022) alipozungumza na wananchi wa kijiji cha Kagunga Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi baada ya kukabidhi hundi mbili zenye thamani ya shilingi bilioni 4.27. Fedha hizo zilizotolewa na taasisi ya CARBON TANZANIA kwa wananchi wa vijiji vinane na Halmashauri ya wilaya ya Tanganyika zimetokana na mauzo ya hewa ya ukaa awamu ya sita.

 

“Fedha hizi mmezipata kutokana na tabia yenu nzuri ya utunzaji wa misitu, endeleeni kuitunza misitu hii ili tupate mvua za kutosha. Pia, tumieni mvua hizi zinazoendelea kunyesha kwa kupanda mazao mbalimbali.”

 

Mheshimiwa Majaliwa amewataka watumishi wa umma nchini waendelee kuweka mikakati ya kuwaelimisha wananchi kuhusu utunzaji wa mazingira. “Kila mtumishi wa umma kwenye eneo lake ahakikishe moja ya agenda iwe uhifadhi wa mazingira.”

 

Kadhalika, Mheshimiwa Majaliwa amezitaka halmashauri zote zenye miradi ya hewa ukaa zifuatilie mikataba inayosainiwa baina ya makampuni na vijiji kwa ajili ya mauzo ya hewa hiyo. “Mikataba hii ni lazima tuijue, wanasheria wetu lazima muifuatilie.”

 

Waziri Mkuu amewataka wana-Vijiji watumie fedha wanazozipata kutokana na mauzo ya hewa ya ukaa kwa maslahi ya wananchi wote. “Wakurugenzi fuatilieni kama mipango ya wanavijiji ina maslahi kwa wananchi wote, jengeni miundombinu ya umma, posho isichukue nafasi kubwa.”

 


Washindi wazoa zawadi za milioni 96.5 NMB MastaBata 'Kote Kote'

$
0
0


Meneja Mwandamizi Biashara za Kadi Benki ya NMB, David Ngusa (kulia) na Meneja wa NMB Tawi la Bank House, Seka Urio (kushoto) wakimkabidhi tiketi ya kuhudhuria tamasha la Fullmoon Party visiwani Zanzibar, Elihuruma Minja (katikati), mshindi wa droo ya nne ya Kampeni ya NMB MastaBata ‘Kote Kote’ inayohamasisha matumizi ya kadi badala ya pesa taslimu.

 

Na Mwandishi Wetu

 

Kampeni ya NMB MastaBata ‘Kote Kote,’ inayoendeshwa na Benki ya NMB, imezidi kupasua anga baada ya zawadi zenye thamani ya Sh. Mil. 10.5 kutolewa kwa washindi 76, hivyo kufanya jumla kuu ya zawadi kufikia zaidi ya Sh. Mil. 96.5 kati ya Sh. Mil. 350 zilizotengwa.

Washindi 76 walipatikana wakati wa droo ya tano iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana, ambako pia washindi wa pikipiki wa droo ya nne na washindi wa safari ya Zanzibar iliyolipiwa kila kitu na NMB, walikabidhiwa zawadi na tiketi zao.



Katika droo hio iliyochezeshwa chini ya Ofisa wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Salim Bugufi, ilishuhudiwa David Kaaya akiibuka mshindi wa bodaboda yenye thamani ya Sh. Mil. 3, huku washindi wengine 75 wakijinyakulia Sh. 100,000 kila mmoja.

Katika hafla hiyo, Elihuruma Minja na Grace Mponeja walikabidhiwa tiketi za safari ya kwenda Zanzibar (wao na wenza wao), ambako watahudhuria tamasha la Zanzibar Full Moon Party, huku Hamza Hamood akikabidhiwa pikipiki aliyoshinda katika droo iliyopita.

Akizungumza kabla ya droo hiyo, Meneja Mwandamizi Biashara za Kadi NMB, David Ngusa, alisema tayari zawadi zenye thamani ya Sh. Mil. 86 zilishatolewa kwa washindi mbalimbali waliopatikana katika wiki nne za kampeni hiyo inayofanyika kwa msimu wa nne sasa.

“Ni kampeni inayohamasisha matumizi ya kadi badala ya pesa taslimu ‘cashless,’ ambayo ni salama na nafuu zaidi, ambako tumetenga zaidi ya Sh. Mil. 350 kuwazawadia wateja wetu wanaotumia kadi za NMB mastercard kwa kutumia POS, Online au Lipa Mkononi (QR Code).



“Kila wiki tunakabidhi Sh. Mil. 7.5 kwa washindi 75, huku tukitoa pikipiki moja. Lakini pia tuna droo za mwezi, tunakowazawadia Sh. Mil 1 washindi 49, sambamba na bodaboda mbili, na droo ya fainali itazawadia safari za Dubai kwa washindi saba na wenza wao kwa siku nne,” alisema Ngusa.

Kwa upande wake, Bugufi alibainisha kuwa usimamizi wa droo za NMB MastaBata uko chini ya GBT, ambayo ni taasisi tanzu ya Serikali yenye jukumu hilo, hivyo kuwataka Watanzania kufanya matumizi yasiyo ya pesa taslimu ili kuwania zawadi mbalimbali za kampeni hiyo.

 Baada ya kukabidhiwa tiketi zao za kwenda Zanzibar kuhudhuria Tamasha la Full Moon Party linalofanyika katika fukwe za Kendwa Rocks, Elihuruma na Grace waliishukuru NMB kwa fursa adhimu ya utalii wa ndani waliyoipata mwishoni mwa mwaka wao na wenza wao.



Magazeti ya Tanzania leo Desemba 13, 2022

UBUNIFU, UBORA WA BIDHAA ZA WAJASIRIAMALI WATIA FORA MAONESHO YA JUAKALI

$
0
0


Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Riziki Pembe Juma na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Robinah Nabbanja wakiangalia bidhaa za mmoja wa wajasiriamali kwenye maonesho ya 22 ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya Wajasiriamali Wadogo na Wakati maarufu Juakali, yanayoendelea jijini Kampala, Uganda. 

 

 Na Mwandishi Wetu, Uganda

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Riziki Pembe Juma ameeleza kuridhishwa na namna Wajasiriamali wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wanavyoongeza viwango vya ubora na ubunifu katika huduma na bidhaa wanazozalisha. 

 

Waziri Riziki Pembe Juma ameeleza hayo alipozungumza kwenye sherehe za ufunguzi wa maonesho ya 22 ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya Wajasiriamali Wadogo na Wakati maarufu kama Juakali, zilizofanyika tarehe 11 Disemba 2022 katika viwanja vya Uhuru vya Kololo jijini Kampala, Uganda. 

Amesema hatua iliyofikiwa na Wajasiriamali hao ni dalili nzuri ya kufikiwa kwa lengo la kuyafanya maonesho hayo  y’a Juakali kuwa jukwaa la fursa ya kukuza masoko, kubadilishana uzoefu na teknolojia. 

 

Ameongeza kuwa hali hiyo inatokana na ukweli kuwa wajasiriamali hao bado wanahitaji kuendelea kujifunza zaidi, kubadilishana uzoefu na teknolojia baina yao katika Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

 

“Sote tumeshuhudia bidhaa mbalimbali zinazouzwa katika baadhi ya mabanda yaliyopo katika maonesho haya ambayo yamejumuisha nchi zote wanachama, bidhaa zina ubora na ubunifu wa hali ya juu. Ongezeko hili la ubunifu na ubora wa bidhaa za wajasiriamali hawa kila mwaka, ni dalili njema kuwa wana Afrika Mashariki katika siku za usoni tutakuwa na bidhaa zinazotosheleza mahitaji yetu kwa ubora na wingi hali ambayo itasaidia kupunguza utegemezi wa bidhaa kutoka nje” alisema Mhe. Waziri Riziki

 

Mhe. Waziri Riziki pia ameeleza kuridhishwa na namna Wanawake walivyojitokeza kushiriki katika maonesho hayo. 

 

Asilimia 87 ya idadi ya Wajasiriamali zaidi ya 300 wa Tanzania kwenye maonesho haya  ni Wanawake, hali hii inadhirisha na uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan unatoa kipaumbele kwa wanawake kwa kuzingatia kuwa mwanamke ni kiungo thabiti katika maendeleo ya familia na nchi kwa ujumla, alisema Mhe. Waziri.

 

Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Robinah Nabbanja ambaye alimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni katika sherehe hiyo ya ufunguzi wa maonesho, ametoa wito kwa Serikali za Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuendelea kufanya mabadiliko muhimu ya sera za uchumi ili ziweze kuleta msukumo katika kuongeza uzalishaji wa bidhaa na kurahisha zaidi ufanyaji wa biashara katika Jumuiya. 

 

“Kundi la wajasiriamali wadogo na wakati linachangia asilimia 60 ya pato la Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, huku 99% ya biashara ndogo na kati zikimilikiwa na wazawa wa Afrika Mashariki, ni muhimu kukumbuka kuwa katika kila Waafrika 10; 6 kati ya hao wamejiajiri katika sekta ya biashara ndogo na kati, hivyo ni sawa na kusema kuwa, biashara ndogo na za kati zinazalisha wastani wa ajira 8 katika kila ajira 10 mpya,” alisema Mhe. Waziri Mkuu Nabbanja

 

Mheshimiwa Nabbanja alisisitiza kuwa endapo sera zitakuwa rafiki zaidi kiasi cha kutatua changamoto zinazowakabili wazalishaji wadogo italeta manufaa makubwa ya kiuchumi kwa Jumuiya, kwa kuwa asilimia 99 ya Wajasiriamali ni wazawa wa Afrika Mashariki hivyo maboresho hayo yatawanufaisha wao moja kwa moja na kuleta mchango mkubwa katika maendeleo ya viwanda na upatikanaji wa ajira za kutosha kwa Vijana na wanawake.

 

Mhe. Nabbanja amesema maonesho ya juakali ni jukwaa muhimu linalowawezesha Wajasiriamali kuonesha na kuuza huduma na bidhaa wanazozalisha, vilevile yanatoa fursa hadhimu kwa Wajasiriamali kuongeza wigo wa soko, kujifunza zaidi kuhusu ubunifu na kubadilishana uzoefu na teknolojia katika masuala mbalimbali kama vile kuongeza thamani ya mazao ya kilimo na mifugo.

 

ARGENTINA NA NUSU FAINALI YA KISASI KWA CROATIA

$
0
0

 Na John Richard Marwa


Wakati zikibakia dakika chache Dunia nzima kushuhudia Nusu Fainali ya kwanza ya Kombe la Dunia pale nchini Qatar kwa Argentina kumeyana na Croatia.


Unatazamwa kama mchezo wa kisasi kwa Lionel Messi na wapambe wake kutoka America Kusini. Ni kisasi cha Fainali za Kombe la Dunia zilizopita kule nchini Urusi ambako Argentina na Croatia zilikuwa kundi moja na mchezo wao Croatia alimbugiza Argentina mabao (3-0).


Leo ni pale Qatar ambako anahitajika mshindi mmoja kutinga hatua ya Fainal ya makala ya 22 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1930.


Argentina wanahitaji kushinda mchezo huo ili kuweka matumaini hai ya Messi kutwaa taji hilo jambo ambalo Dunia nzima inasubiri kutazama.


Wakati Croatia wakiwa wanahitaji kucheza fainali ya pili mtawalia mara baàda ya kufanya hivyo 2018 pale Urusi ambako Ufaransa aliwaa taji hilo mbele yao.


Miamba hiyo imekutana mara tano, kila timu ikishinda mara mbili na sare moja.

TUME YA KUREKEBISHA SHERIA NI INJINI YA SEKTA YA SHERIA NCHINI

$
0
0

 

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akizungumza na viongozi wa Wizara na watumishi wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania wakati akifungua mafunzo ya siku tatu kwa watumishi hao kuhusu Sheria, Taratibu na Kanuni za Utumishi wa Umma yanayofanyika Jijini Dar es Saalam.

 

Na Mwandishi Wetu, LRCT Dar es Salaam

 

Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania (Law Reforms Commission of Tanzania – LRCT) ni injini ya Sekta ya Sheria nchini ambayo imeundwa na Serikali na kukasimiwa majukumu ya kurekebisha sheria nchini ili kuhakikisha uwepo wa haki na maendeleo ya taifa kwa wananchi ambapo ni vema kutekeleza majukumu kwa kuzingatia maadili, sheria, taratibu na kanuni za utumishi wa umma

Hayo yameelezwa na Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.), Waziri wa Katiba na Sheria wakati akifungua mkutano wa kikao kazi cha mafunzo baina ya viongozi wa Wizara na watumishi wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania yanayofanyika kwa siku tatu kuanzia leo kwenye ukumbi wa Ofisi za Bunge, Dar es Salaam

Waziri Dkt. Ndumbaro amesema kuwa LRCT ni injini ya kurekebisha sheria nchini hivyo amewataka watumishi kutambua kuwa wamebahatika kupewa jukumu la kufanya kazi kwenye Tume na amewahimiza kuzingatia maadili, sheria, taratibu na kanuni za utumishi wa umma kwa vitendo, kwa kujitoa sadaka na kutumikia cheo alichopewa ili kuwapatia wananchi huduma stahiki

“Hii ni taasisi ya umma, na siyo ya kwenu binafsi, lazima msimame kwenye sheria, taratibu na kanuni na siyo kutoka nje ya sheria, taratibu na kanuni kwa kuwa sisi wote ni watumishi wa umma na hakuna mwenye hati miliki ni muhimu mfanye kazi kwa kuzingatia uzalendo, tuchape kazi kwa bidii, tuheshimu mamlaka ili kuifanya Tume ing’ae, iendelee kuwa na thamani na kukubalika”, amesisitiza Mhe. Dkt. Ndumbaro

Naye Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bi. Mary Makondo amesema kuwa viongozi na watumishi wa Tume watapatiwa mafunzo kuhusu maadili kwa watumishi wa umma; utawala bora; na kutokomeza rushwa katika utumishi wa umma; ambapo lengo la Wizara kutoa mafunzo hayo ni kuhakikisha mafunzo hayo yanawawezesha kutekeleza majukumu yao kisheria kwa ajili ya haki na maendeleo ya taifa letu ili kuwa na uwajibikaji kwa kuzingatia maadili ya watumishi wa umma na mafunzo hayo yanatolewa na Ofisi ya Rais – Ikulu; Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora; TAKUKURU; na Sekretariati ya Viongozi ya Maadili ya Umma

Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Tume, Mwenyekiti wa Tume hiyo, Mhe. Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Januari Msofe amesema kuwa Tume imezingatia maelekezo ya Waziri Dkt. Ndumbaro hususani masuala ya maadili kwa kuwa maadili ni kila kitu, maadili ni popote iwe nyumbani, kazini na mbele ya jamii hivyo pamoja na mafunzo yaliyotolewa leo viongozi na watumishi wametambua kuwa ni muhimu kuendelea kujifunza ili kuweza kutekeleza vema majukumu na kuhudumia wananchi

Naye Katibu Mtendaji wa Tume hiyo, Casmir Kyuki ameishukuru Wizara kwa kuendeleza utaratibu wa kusimamia Tume hiyo na anaamini kupitia mafunzo hayo watumishi watatoka na mwamko mpya wa kutekeleza majukumu

Magazeti ya Tanzania Desemba 14, 2022

Walimu Arusha wakabidhiwa vishkwambi

$
0
0


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Angellah Kairuki, akikabidhi kishkwambi kwa Afisi Elimu Mkoa wa Arusha, Abeli Mtupwa kwa niaba ya walimu wa sekondari na shule za msingi kwa ajili ya kuwaongezea uwezo walimu wa kutunza kumbukumbu katika ufundishaji kwenye mkutano wa kuzindua mradi wa uboreshaji wa elimu kwa shule za msingi na sekondari mkutano uliofanyika jijini Arusha jana (Picha na Kassim Mohamed).


RAIS WA ZANZIBAR AKUTANA NA MWENYEKITI WA UVCCM TAIFA

$
0
0

 



RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Uongozi wa UVCCM Taifa ukiongozwa na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Ndg. Mohamed Ali Kawaida (kulia kwa Rais) walipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo na kumpongeza kwa kuchaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu leo 13-12-2022.(Picha na Ikulu)

  NMB yaimarisha mtaji wa rasilimali watu kupitia program ya Management Trainee

$
0
0

Wahitimu wa Programu ya Management Trainee wakiwa kwenye picha ya pamoja na Kaimu Mtendaji Mkuu wa NMB – Filbert Mponzi (kushoto), Mjumbe wa Bodi wa NMB – Ramadhani Mwikalo na Afisa Mkuu Rasilimali Watu – Emmanuel Akonaay (kulia).

 

 Programu ya Benki ya NMB ‘Management trainee’ inayotoa mafunzo kazini kwa wahitimu wa vyuo vikuu umeiwezesha taasisi hiyo kuimarisha mtaji wake wa rasilimali watu na kuisadia kuwa muajiri bora nchini.

 

Hadi sasa programu hiyo iliyoanza takribani miaka 13 iliyopita imezalisha wataalamu wa maswala ya kifedha na kibenki zaidi ya 60.

 

Wanufaika nane wa uwekezaji huo walihitimu wiki jana jijini Dar es Salaam na kuahidi kufanya kazi kwa bidii na weledi wa hali ya juu.

 

“Ndoto zetu za kuwa wataalamu wa masuala ya kibenki leo imetimia. Tunaahidi kufanya kazi kwa nguvu zetu zote kama waajiriwa wa taasisi bora na kubwa ya fedha nchini Tanzania,” Bi Amanda Eseko alisema kwa niaba ya wenzake.

 


Aidha, aliongeza kuwa miaka miwili ya mafunzo mbalimbali waliyopitia haikuwa ya lelemama. Hata hivyo, alifafanua, miaka hiyo imekuwa ya manufaa makubwa kwao kwasababu wamejifunza mambo mengi na kupata fursa ya kufanya kazi NMB na kulihudumia taifa kwa ujumla.

 

Afisa Mkuu Rasilimali Watu wa NMB, Bw Emmanuel Akonaay, alisema ana matumaini makubwa sana na vijana hao ambao hana shaka wataisaidia benki hiyo kuendelea kuwa kinara wa huduma za kifedha nchini.

 

“Kwa kipindi chote cha mafunzo yao, hawa vijana wameonyesha uwezo wa hali ya juu. Hii ni pamoja na kuweza kupata amana zenye thamani ya TZS bilioni saba na kusaidia kufunguliwa kwa akaunti mpya 5,000,” Bw Akonaay alibainisha.

 

Mgeni rasmi ambaye alikuwa ni Mjumbe wa Bodi wa NMB, Bw Ramadhani Mwikalo, aliyesema kuwa uendelezaji wa vipaji kama huo ni moja ya vitu vinavyofanya NMB kuwa mwajiri bora na kinara nchini, na kuwa na wafanyakazi wenye ujuzi na weledi mkubwa, ndiyo rasilimali namba moja ya benki hiyo na mtaji unayoifanya kuongoza sokoni.

 

Awali, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Bw Filbert Mponzi, aliwaambia wahitimu hao kuwa kuajiriwa na mwajiri bora Tanzania ni kuwa sehemu sahihi na katika mikono salama kiajira.

 

Ili wafanikishe, alibainisha, ni lazima wazingatie kupata matokeo chanya katika kila wanalolifanya kwani hiyo ndiyo siri ya kufanikiwa kwa watu kama yeye ambao walianzia ngazi za chini walipoajiriwa NMB.

  WAZIRI MKUU AIAGIZA TAKUKURU IWACHUNGUZE WATUMISHI WAWILI KATAVI

$
0
0

*Amuagiza Mkuu wa mkoa kusimamia vizuri Idara ya Ardhi kuanzia ngazi ya mkoa

 

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa {TAKUKURU} mkoa wa Katavi awachunguze watumishi wawili akiwemo Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Mazingira Mpanda {MUWASA}, Hussein Nyemba  kwa tuhuma za kukiuka taratibu za manunuzi ya umma.

 

Mwingine ni Afisa Mipango Miji wa Halmashauri ya wilaya ya Tanganyika Bw Abraham Casto ambaye anadaiwa kujipatia ardhi katika vijiji mbalimbali bila ya kufuata taratibu za kisheria na kusababisha migogo ya ardhi baina yake na wana vijiji. Watumishi wote hao wawili wamesimamishwa kazi kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili.

 

Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo jana (Jumatatu, Desemba 12, 2022) alipozungumza na watumishi wa Halmashauri za Mpanda, Nsimbo na Tanganyika katika ukumbi wa Mpanda Social Hall akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa mkoani Katavi. Amewasisitiza watumishi wa umma kuwatumikia wananchi ipasavyo.

 

Pia Waziri Mkuu ameiagiza TAKUKURU ichunguze ununuzi wa pikipiki 30 zilizonunuliwa Jijini Dar es Salaam kwa gharama ya sh. milioni 3.8 kila moja huku wilayani Mpanda pikipiki moja inauzwa sh. milioni 2.7, pia ununuzi wa mita za maji 1,000 uliofanywa bila ya kukaguliwa na TBS pamoja na ajira ya watumishi 25 alizoajiri bila kibali.

 

“Rais Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema hatomvumilia mtumishi yeyote ahakikishe anasimamia majukumu yake. Watumikieni wananchi bila ya kuwabagua, sisi ni wahudumu wa wananchi lazima tufanye kazi na pangeni muda wa kuwafuata katika maeneo yao na kusikiliza kero zao na kushirikiana nao katika kuzipatia ufumbuzi.”

 

Kadhalika, Mheshimiwa Majaliwa ametumia fursa hiyo kumuagiza Mkuu wa Mkoa wa Katavi ahakikishe Idara ya Ardhi kuanzia ngazi ya mkoa hadi wilayani inasimamiwa vizuri. “Idara ya ardhi mkoa ijitathmini migogoro ni mingi na haishughulikiwi ipasavyo. Wananchi wana migogoro mingi ya ardhi.”

 

Mheshimiwa Majaliwa ametoa agizo hilo ikiwa ni utekelezaji wa maagizo Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Ndugu Abdulrahman Omari Kinana aliyoyatoa alipokuwa katika ziara ya kikazi mkoani Katavi tarehe 25 Julai, 2022.  Miongoni mwa maagizo aliyoyatoa ni pamoja na kuitaka  idara ya ardhi mkoa wa Katavi itazamwe kutokana na kugubikwa na rushwa na ujanja ujanja.

 

Hata hivyo, Waziri Mkuu amewaagiza wakuu wa Idara katika Halmashauri kwa kushirikiana na Madiwani waibue vyanzo vipya vya mapato na wahakikishe wanafahamu kiasi cha fedha kinachokusanywa katika kila eneo badala ya kuweka makadirio

 

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ametoa muda wa mwezi mmoja kwa watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Tanganyika ambao wanaishi katika Halmashauri ya wilaya ya Mpanda wakiwemo baadhi ya wakuu wa Idara wawe wamehamia Tanganyika ifikapo Januari 15, 2023 ili waweze kuwahudumia wananchi ipasavyo.

 

Pia, Waziri Mkuu ameagiza mkataba wa mradi wa kuzalisha hewa ukaa ambao unahusisha misitu ya vijiji vinane yenye ukubwa wa hekta 216,944 za ardhi na wakazi 34, 242 katika wilaya ya Tanganyika ukafanyiwe uchunguzi kwa mwanasheria ikiwa ni pamoja na kupitia masharti yaliyowekwa.

 

  WAZIRI MKUU AZINDUA KIWANDA CHA KUCHAKATA MAZIWA NSIMBO

$
0
0

* Kiwanda hicho kina uwezo wa kusindika wastani wa lita 10,000 kwa saa

 

 

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezindua kiwanda cha kuchakata maziwa cha MSS kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo, Mkoani Katavi ambacho kina uwezo wa kusindika wastani wa lita 10,000 kwa saa.

 

Akizungumza baada ya kuzindua kiwanda hicho ambacho uwekezaji wake umegharimu shilingi milioni 600, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Rais Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amedhamiria kuendelea kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji ili kila mwenye uwezo awekeze.

 

Amesema hayo leo {Desemba 13, 2022} wakati akizungumza na wananchi baada ya kuzindua kiwanda hicho ambacho kwa sasa kinazalisha maziwa ya mtindi na maziwa fresh na kinatarajia kuanza uzalishaji wa Samli hivi karibuni.

 

Pia, Mheshimiwa Majaliwa ametoa rai kwa wafugaji wanaozunguka kiwanda hicho kuuza maziwa kwa mwekezaji huyo ili waweze kujiongezea kipato na kumwezesha mwekezaji huyo kuwa na uhakika wa malighafi ya kutosha.

 

“Huyu Bwana Maliki anamuunga mkono Rais Mheshimiwa Dkt. Samia katika nia yake ya kuendeleza uwekezaji nchini. Uwepo wa kiwanda hiki kunaisaidia kuendeleza  mkakati wa lishe bora kwa kila Mtanzania, kwa sasa tunamshauri aendelee kupanua kiwanda hiki ili aongeze uzalishaji na wananchi wengi wazidi kupata ajira.”

 

Awali, Waziri Mkuu aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi inayojengwa katika eneo la Ilembo, Mpanda, ambapo alieleza kuwa Serikali ya Awamu ya sita imeendelea na mkakati wa kupeleka huduma karibu na wananchi kwa kuhakikisha inajenga majengo ya ofisi ya mikoa na wilaya mpya  Katavi ukiwemo.

 

Aidha,alitumia fursa hiyo kuwahakikishia wananchi kwamba Serikali yao itaendelea kuwatumikia, hivyo waendelee kuiamini na kuiunga mkono. “Serikali itaendelea kuwatumikia na haitowaangusha sisi wasaidizi wa Rais Mheshimiwa Dkt. Samia tutafanya kazi wakati wote, wakati wa jua kali na hata wakati wa mvua, tunataka kuhakikisha dhamira ya Rais wetu ya kuleta maendeleo inatimia.”

 

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega alisema kuwa Rais Dkt. Samia ameridhia kutoa shilingi milioni 200 kupitia Bodi ya Maziwa kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha ukusanyaji wa maziwa Mpanda, Katavi. “Vituo hivi vitajengwa takribani kumi nchi nzima na kila kimoja kitagharimu shilingi milioni 200.”

 

Ameongeza kuwa Rais Dkt. Samia ametoa fedha kwa ajili ya ununuzi wa mitamba ya maziwa 500 na madume ya nyama 500 ambayo yatagawiwa nchi nzima, lengo likiwa ni kuboresha aina ya mifugo inayofugwa na wananchi. “Serikali inataka wananchi wafuge kisasa na kibiashara.”

 

Naye, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Geofrey Pinda alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini {DPP} kufanya mapitio ya kesi na  majalada mbalimbali ili yasiyokuwa na mashiko au ushahidi wa kutosha yaondolewa ili wahusika  wakaendelee na shughuli za uzalishaji mali.

 

WAZIRI JENISTA AMTEMBELEA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS NA WAZIRI MKUU MSTAAFU, CLEOPA MSUYA

$
0
0

 


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama akimsalimia Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Cleopa Msuya alipomtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam.


                   

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama akifafanua jambo kwa Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Cleopa Msuya alipomtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam. 



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama akimsikiliza Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Cleopa Msuya alipomtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam.



Wanawake Mafia wapongezwa

$
0
0

WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake, na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima amewapongeza Wanawake wilayani Mafia kwa kuandaa Kongamano la kuhitimisha wiki ya maadhimisho ya mapambano dhidi ya ukatili kwa wanawake na watoto.

“Nimefurahishwa sana kwa jinsi mlivyojitokeza kuungana kupaza sauti zetu kupinga kwa dhati matukio ya kikatili wanayofanyiwa wanawake na watoto”

Dkt. Gwajima ameyasema hayo wakati akifungua Kongamano lililoandaliwa na wanawake kisiwani Mafia ikiwa ni kilele cha maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili kwa wanawake na wasichana Duniani.


Maadhimisho ya kupinga ukatili kwa wanawake na wasichana hufanyika kila mwaka kuanzia  Novemba 25 hadi tarehe Desemba 10.

 WATENDAJI WIZARA YA ELIMU, WAASWA KUJIVUNIA JUHUDI ZAO

$
0
0


Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Tekinolojia Dkt, Francis Michael (kulia), akizungumza wakati akifungua kikao kazi cha Watendaji Wakuu wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Elimu Sayansi na Tekinolojia kilichofanyika jijini Dar es Salaam leo Desemba 14, 2022.

 

 Na Mwandishi Wetu

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Tekinolojia Dkt, Francis Michael, amewaasa watendaji wa Wizara hiyo kujivunia juhudi zao binafsi ambazo zimekuwa chachu ya Wizara hiyo kufanya vizuri.

Ameyasema hayo leo wakati akifungua kikao kazi cha Watendaji Wakuu wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Elimu Sayansi na Tekinolojia kinachofanyika katika ukumbi wa Wizara, Dar es Salaam.

"Ndugu viongozi, kikao hiki kimetuleta pamoja Wakuu wa taasisi zilizo chini ya Wizara yetu, ambao ndio Watendaji na watekelezaji Wakuu wa miongozo, sera na mipango tunayojiwekea Wizara katika kufikia malengo yaliyoainishwa na Dira ya maendeleo ya Taifa, Ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

"Lengo la kikao kazi hiki ni kubadilishana uzoefu, kujifunza kupeana mbinu mbadala na weledi katika namna bora kipindi hiki ambacho Wananchi wana hamasa kubwa ya kutaka kufahamu mambo mbalimbali ambayo serikali inayatekeleza." amesema na kuongeza kuwa.

"Miongoni mwa mambo niliyoyaona ambayo taasisi zenu hazifanyi vizuri ni kueleza Wananchi juu ya mambo mazuri tunayoyafanya. Mnafanya mambo mengi mazuri lakini mpo kimya sana. Mara nyingi nawaona mkijitokeza kujibu malalamiko ya Wananchi lakii siwaoni mkitumia vyombo vya habari kujitagaza hasa kwenye mambo ambayo yanawapa heshima na kuwaongezea sifa.

"Ndugu viongozi nyinyi mmeshika hatma ya Taifa na kwa kipindi chote mmemudu kutekeleza majukumu yenu kikamilifu tena kwa ubunifu, kuna taasisi kutokana na asili ya shughuli zake lazima kila  mwaka waje na mbinu za za kibunifu. Mbinu zenu ndio zinazotuvusha kila mwaka." amesema.

Hata hivyo amewasisitiza kuwa lazima kuwaambia Wananchi juu ya namna wao kama Watendaji wanaumiza vichwa vyao kwa ajili ya maendeleo yao.

" Kweli watu wanapoona haya yote yanatokea lazima waambiwe kuwa watu waliumiza vichwa kufanikisha hayo. Na watu hao ndio ninyi.

"Leo kikao hiki ni kikao cha ndani baina yetu lakini natamani tuwe na kikao cha kutangaza mafanikio yetu, tuite vyombo vya habari ikiwezekana tuwe mubashara kuileza Dunia nini tunafanya." amesema Dkt Francis Michael


Miss Afrika akabidhiwa bendera

$
0
0

Akimkabidhi Bendera ya Taifa katika ofisi za BASATA jijini Dar es Salaam Desemba 13/12/2022, Katibu Mtendaji wa BASATA,Dkt.Kedmon Mapana alimtakia ushiriki mwema Miss Africa Calabar 2022 Eng. Nancy Matta katika shindano hilo litafanyika Nchini Nigeria tarehe 27/12/2022 ambalo litarushwa moja kwa moja kupitia chaneli ya DSTV.

Dkt Mapana amemtaka Mrembo huyo kuzingatia nidhamu kwani kwa kufanya hivyo kutamsaidia kupiga hatua kubwa katika shindano hilo na hatimaye kuibuka mshindi.

Naye Miss Africa Calabar 2022 Eng. Nancy Matta amewaahidi Watanzania kuwa,matarajio yake ni  kufanya vizuri kutokana na maandalizi mazuri aliyoyafanya kupitia usimamizi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) pamoja na wadau wengine wa Sanaa Nchini tanzania.

Huu ni Msimu wa Sita tangia kuanzishwa kwa shindano hilo la Miss Africa Calabar na litafanyika katika mji wa Calabar nchini Nigeria tarehe 27/12/2022 .

Magazeti ya Tanzania Desemba 15, 2022

 Wananchi Bunda wamlilia Rais Samia

$
0
0

NA MWANDISHI WETU

 

WANANCHI zaidi ya 13,000 wa vijiji vinne vya Kata ya Nyatwali Wilaya ya Bunda wameulalamikia uongozi wa wilaya hiyo kwa kile wanachodai kutumia jina la Rais Samia Suluhu Hassan kutaka kuwapora maeneo yao.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi mara baada ya kikao kuvunjika wananchi hao walisema Katibu Tawala wa Wilaya (DAS) Salimu  Cherera anataka wananchi hao waondoke kwa madai kuwa amepokea waraka kutoka kwa Rais Samia ukiwataka wakazi hao waondoke mara moja.

“Katibu Tawala Cherera alikuja kama mlivyoshuhudia kwenyewe kikao amesema kuwa Rais ameandika waraka wa kutaka wakazi wa vijiji vinne vya Kata ya Nyatwali ambavyo ni Kariakoo, Tamau, Serengeti na Nyatwali kuondoka mara moja”. Alisema Diwani wa Kata ya Nyatwali Malongo Mashimo.

Aliendelea kusema “Sisi wananchi wa vijiji hivi tunaonewa na kutishiwa maisha na ofisi ya Mkuu wa Wilaya kupitia Katibu Tawala na genge lake, ambapo Desemba 8,2022 Katibu Tawala huyo aliambatana na kundi la askari Polisi pamoja na  mwekezaji bila kuwepo diwani wa Kata ya Nyatwali na kuitisha kikao kibabe na akawa mwenyekiti wa kikao hicho”.

Diwani Malongo alisema Katibu Tawala huyo aliendesha kikao hicho na ajenda kuu ilikuwa ni Rais Samia ameagiza watu wote wa Kata ya Nyatwali kuondoka mara moja katika maeneo yao.

“Baada ya tamko hilo uongozi wa kata ulianza kuhoji kwa nini Katibu Tawala aendeshe kikao kwa niaba ya Diwani wakati si utaratibu, pia polisi wengi kiasi hiki kwani kuna vita?

Tuliomba kuonyeshwa waraka huo unaodaiwa umetoka kwa Rais Samia, lakini Katibu Tawala  alituambia kuwa sisi kwa vyeo vyetu haturuhusiwi kuonyeshwa nyaraka za Serikali”. Alisema Malongo.

Diwani Malongo alisema Desemba 12,2022 kilifanyika kikao cha viongozi wa Kata alichokiandaa  yeye kwa agizo la Katibu Tawala ambapo DAS alifika na timu yake na baadhi ya maafisa aliodai wametoka Ikulu kwa madai kuwa wametumwa na Rais Samia hakuwatambulisha kwa majina na aliwaagiza viongozi wote wa Kata kuzima simu zao na kwamba akigundulika mmoja ajazima atachukuliwa hatua kali.

“Ajenda ya kikao ilisomwa na Katibu Tawala kuwa amekuja na timu yake kutufahamisha agizo la Rais Samia la kutuhamisha, viongozi tuliomba tuonyeshwe waraka huo, ambapo DAS alitoa waraka wa maelekezo ya nchi ya jumla ambayo yanataja namba ya (Stiki) ambapo sisi viongozi wa Kata tulianza kuhoji ni wapi kwenye waraka huo kata ya Nyatwali na vijiji vyake vinne imeajwa? Kikao kikavunjia watu wakatawanyika” Alisema Diwani Malongo.

Nao wazee wa Kata hiyo wakiongozwa na Mwenyekiti Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Bunda Alfredi Malagira (80) Pamoja na Katen Mstaafu Richard Chacha wao wamesema watapigania haki ya wakazi wa Nyatwali mpaka mwisho kwani jambo hilo lilianza tangu mwaka 2002 lakini dhuruma hiyo ilidhibitiwa na Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda Mei 12,2014 kwa barua No PM/P/1/569/15.

Waliendelea kusema kuwa kana kwamba hiyo haitoshi Rais John Pombe Magufuli alizuia dhuruma hiyo kwa barua iliyoandikwa  Januari 15,2019 na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu na kusainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu wakati huo Gerson Msigwa.

Naye Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Alfredi Malagira  alisema wanashangaa uongozi wa Wilaya kuja na suala hili kwa kutumia nguvu kubwa ya polisi na maneno ya kumsingizia Rais Samia kuwa kaagiza wananci  kuondolewa katika eneo hilo.

“Kutokana na hali hiyo tumefunga safari kutoka Bunda kuja Dar es Salaam kumuona  Makamu Mwenyekiti wa CCM Abrulhaman Kinana ili atupeleke kwa Rais Samia kufikisha kilio chetu hiki”.Alisema Malagira.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii Katibu Tawala wa Wilaya ya Bunda  Salimu  Cherera alisema kuwa “Sisi tunaendesha vikao na wananchi wa eneo husika hatuzungumzi na watu wengine watafute wao watakueleza kinachoendelea.

“Sisi tunaheshimu sana vyombo vya habari kama unataka kujua suala hili funga safari kuja Bunda tutakupa ufafanuzi kwanini tunataka kuwahamisha”. Alisema Cherera.

Juhudi za kumpata Mkuu wa Wilaya ya Bunda Joshua Nasari zimegonga mwamba kwa takriban wiki mbili sasa kutokana na simu yake kutokupokelewa.

.

 NI VITA YA MESSI NA MBAPPE FAINALI KOMBE LA DUNIA QATAR

$
0
0


Na Mwandishi Wetu

HATIMAYE imejulikana, ni vita ya Mwanaume dhidi ya Mvulana aliyekoma yaani Lionel Messi dhidi ya Mbappe ni baada ya hapo jana Mabingwa watetezi wa kombe la Dunia kureje tena Fainal kwa mara ya pili mtawalia.

Ufaransa ambao ndio Mabingwa watetezi wakitwaa taji hilo 2018 pale Urusi sasa wanalitaka tena baada ya kuwaondosha Morocco katika hatua ya Nusu Fainali kwa mabao (2-0).

Wakati Argentina wao waliwazima Croatia kwa mabao (3-0) hapo juzi, sasa nani kutwaa mwali jumapili hii? Ni vita ya Mwanaume dhidi ya Mvulana aliyekomaa.


Licha ya ubora wa Morocco Ufaransa wanajua jinsi ya kutumia nafasi zao , walipiga mashuti mawili tu yaliyolenga lango na yote yakazama nyuni , na wanajua kucheza kitimu hasa wakiwa hawana mpira.

Bila mpira Ufaransa wanakuwa umbo la 4-5-1 , tena ni Giroud ndio anarudi mpaka karibu na Griezman na kumuacha Mbappe peke yake mbele tena pembeni ya uwanja mahususi kwa ajili ya mashambulizi ya kushitukiza na ya kujibu, Deschamps akiamini atabaki dhidi ya mabeki wawili tu tena wa kati

Kocha wa Morocco, Regragui aliamua kuanza na mabeki watatu , ili kuwapa athari chanya 'wingbacks' wake ( Hakimi na Mazraoui ) nafasi ya kushambulia zaidi , kuwarudisha nyuma Mbappe na Dembele wakati huo huo kuwapa nafasi nzuri Ziyech na Boufal kushambulia ndani zaidi badala ya kukabiliana dhidi ya Kounde na Hernandez ... mpaka pale Saiss alipoumia

Kipindi cha pili, ndio Morocco walitandaza kandanda safi tangu kuanza haya mashindano hasa wakiwa na mpira ... nini Regragui alifanya ?

Kutengeneza idadi kubwa ya wachezaji pembeni ya uwanja ... kwanini ? Kwasababu Mbappe na Dembele sio wazuri kuzuia kwahiyo Kounde na Hernandez watakuwa wazi sana dhidi ya mikimbio ya Atalah , Boufal na Amallah kushoto , Hakimi Ounahi na Ziyech kulia huku Amrabat anabaki kama namba 6 pekee mbele ya mabeki wawili wa kati

Shida yao ilikuwa Konate na Varane , kila wakipiga krosi Morocco mabeki wawili wa kati wa Ufaransa walikuwa bora sana kwenye kukabiliana nayo.

Hivo ndo fuutiboli ya Dunia huchezwa na timu kubwa Ufaransa wakaibuka washindi kwa ubora wa mchezaji mmoja mmoja na timu kwa ujumla.


Sasa imebaki michezo miwili kuhitimisha makala ya 22 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1930, mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu kati ya Croatia dhidi ya Morocco na Fainali ya Argentina dhidi ya Ufaransa.

 Mfuko wa Sanaa Wapata Vifaa, Dkt. Abbas Aongoza Maandalizi Tuzo za Muziki 2022

$
0
0


Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi leo Desemba 13, 2022 amekagua na kukabidhi vifaa vya kisasa vitakavyotumiwa na Ofisi ya Mfuko wa Maendeleo ya Utamaduni na Sanaa.


Dkt. Abbasi amekabidhi vifaa hivyo kwa  Mratibu wa Mfuko huo Mfaume Said ikiwa ni juhudi za Wizara hiyo chini ya Waziri Mohamed Mchengerwa, kuuwezesha Mfuko kuanza kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi zaidi katika sekta hizo.


Mfuko huo umetengewa kiasi cha shilingi Bilioni 3.9 kwa Mwaka wa Fedha 2021 hadi 2023 na vifaa hivyo vitakapofika vyote vitagharimu TZS milioni 90.

Katika hatua nyingine, Dkt. Abbasi ameongoza kikao cha Bodi ya Baraza la Sanaa nchini (Basata), ambapo miongoni mwa nyaraka zilizojadiliwa ni Mwongozo wa Maadili kwa Wasanii na Mwongozo wa Maandalizi ya Tuzo za Muziki (TMA) za mwaka 2022 lakini zitatolewa April, 2023.



Ametumia fursa hiyo kuwaagiza watendaji kadhaa wapya waliohamishiwa Basata kutoka taasisi mbalimbali za umma ikiwa ni sehemu ya maboresho na wale wa zamani kuendeleza umoja na ubunifu kwani sekta ya sanaa ni moja ya sekta za kimkakati kwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Viewing all 19659 articles
Browse latest View live