Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all 19659 articles
Browse latest View live

Daah! Masikini Celine Dion

$
0
0

Celine Dion akiwa na Drake.

 

Mwanamziki wa R&B kutoka nchini Canada, Celine Dion (54), ameweka wazi hali ya afya yake kwa kusema amegundulika kuwa ana ugonjwa usiotibika unaofahamika kama Stiff Person Syndrome (SPS), ambao ni ugonjwa wa neva.

Celine Dion alitoa taarifa hiyo kupitia akaunti yake ya Instagram kuwa, ugonjwa huo unaifanya misuli yake isimame bila kudhibitiwa na amekuwa akikabiliana na ugonjwa huo kwa muda mrefu.



Mara kadhaa ugonjwa huo umesababisha Celine kushindwa kutembea na hata  kuimba, hali itakayomlazimu pia  kuahirisha kushiriki kwenye  maonesho yaliyopangwa kufanyika Ulaya  mwezi Februari mwaka 2023.


"Hivi majuzi nimegunduliwa kuwa na ugonjwa wa nadra sana wa Neva unaoitwa Stiff Person Syndrome ambao kwa wastani huathiri mtu mmoja kati ya watu milioni moja'' alisema Celine




R Kelly aachia album akiwa gerezani

$
0
0

 Mwanamuziki wa RnB kutoka nchini Marekani Robert Sylvester Kelly 'R Kelly' (55), ameachia album yake ya kwanza akiwa gerezani.


Msanii huyo anatumikia kifungo cha miaka 30 gerezani kwa makosa mbalimbali ya unyanyasaji wa kingono kwa watoto wenye umri mdogo.
Album hiyo ya R Kelly aliyoipa jina la 'I ADMIT IT' ina jumla ya ngoma 13.

TANZANIA KUNUFAIKA NA DOLA BILIONI 1 KUTOKA KOREA

$
0
0

 

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akiipongeza Korea kwa kutoa misaada na mikopo yenye mashariti nafuu kwa Tanzania, wakati wa mkutano kati yake na Waziri Ofisi ya Uratibu wa Sera wa Korea, Mhe. Moon-Kyu Bang (hayupo pichani), jijini Dodoma, kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Emmanuel Tutuba.


 
 Na Peter Haule, WFM, Dodoma

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Korea kwa kutenga kiasi cha dola za Marekani bilioni 1 zitakazotolewa kwa njia ya mkopo nafuu kwa Tanzania kupitia Mfuko wa  Shirika la Maendeleo ya Kiuchumi (EDCF), kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa kipindi miaka mitano

Dkt. Nchemba ametoa shukrani hizo jijini Dodoma, alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri anayesimamia uratibu wa masuala ya Sera wa Korea Mheshimiwa Moon-Kyu Bang, alipokutana na kufanya mazungumzo naye akiwa katika ziara ya kikazi nchini.

“Septemba mwaka 2022, Tanzania na Korea tulisaini makubaliano yatakayoiwezesha Tanzania kupata mkopo wenye riba nafuu wenye thamani ya dola za Marekani  bilioni moja ambapo Tanzania itakopa mkopo huo kwa riba ya asilimia 0.01 kwa mwaka na kuulipa kwa kipindi miaka 40 ambacho kimeambatana na kipindi cha neema cha miaka 15.” alisema Dkt. Nchemba

Dkt. Nchemba aliishukuru Korea kwa kuahidi pia kusaidia utekelezaji wa miradi miwili mipya ukiwemo mradi wa maji na usafi wa mazingira mkoani Iringa wa Iringa na ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Binguni-Zanzibar, ambayo italeta manufaa makubwa kwa wananchi.

Alisema kuwa Wizara na Serikali kwa Maelekezo na mwongozo wa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, ipo tayari kushirikiana na timu ya Serikali ya Korea na wawakilishi wa Benki ya Exim nchini kuweza kukamilisha kwa haraka taratibu zote za kitaalamu ili miradi hiyo iweze kutekelezwa.

Aidha Dkt. Nchemba, amezikaribisha Kampuni za Jamhuri ya Korea kuwekeza nchini ukiwemo uwekezaji wa ubia katika miundombinu wezeshi ikiwemo ya barabara, nishati, afya, usafiri wa majini na Tehama.

Dkt. Nchemba alisema kuwa Serikali ya Tanzania ina fursa nyingi za uwekezaji kwa kuwa ni lango la nchi nchingi zikiwemo za Afrika Mashariki na kusini mwa Afrika na pia ina mazingira bora ya uwekezaji na ufanyaji biashara.
 
Pia alibainisha kuwa ushirikiano kati ya Tanzania na Korea ni wa kirafiki na kindugu, ikizingatiwa kuwa Serikali ya Korea iliwezesha Tanzania kupata fedha za kutekeleza miradi mingi ukiwemo mradi wa ujenzi wa daraja la Tanzanite jijini Dar es Salaam.

Kwa upande wake    Waziri Ofisi ya Uratibu wa Sera wa Jamhuri ya Korea, Mhe. Moon-Kyu Bang aliahidi kuwa mradi wa kuboresha usambazaji maji na mazingira wa Iringa uamuzi wake wa kuutekeleza utafanyika mwishoni mwa mwaka huu na utekelezaji utaanza mara moja ilihali mradi wa Hospitali ya Rufaa ya Binguni  Zanzibar, taratibu za kitaalam zitakamilishwa ndani ya miezi sita ili utekelezwe. 

Vilevile ameeleza kuwa Korea inampango wa kuongeza zaidi ya marambili kiwango cha bajeti ya kutoa misaada kwa Afrika hadi kufikia mwaka 2030, hivyo ameitaka Tanzania kuandaa miradi ambayo itatekelezwa katika mpango huo utakapoanza ikiwemo miradi ya ubia na Sekta binafsi katika maeneo ya barabara, reli na mingine.

Mhe. Bang aliipongeza Serikali kwa kutekeleza mradi wa kimkakati wa reli ya kisasa ambao amesema ni kubwa na utasaidia kuinua uchumi wa nchi na nchi Jirani na kuahidi kuwa atazishawishi kampuni kutoka nchini mwake kushiriki katika mradi huo kwa njia ya utaratibu wa ubia kati ya umma na sekta binafsi.


BRAZIL WAKUTANA NA NDOIGE YA CROATIA, ARGENTINA WATINGA NUSU FAINALI

$
0
0


 

 Na Mwandishi Wetu

Timu ya Taifa ya Brazil imeondoshwa katika Fainal za Kombe la Dunia kwa mikwaju ya penati (4-2) na Croatia mchezo wa hatua ya Robo Fainali.

Licha ya matarajio makubwa ya wapenda soka kote Ulimwenguni bado kazi ilikuwa ngumu kwa wafalme hao wa Soka Duniani.

Croatia waliamua kuzuia kwa ufanisi , wakaziba mianya  katikati ya uwanja , waache Brazil wapige krosi kama wanaweza.

Wakipata mpira waligoma kubutua , uwepo wa viungo wao watatu mafundi Modric Kovacic na Brozovic walifanya Brazil wautafute mpira sana na ule ndio ulikuwa muda wa kupumzika kwa Croatia ( kumiliki mpira ) kwasababu kwenda mbele hawakuwa na hatari sana

Baada ya ufundi wa Neymar , kufunga goli ...Brazil walipoteza nidhamu ya uzuiaji , una viungo wawili wakabaji uwanjani ( Casemiro na Fred ) na bado shambulizi la kushtukiza la Croatia ilionekana Brazil wapo wazi sana mpaka ilifika hatua nyuma wamebaki watatu dhidi ya watatu wa Croatia ... pale Tite hatowaelewa wachezaji wake na kocha wa Croatia kamari ya kuingiza washambuliaji wengi itakuwa imemlipa

Mechi ilikuwa taratibu sana , hakuna timu ambayo ilikuwa inaweka presha kwenye mpira , wachezaji wanagusa mpira mara nyingi sana , kupoteza mpira kirahisi ( na hili kosa halikuadhibiwa sana )
 
Livakovic amefanya saves 10 katika mechi moja hiyo ni rekodi katika mashindano haya mwaka huu mpaka sasa kufanya saves 10 katika mechi moja na bado aliokoa penati moja

Modric Brozovic na Kovacic wakiamua kutawala mpira ... utajuta na Kaburi la Brazil lilichimbwa hapa  


Dakika 120 hakuna mbabe na mikwaju ya penati inawaondosha Brazil na kuiaga michuano ya Kombe la Dunia pale Qatar.

Robo Fainali nyingine ilikuwa ya Uholanzi dhidi ya Argentina mtanange ulitamatika kwa Argentina kutinga hatua ya Nusu Fainali kwa mikwaju ya penati baada ya sare ya mabao (2-2) katika dakika 120.

Michezo mingine itapigwa Leo ambalo wawakilishi wa Afrika Morocco watawakabili Ureno huku vita nyingine itakuwa kwa England dhidi ya Ufaransa.

George Mpole amalizana na Geita Gold

$
0
0


Aliyekuwa mshamuliaji wa Geita Gold, George Mpole amesema kwa sasa anaangalia changamoto nyingine baada ya kumalizana na timu yake ya zamani.


"Kila kitu kikiwa poa nitaweka wazi wapi nakwenda, hivi sasa ni mapema kuitaja timu, lakini ipo na nimeshamalizana nayo, kuna baadhi ya vitu nikivikamilisha kila kitu kitakuwa wazi.

Aidha Mpole amesema "Sikuwa na shida Geita Gold maana pale ni nyumbani, muda umefika wa mimi kuondoka".

"Nashukuru nimemalizana nao vizuri, kuachana kwa wema ni jambo jema maana huu ni mchezo wa maslahi, sina ninachowadai na hawana wanachonidai " alisema George Mpole.

Sakata la George Mpole na klabu yake limeanza kufukuta tangu Oktoba 13, mwaka huu baada ya mchezo wa raundi ya saba ambapo nyota huyo hakuungana na wenzake kwa maandalizi ya michezo iliyofuata.

Mpole hakuonekana kambini kwenye michezo mbalimbali ya timu hiyo kwa kile alichoeleza kuumwa na yuko nyumbani kwao mkoani Mbeya anatibiwa kwakuwa madaktari wa timu hiyo wameshindwa kumpa tiba huku baadhi ya taarifa zikidai mshambuliaji huyo anadai stahiki zake za mshahara wa mwezi wa 10.

Hata hivyo, Novemba 17, mwaka huu klabu yake ilimpa wiki moja ya kuripoti kwenye kituo cha kazi ili kuendelea na program za timu na kama angeshindwa kuhudhuria angechukuliwa hatua kali za kinidhamu, baada ya kutoonekana kwa muda mrefu huku uongozi ukiwa hauna taarifa yoyote.

Mpole alirejea Geita kujiunga na timu hiyo ambapo Desemba 4 alikuwa sehemu ya kikosi cha timu hiyo kilichocheza dhidi ya Mtibwa Sugar na kulazimishwa sare ya 2-2 katika Uwanja wa Nyankumbu huku akiishia benchi.

 

Gwiji wa muziki wa Dansi afariki Dunia

$
0
0

Mwanamuziki mkongwe wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Elizabeth Tshala Muana Muidikay maarufu kama TSHALA MUANA amefariki dunia Jumamosi Desemba 10, 2022.


Kwa mujibu wa vyanzo vya habari vya Congo, Muana alifariki mjini Kinshasa akiwa na umri wa miaka 64.

Mume wa marehemu, Claude Mashala, alithibitisha kifo chake katika chapisho la Facebook.


"Mapema asubuhi ya leo, Bwana mwema alichukua uamuzi wa kumchukua Mama wa Taifa Tshala Muana. Mungu mwema atukuzwe kwa nyakati zote njema alizotujalia hapa duniani. Kwaheri Mama kutoka kwa M,"ameandika Mashala.

Mashala hakutoa maelezo kuhusu chanzo cha kifo chake.


 

Marehemu Tshala Muana alipata umaarufu barani Afrika kwa nyimbo kadhaa zilizovuma kila pembe sambamba na mtindo wa Mutuashi.

Nyimbo "Dezo Dezo" ya Ndala Kasheba na nyingine za Kiswahili ya "Karibu yangu", "Tshibola" na nyingine zilimpa umaarufu sana Tanzania ambako alizuru mara kadhaa miaka ya 80 na 90.

WAKILI MPANJU AWAPA MAJUKUMU JUKWAA LA KITAIFA LA MALEZI MBADALA

$
0
0


 Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Wakili Amin Mpanju akifungua kikao cha Siku tatu cha Jukwaa la Malezi Mbadala lilikutana mjini Morogoro kwa ajili yakuweka Mikakati ya Malezi Mbadalakuanzia Disemba, 08-10, 2022

 

Na WMJJWM, Morogoro

 

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Wakili Amon Mpanju, alimelitaka Jukwaa la Kitaifa la Malezi mbadala kutoka na mbinu itakayosaidia kuwanusuru watoto wanaopitia madhila mbalimbali katika hatua za makuzi na kujikuta wapo eneo la Malezi Mbadala.

 

Wakili Mpanju ametoa wito huo leo Disemba 09, 2022 wakati akifungua kikao kazi kati ya Serikali na wadau mkoani Morogoro.

 

Mpanju amemtaka Kamishana wa Ustawi wa Jamii, kuhakikisha Jukwaa hilo linakuwa na Uongozi utakaowezesha kuwakutanisha mara mbili kwa mwaka kwa ajili ya kuona ni mikakati ipi itakayosadia kwenye suala la Malezi Mbadala.

 

“Kamishna hakikisha Jukwaa hili linasimamiwa ipasavyo, hakikisheni, linakutana Mara mbili kwa Mwaka, tengenezeni Muundo, wekeni Mikakati na Mbinu zipi zitumike kuboresha Malezi ya Mtoto, aidha mhakikishe Jukwaa likafika hadi ngazi ya Vijiji na Mitaa” amesema Mapanju.  

 

Katika hatua nyingine Wakili Mpanju ametaka suala la Malezi Mbadala liwe ni suala la mpito, kwani anaamini kuwa kila Mtoto aliye ndani ya Jamii ana mlezi wake hivyo Jamii isichululie suala la Malezi Mbadala kama ndio suluhisho la kudumu.

“Sheria ya Mtoto Na. 21 ya Mwaka 2009 iliyofanyiwa marekebisho Mwaka 2019, kifungu cha 16 na 144. Watoto wanaohitaji huduma ya Malezi mbadala ni Watoto wanaoishi katika Makao ya Watoto na Watoto waliokinzana na Sheria, Watoto wanaoambatana na mama zao Gerezani, Watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani au wanaombata na mzazi/mlezi ambaye anaomba mitaani, Watoto wanaoishi katika familia ambazo mkuu wa kaya ni mtoto, Mtoto anayeishi na mtu ambaye ni mgonjwa, mlemavu au mzee ambaye anashindwa kukidhi mahitaji ya msingi, Watoto walio katika hatari ya kufanyiwa ukatili wakiwepo wahanga wa usafirishaji haramu wa binadamu” amesema Mpanju.

 

Wakili Mpanju ameongeza kuwa Serikali imeendelea kushirikiana na wadau mbali mbali katika utoaji wa huduma ya malezi mbadala.

 

“Hadi sasa jumla ya Mkao ya watoto 325 yamesajiliwa yakiwemo mawili  ya Serikali yenye Jumla ya watoto 9011 Wavulana 4897 na Waschana 4114, aidha serikali imeendelea kuratibu huduma ya malezi ya Kambo na Kuasili ambapo kwa kipindi cha 2020/21 Wizara ilipokea maombi 110  jumla ya watoto 40 waliwekwa kwenye Malezi ya kambo na watoto 50 waliasiliwa wakiume 28 na wakike 22 ikilinganishwa na maombi 131 ambapo jumla ya watoto 48 wakiume21 wakike 27 waliwekwa kwenye malezi ya kambo na watoto 56 waliasiliwa wakiume 17 wakike 39 kwa mwaka 2021/22.

 

Wakili Mpanju, ameiomba Ofisi ya Rais TAMISEMI, kutumia mifumo Madhubuti ya TEHAMA, itakayosaidia kuweka takwimu sahihi kwa kuwabaini watoto wanaohitaji Malezi mbadala

 

Kwa upande wake Mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mariam Nkumbwa, amesema watahakikisha wanaimarisha mifumo ya Ufuatiliaji na shughuli zote za Malezi zinaingia kwenye Mipango ya bajeti sambamba na kuimarisha ushirika na wadau ili kuwa na takwimu sahihi.

 

Naye mwakilishi wa Shirika la SOS Onesmo Itozya amesema,Usalama wa Watoto wa leo ndio Usalama wa Taifa la kesho, wao kama SOS ambao wamekuwa nchini  kwa zaidi ya Miaka 30 bado wanaiona ipo haja suala la Malezi Mbadala likapewa kipaumbele.

 

“Toka kupata kwa Uhuru wa Nchi yetu, leo tukiwa tunatimiza Miaka 61, nafurahi kwa mara ya kwanza tunakuwa na jukwaa la pamoja la kujadili masuala ya Malezi Mbadala hii haijawahi kutokea, hivyo tutatumia fursa hii tuweze kutoka na afua zitakazo weza kulinusuru taifa na watu waliokosa Malezi bora” amesema Itozya.

 

Awali akitoa Salaama za Mkoa, Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa, Wahida Ntiro amesema anaipongeza Serikali kwa hatua hiyo huku akiomba Wizara kuongeza Wataalam wa Ustawi wa Jamii kwenye ngazi za Mikoa na Halmashauri ili kuwezesha shughuli hizo kutokukwama.

MKUTANO MKUU WA MWAKA WA WADAU MADALE, WAJADILI CHANGAMOTO NA MAFANIKIO

$
0
0

 

Stephen Kazimoto Mwenyekiti wa Wadau Madale akizungumza kwenye mkutano mkuu wa Mwaka wa Wadau hao Leo uliofanyika kwenye ukumbi wa Lemoon Catering mkabala na Kituo Cha Polisi Madale Kata ya wazo wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam.

.........................

Kikundi cha Wadau Madale Group wamekutana na kufanya mkutano mkuu wa Mwaka eo  kwenye ukumbi wa  Lemoon Garden Madale ikiwa ni kujadili maendeleo pamoja na changamoto mbalimbali zinazokabili kundi hilo.

 

Kikundi cha Wadau Madale kina takribani miaka mitano(5) ambapo wadau hao wamekuwa wakisaidiana kwenye mambo mbalimbali ya kijamii.

 

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Wadau Madale Group Bw.Stephen Kazimoto wakati akizungumza na Wanachama Katika mkutano wa Mwaka wa kikundi hicho uliofanyika Leo jijini Dar es Salaam na kushirikisha wanakikundi.

 

Moja wapo ya baadhi ya Vipengele ambavyo vipo kwenye katiba ya Wadau Madale Group  ni kuwepo kwa michango ya msiba endapo mmoja wa wadau atapata msiba, kuwepo kwa ulazima wa michango ya mkutano mkuu kwa kila mdau ambapo mkutano huo utafanyika kila mwaka, matangazo ya Biashara kwa kila meza ni shilingi elfu ishirini (20) hii kwa ajili ya wajasiriamali wadogo wadogo.

 

Aidha mkutano wa leo tarehe 10 Decemba 2022 umeazimia kutokuwepo kwa uchaguzi wowote wa viongozi hivyo viongozi wa zamani wataendelea kushikilia nafasi zao kwa kipindi cha miaka mitatu (3), kuwepo kwa ada ya elfu ishirini(20) kila mwezi kwa kila mdau ambapo mchango huo utakuwa na Kwa ajili ya kuchangia Wadau pindi wanapopata misiba ya wao wenyewe au wategemezi.

 

Ifikapo mwaka 2023 kikundi cha wadau kitakuwa tayari kishafungua akaunti ambapo michango yote itakuwa inawekwa kwenye akaunti hiyo lakini pia wadau watafungua Sacoss na wanakaribisha wadau ambao watapenda kujiunga, wadau wameshauri kuwepo kwa jumbe za simu za kawaida ambazo sikitumwa zinaweza mfikia mdau yeyote hata kama anatumia simu isiyokuwa na WhatsApp.

 

Hata hivyo viongozi wa Wadau mlMadale Group  wameendelea kutoa shukurani kwa wadau wa Madale kushiriki vyema katika mambo mbali mbali ya kijamii lakini pia amewaomba baadhi ya wadau wasiokuwa waaminifu kubadilika na kutoa michango kwa wakati ili waweze kufanikisha kikundi hicho kufika mbali na kufanikisha malengo kwa wakati.

 

Elesia Mbuya Katibu wa Wadau Madale akizungumza kwenye mkutano mkuu wa Mwaka wa Wadau hao Leo uliofanyika kwenye ukumbi wa Lemoon Catering mkabala na Kituo Cha Polisi Madale Kata ya wazo wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam.

 

Mmoja wa Wanachama wa Wadau Madale akizungumza kwenye mkutano mkuu wa Mwaka wa Wadau hao Leo uliofanyika kwenye ukumbi wa Lemoon Catering mkabala na Kituo Cha Polisi Madale Kata ya wazo wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam

 

Frank Magige Mhazini wa Wadau Madale akizungumza kwenye mkutano mkuu wa Mwaka wa Wadau hao Leo uliofanyika kwenye ukumbi wa Lemoon Catering mkabala na Kituo Cha Polisi Madale Kata ya wazo wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam.

 

Gration Mbelwa Mwenyekiti mstaafu Wadau Madale wa Wadau Madale akizungumza kwenye mkutano mkuu wa Mwaka wa Wadau hao Leo uliofanyika kwenye ukumbi wa Lemoon Catering mkabala na Kituo Cha Polisi Madale Kata ya wazo wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam.

 Picha mbalimbali zikiwaonesha Wanachama wa Wadau Madale wakiwa kwenye mkutano mkuu wa Mwaka wa Wadau hao Leo uliofanyika kwenye ukumbi wa Lemoon Catering mkabala na Kituo Cha Polisi Madale Kata ya wazo wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam.


 Seba Nkoma, kocha mkuu Yanga Princess

$
0
0


Na Mwandishi Wetu


UONGOZI wa klabu ya Yanga umemtangaza Sebastian Nkoma kuchukua nafasi ya Edna Lema.

Kabla ya kuifundisha Yanga Princess, Seba Nkoma aliwahi kuifundisha Simba Queens.

Lema kabla ya kuwa Kocha Mkuu wa Yanga Princess alikuwa mchezaji wa timu ya Taifa ya wasichana Twiga Stars

MAGAZETI YA TANZANIA DESEMBA 11, 2022

Viongozi ACT Wazalendo washikiliwa Pemba

$
0
0

Na Hassan Msellem

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kusini limewakamata na kuwahoji watu wawili ambao ni wanachama wa chama cha ACT Wazalendo kwa tuhuma za kuwakashifu viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kutoa kauli za uchochozi.

Waliokamatwa ni Salum Abdalla Herezi maarufu wa Mwalimu Herezi mwenye umri wa miaka 65, na mjumbe wa kamati ya uongozi wa Jimbo la Mtambile mkaazi wa Mjimbini, mwengine ni Nachia Ali Jamali mwenye umri wa miaka 39, mjumbe wa kamati ya fedha ya Jimbo mkaazi wa Wambaa. Baada ya mahojiano hayo wamechiwa huru kwa ajili ya uchunguzi. 

Watu hao walikamatwa wakiwa katika kikao cha ndani cha chama wakitoa maoni ya kupinga uteuzi wa Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar 'ZEC' Mhe. Thabit Idrissa Faina.


Magazeti ya Tanzania Desemba 12, 2022

WAJEDA WAACHANA NA UKAPERA BAADA YA KUFUNGA NDOA WAPEWA MANENO MAZITO

$
0
0

Wanajeshi (WAJEDA) Wanandoa Valentino John Tuka na Tusibwene Mustafa Juma kutoka Songea mkoani Ruvuma wakionesha tabasamu baada ya kuachana na ukapera kwa kufunga ndoa Takatifu katika Kanisa la Moravian Usharika wa Kimara  mwishoni mwa wiki Desemba 10, 2022 jijini Dar es Salaam.
Mchungaji wa Kanisa hilo Usharika wa Kimara, Alamu Mwambande Kajuni akifunga ndoa hiyo.
Mchungaji wa Kanisa la Moravian Usharika wa Pugu Kajiungeni , Laiton Silumbwe akiongoza ibada ya ndoa hiyo Takatifu.
Wanandoa hao wakionesha furaha yao baada ya kuingia ukumbuni.
Brigedia Mstaafu, Cosmas Kayombo na mke wake walikuwa ni miongoni mwa wageni waalikwa walihudhuria hafla ya ndoa hiyo.
Ibada ya ndoa ikiendelea.
Mama Mzazi wa Bibi Harusi Ambwene Anyitike Kyoga (kulia) akionesha umahiri wa kuongoza Kwaya ya Kanisa hilo Usharika wa Pugu Kajiungeni wakati ikitoa burudani.
Baba Mzazi wa Bwana Harusi Mzee John Ambros Tuka (kushoto) akiwa kwenye ibada hiyo ya ndoa.
Ibada ikiendelea hao ni ndugu wa Bibi Harusi wakiwa kwenye ibada hiyo.
Kwaya ya kanisa hilo Usharika wa Kimara ikitoa burudani.
Kwaya ya kanisa hilo kutoka Pugu Kajiungeni ikitoa burudani.
Ibada ikiendelea.
Vijana walioshiba kisawasawa ndugu wa Bibi Harusi kutoka Pugu Kajiungeni wakiongozwa na Chambuso Alphan Shukuru  (kushoto) wakiwa kwenye hafla hiyo.
Bibi wa Bwana Harusi akitoa neno la kuwahusia wanandoa hao.
Mama mkubwa wa Bibi Harusi Mary Anyitike akitoa neno la shukurani kwa uongozi wa kanisa hilo.
Kwaya kutoka Pugu Kajiungeni ikitoa burudani.
Picha ya pamoja baada ya ibada hiyo ya ndoa Takatifu.

Dada wa Bibi Harusi Anna Segere Mirambo akiwa katika picha ya pamoja na Bibi Harusi, Tusibwene Mustafa Juma.

Picha ya pamoja Bibi Harusi na wadogo zake na dada yake Mbumi Donald Mwaibale (kulia)

Wanandoa wakiwa katika picha ya pamoja na mama zake Bibi Harusi  na Mjomba wao Donald Mwaibale (kulia)
Wanandoa wakiwa katika picha ya pamoja na wazazi wao wa pande zote mbili.
Wanandoa hao wakiwa katika picha ya pamoja na wazazi wa Bwana Harusi.
Wanandoa hao wakiwa katika picha ya pamoja na wazazi wa Bibi Harusi.
Picha ya pamoja.
Wajomba wa Bibi Harusi na mama zake wakiwa katika picha ya pamoja.
Baba wa Wanandoa hao wakiserebuka wakati wakiingia ukumbini.Kushoto ni Baba wa Bwana Harusi, John  Ambros Tuka na kulia ni Baba wa Bibi Harusi, Mustafa Juma.
Mama wa wanandoa hao wakionesha umahiri wa kuserebuka wakati wakiingia ukumbuni. Kushoto ni Mama ya Bibi Harusi, Ambwene Kyoga na kulia ni Mama wa Bwana Harusi, Augusta Francis Mapunda.
Burudani zikiendelea kutolewa ukumbini.
Maharusi wakiwa katika picha ya pamoja na kamati yao ya maandalizi ya sherehe hiyo.
 

Na Dotto Mwaibale,Dar es Salaam

 

WANAJESHI (WAJEDA) Valentino John Ambros Tuka na Tusibwene Mustafa Juma kutoka Songea mkoani Ruvuma wameamua kuukimbia ukapera kwa kufunga ndoa Takatifu katika Kanisa la Moravian Usharika wa Kimara  jijini Dar es Salaam.

 

Ndoa hiyo iliyokuwa ya kuvutia na ya aina yake ambayo imefungwa Desemba 10, 2022 na kuhudhuriwa  na mamia ya watu ilikuwa na mvuto kutokana na shamrashara mbalimbali na burudani za kwaya mbili zilizokuwa zikitoa burudani ikiwepo kwaya ya kanisa hilo kutoka Pugu Kajiungeni na Kimara huku ikisindizwa na ngoma ya ya asili ya kabila la Wangoni.

 

Ndoa hiyo iliwahusisha ndugu jamaa na marafiki wa pande zote mbili wakiongozwa na wazazi wa wanandoa hao, Mzee John Ambros Tuka na mke wake Augusta Francis Mapunda wakiwa ni  wazazi wa bwana harusi na wazazi wa Bibi Harusi Mustafa Juma akiwa na mzazi mwenzake Ambwene Anyitike Kyoga.

 

Mchungaji wa Kanisa la Moravian Usharika wa Pugu Kajiungeni , Laiton Silumbwe akitoa wosia kwa wanandoa hao aliwaambia kuwa sasa wamekuwa mwili mmoja hivyo ndoa yao na iheshimiwe na watu  wote na silaha kubwa kwao ni kumtanguliza Mungu katika maisha yao,kudumisha upendo na kuomba msamaha pale watakapokoseana na si vinginevyo.

 

Alisema ndoa ni kusikilizana na haihitaji ubabe ni kila mmoja kumsikiliza mwenzake na kuwa na watoto ni majaliwa ya Mungu ambapo aliendelea kuwasisitiza wanandoa hao kumtumikia Mungu wakati wote wa maisha yao.

 

"Kutokana na kuwepo kwa utandawazi kumekuwa na changamoto nyingi kwenye ndoa nahata kufikia kupigana kwa wanandoa mambo haya nendeni mukayashinde kwani hayampendezi Mungu" alisema.

 

Mwinjiristi Atupele Kyomo kutoka kanisa hilo Usharika wa Msamala  mkoani Ruvuma ambaye aliwasindikiza wanandoa hao alisema sasa wamekuwa mwili mmoja hivyo watu wa nje wakiwepo ndugu, jamaa na marafiki waache kuwaingilia na mtu yeyote atakayehitaji msaada kwa wanandoa hao wanapaswa kuwahusisha wote.

 

"Kabla ya kufunga ndoa kuna baadhi ya ndugu walikuwa wakimpigia Bwana harusi au Bibi harusi wakiomba hela au mahitaji fulani lakini sasa nawaomba mambo hayo yaacheni ukiwa na shida washirikisheni wote" alisema Mwinjilisti huyo.

 BASATA YAPONGEZA TUZO ZA DANSI, YAAHIDI KUZIKUZA

$
0
0


Katibu Mkuu wa Baraza la Sanaa Taifa (BASATA), Dokta Kedmon Mapana (pichani) amezipongeza tuzo za muziki wa dansi nchini huku akiahidi kuzikuza kitaifa.

Ametoa pongezi hizo jijini Dar es Salaam hivi karibuni katika tamasha la utoaji wa tuzo pekee za muziki wa dansi nchini za Cheza Kidansi.

Dokta Mapana amesema Cheza Kidansi inakuza sanaa na utamaduni nchini huku ikiboresha maisha ya wanamuziki jambo linalostahili kuungwa mkono.

'Tunawaunga mkono kwa kutusaidia kwa kiwango kikubwa kukuza sanaa nchini kwani hili ni jukumu letu, nasi tunapoona jambo zuri tupo tayari kuliendeleza ili kuwanufaishe wengi zaidi'

'Kupitia tuzo hizi ikiwa ni mwaka wa nne, nyie mnawasaidia wananchi kuboresha maisha yao kwani muziki ni ajira na kila mnachofanya kukuza tasnia hii mnaisaidia pia serikali kuboresha maisha ya watu wake'

Dokta Mapana ameahidi kutoa ushirikiano wowote utakaohitajika kwa Cheza Kidansi ili kuzifanya tuzo hizo kuwa na mwonekano mkubwa wa kitaifa.

'Muziki wa dansi una heshima kubwa, hivyo jitihada mnazofanya za kuukuza na kuutangaza zaidi hasa kupitia tuzo hizi, serikali itawapa ushirikiano wowote ili ziboreke'

Katika tukio hilo la kuwatangaza washindi wa tuzo hizo, bendi za Town Classic na Orchestra Sikinde OG zilipata fursa ya kutoa burudani nzito iliyokata kiu ya wafia dansi.

Wadau wengi wa dansi walihudhuria tukio hilo kutoka kada mbalimbali wakiwemo wanahabari, wafanyabiashara na wadau wa maendeleo pia wananchi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni ya Cheza Kidansi Entertainment ambao ni waandaaji wa tuzo hizo Bernard James ameahidi kutoa ushirikiano mkubwa kwa BASATA na kuziboresha tuzo huko huku akiahidi kuendelea kukuza muziki wa dansi.

'Mwakani tutafanya maboresho makubwa ili tuzo ziwahusishe pia wanamuziki wa nje ya nchi ili kuwapa changamoto wanamuziki wetu wawe wabunifu zaidi'

Amesema watawaalika wanamuziki wa Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda na Kongo DRC ili kuwapa hamasa wanamuziki watanzania kukua kimataifa.

'Tunataka tuone uwezo wa wanamuziki wetu kama unakua kwa kuwashindanisha na wenzao wa mataifa mengine ili kuufanya muziki wetu ukue zaidi'

Huu ni msimu wa nne wa tuzo hizo zilizoanza mwaka 2019 jijini Mwanza.

Washindi wa tuzo za mwaka huu ni wafuatao;

1. Wimbo bora kushirikiana- Ukinipenda-Ticha Star ft Caty Soul

2. Chipukizi bora-Ticha Star

3. Rapa Bora-Difenda

4. Mtunzi Bora-Fadhili Nkurlu

5. Video bora-Arumbaya(Bogoss Musica)

6. Wimbo bora-Mchepuko(Orchestra Sikinde Original)

7. Mpiga gitaa bora-Yaniki Solo(Mjengoni Classic Band)

8. Mpiga drum-Martin Kibosho

9. Bendi bora-Sky Melodies

10. Mwimbaji bora KE-Hadija Mnoga

11. Mwimbaji bora ME-Kelly Hasso

12. Mnenguji bora-Kisura(Mjengoni Classic Band)

13. Dansa bora-Hamza Mapande(Twanga Pepeta)

14. Mdau bora-Angela Bushoke

15. Hall of fame-Joseph Mangapi

16. Mtayarishaji bora-Daddy One

17. Mwanamuziki bora-Nyoshi El Saadat

18. Mwandishi bora-Khamis Dacota

 KMC FC YAANZA KUJIFUA KWA MZUNGUKO WA PILI DISEMBA 15 DHIDI YA COASTAL UNION

$
0
0

Kikosi cha Timu ya KMC FC leo kitaanza maandalizi kuelekea katika mzunguko wa pili wa michuano ya Ligi kuu ya NBC soka Tanzania Bara itakayoendelea Disemba 15 mwaka huu kwa mujibu wa ratiba ya Bodi ya ligi kuu Tanzania TPLB.


Katika hatua hiyo KMC FC itawakaribisha Coastal Union ya mkoani Tanga katika uwanja wa Uhuru hapa Jijini Dar es salaam ambapo itapigwa siku ya Alhamisi ya Disemba 15 saa 16:00 jioni.

Timu hiyo ya Manispaa ya Kinondoni chini ya kocha Mkuu Thierry Hitimana itaanza maandalizi hayo leo ikiwa imetoka kupata ushindi katika mchezo hapo jana wa michuano ya kombe la Azam Sports Federation ASFC  dhidi ya Tunduru Korosho uliomalizika kwa KMC FC kupata ushindi wa  magoli sita kwa moja.

Aidha katika michezo hiyo ya ligi kuu ya NBC,  KMC FC inajiweka vema ili kuanza vizuri katika michezo mitatu ya nyumbani kwa kuhakikisha kwamba inavuna alama zote muhimu na hivyo kuendelea kujiweka sawia katika msimamo wa Ligi.

" Tunakwenda tena kwenye mzunguko wa pili, tunafahamu kuwa utakuwa wenye ushindani zaidi ya ule wa kwanza kutokana na kwamba ndio tunakwenda kumaliza ligi , sasa kila timu itakuwa inajipanga kwa ajili ya kupata matokeo, hivyo KMC FC tunakwenda tukiwa imara na tutafanya vizuri kwenye michezo yetu.

Tutakuwa na michezo mitatu ya mwanzo wa mzunguko wa pili ambapo yote tutakuwa nyumbani,  michezo hiyo ni dhidi ya Coastal Union ya mkoani Tanga, Polisoi Tanzania pamoja na Simba, hivyo tuna waahidi mashabiki zetu kuwa tutafanya vizuri kwenye michezo hiyo.

KMC FC ipo katika nafasi ya 10 na jumla ya alama 16 baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza na kwamba inakwenda kwenye mzunguko huo wa pili ikihitaji ushindi kwa kila mchezo ili kufanikisha kupanda kwenye nafasi nzuri mwa msimamo wa Ligi Kuu ya NBC.



 IGOWOLE FC BINGWA WA KIHENZILE CUP

$
0
0

Kushoto aliyeshika MIC ni mbunge wa jimbo la Mufindi Kusini na wakatikati ni MNEC Richard Kasesela pamoja na nahodha wa timu ya Igowole iliyochukua ubingwa wa Kihenzile Cup and Awards
Kushoto aliyeshika MIC ni mbunge wa jimbo la Mufindi Kusini na wakatikati ni mwenyekiti wa CCM wialya ya Mufindi pamoja na nahodha wa timu ya Nyololo iliyoshika nafasi ya pili katika mashindano ya Kihenzile Cup and Awards
MNEC Richard Kasesela pamoja na nahodha wa timu ya Igowole iliyochukua ubingwa wa Kihenzile Cup and Awards akikabidhiwa zawadi mbalimbali za kuwa mabingwa
Kushoto ni mbunge wa jimbo la Mufindi Kusini,katika ni mwandishi mwandamizi wa habari za Michezo Shaffih Dauda akiwa na Nahodha wa timu ya Nyololo aliyeibuka mchezaji bora wa mashindano ya Kihenzile Cup and awards

Mashabiki walikuwa wakifuatilia fainali ya Kihenzile Cup and awards.



Na Fredy Mgunda, Iringa

 

Mashindano ya kihenzile cup and awards 2022 yametamatika kwa timu ya Igowole FC kuibu bigwa baada ya kuifunga timu ya Nyololo kwa mikwaju ya penati baada ya kutoka sare ya kufungana goli 2-2 ndani ya dakika 90 mchezo huo ulichezwa katika kiwanja cha shule ya msingi Igowole.

 

Kwa ushindi huo Timu ya Igowole imefanikiwa kujinyakulia kiasi Cha shilingi laki 5, Jezi seti 2, mipira miwili, Na T-shirt ambayo atavaa nahodha wa timu Hiyo.

 

Timu ya Nyololo iliyoambulia nafasi ya Pili imepewa kiasi Cha shillingi Laki 3, Jezi seti 2 na Mipira miwili pamoja na t-shirt Moja Kwa ajili ya Nahodha.

 

Kwa mujibu wa Mdhamini wa Michuano Hiyo, Mbunge wa Jimbo la Mufindi kusini David Kihenzile, Mshindi wa Tatu ambaye ni timu ya Mtwango baada ya kuifurusha timu ya Malangali Goli 7-0 amejunyakulia Shillingi Laki 1, Jezi seti 1 na T-shirt ya Nahodha.

 

Kihenzile alisema kuwa Lengo la michuano Hiyo ni kuibua vipaji vya vijana katika Jimbo la Mufindi Kusini na kuwaepusha na makundi hatarishi.

 

Alisema kuwa atawasemea wanamichezo bungeni ili serikali iweze kupunguza Kodi ya vifaa vya michezo Kwa lengo la kuwatengeneza vijana Kwa faida ya Timu za Tanzania na Taifa kwa ujumla

 

Kihenzile alisema kuwa katika Kutambua mchango wa shule za msingi zilizofanya vizuri katika mitihani ya darasa la saba mwaka huu, ametoa zawadi kwa shule ya tatu za halmashauri ya wilaya ya Mufindi ili kuhamasisha Taaluma.

 

Katika fainali ya Kihenzile Cup and awards Mgeni Rasmi alikuwa ni Naibu Waziri wa Utumishi na Utawala na Utawala Bora Deogratius Ndejembi alimpongeza Kihenzile Kwa kuanzisha mashindano Hayo huku akimtaka kuandaa Combine ya wachezaji waliofanya vizuri katika mashindano hayo ili waweze kuunda Timu ambayo itaenda kucheza mechi ya kirafiki na Timu ya Combine ya Chamwino Jijini Dodoma.

 

Mashindano Hayo yamehusisha Timu 16 kutoka katika kata za Jimbo la Mufindi kusini yameshuhudiwa na Mwandishi Nguli wa Habari za Michezo hapa Nchini Shaffih Dauda ambaye ameahidi kuwachukua vijana waliofanya vizuri ili kuwapeleka katika vilabu vikubwa na kufanya majaribio.

 

Naye Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa bara NEC, Mh. Richard Kasesela amewapongeza washindi waliopatikana katika michuano hiyo ya Kihenzile Cup huku akiwasisitiza vijana watakaopata nafasi ya kuchaguliwa na Mwanahabari Dauda kwenda kufanya majaribio, kuonesha nidhamu na kufanya vizuri ili kuwashawishi Maskauti wengine kuja Mkoani Iringa kutafuta wachezaji wenye vipaji vya Mpira.

 

SIMBA SC YAANGUKIA KUNDI C LIGI YA MABINGWA CAF CL 2022/23

$
0
0

 

Na Mwandishi Wetu


Wawakilishi Bora wa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati katika Mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) kwa misimu mitano mtawalia Simba SC wamepangwa kundi C msimu huu wa 2022/23.


Katika droo iliyopangwa mchana wa leo jijini Cairo nchini Misri Simba wameangukia kundi C ambapo watapambana na Raja Casablanca ya Morocco, Horoya ya Guinea Bissau na Vipers ya Uganda.


Simba walitin2 15,


ga hatua ya makundi kwa kuwaondoa De Agosto ya Angola baada ya hatua za awali kuwafulumusha Nyasa Big Bullets ya Malawi.

Katika hatua hiyo ya makundi washindi wawili katika kila kundi watatinga hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika CAFCL. 


Makundi ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika ukiachana na kundi C ni haya yafuatayo.


*CAF CHAMPIONS LEAGUE*


 _*GROUP A*_ 

*W.A.C* mar

*A Petro* Ang

*Js kabylie* alg

*As vita club* Congo


 _*GROUP B*_ 

*Al-ahly* egy

*Mamelod* Rsa

*El -hilal* sud

*Coton sport* cmr


 _*GROUP C*_ 

*Raja*

*Horoya a.c* gun

*Simba sc* Tan

*Vipers sc* uga


 _*GROUP D*_ 

*E.S.T* tun

*Zamale sc* egy

*Cr belouzdad*  alg

*Al -merikh* sud


Mwisho

YANGA YAANGUKIA KUNDI D NA TP MAZEMBE CAF CC

$
0
0

 



HATIMAYE Drooo ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika CAF CC imepangwa muda mchache uliopita jijini Cairo nchini Misri ambapo wawakilishi wa Tanzania Yanga SC wameangukia kundi D.


Droo hiyo ambayo inafanyika mchana huu imeanza na Kombe la Shirikisho CAFCC kisha Ligi ya Mabingwa Afrika CAFCL.



Yanga ambao ni wawakilishi wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho wameangukia kundi D sambamba na TP Mazembe ya DR Congo, US Monastir ya Tunisia na Real Bamako ya Mali.


Katika hatua hiyo kila timu itacheza mechi sita, tatu nyumbani na tatu ugenini na washindi wawili wa juu katika kila kundi watatinga hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika CAFCC, 2⁰22/2023.


Makundi mengine ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika CAFCC ni kama yafuatayo..


🔴 Group A:  


• USM Alger 🇩🇿 

• Marumo Gallants 🇿🇦

• Al Akhder 🇱🇾 

• Eloi Lupopo 🇨🇩


🔴 Group B:


• ASEC Mimosas 

• Diables Noir 🇨🇬

• Rivers United 🇳🇬 

• Motema Pembe 🇨🇩


🔴 Group D:


• TP Mazembe 🇨🇩

• US Monastir 🇹🇳 

• Yanga SC 🇹🇿 

• Real Bamako 🇲🇱


Mwisho

  China Dasheng Bank yazindua Tawi jipya Kariakoo

$
0
0
Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam

Benki ya China Dasheng imezindua Tawi jipya katika Mtaa wa Agrey na Lumumba, Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo leo  jijini humo Mkurugenzi wa Benki hiyo Jimmy Mrosso amesema China Dasheng Benki ni benki inayokua haraka na yenye mtaji wa kutosha.

Amebainisha kuwa kwa sasa benki hiyo inapatikana nchini Tanzania kwamba tawi hilo lililozinduliwa ni lapili na hivyo matamanio yao ni kufungua matawo nchi nzima pamoja na mataifa mengine.

“Lengo tunataka kuunganisha uchimi wa Tanzania na China moja kwa moja, hatuwezi kupuuza umuhimu wa uchumi wa China kwa Tanzania,” amesema Mrosso.

Amesisitiza kuwa benki hiyo imekuja kuunganisha Tanzania na China moja kwa moja kiuchumi.

Ameongeza kuwa  wanategemea kuwekeza zaidi kwenye benki hii ili kuongeza zaidi faida kwa wateja wao na kwa Tanzania na China kwa ujumla.

Amemtaka kila Mtanzania kuhakikisha anatumia fursa ya kuwepo kwa benki hii nchini katika kunufaika kiuchumi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Bodi ya Benki hiyo Poniwoa Mbisse, amesema kuwa wanayofuraha kufikisha miaka minne nchini ya kutoa huduma tangubenk hiyo ilipoanzishwa.

Amewashukuru Watanzania kwa kufanikisha mafanikio yao kwani bila wao wasingefikia hapo walipo.

Mbisse amefafanua kuwa lengo la Benki hiyo ni kuongeza mahusiano baina ya Tanzania na China.

 Wadau wa Bahari kutoka Nchi 15 wanolewa, TASAC yaahidi kuridhia Mkataba wa Kimataifa wa Bahari

$
0
0

Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam


Katika kuhakikisha mazingira ya Bahari na maji yanatunzwa Wadau wa Mazingira kutoka Nchi Wanachama 15 wa Afrika wameshiriki katika Warsha ya siku tatu kwaajili ya kukuza Uelewa wa pamoja juu ya Mkataba wa Kimataifa wa Utunzaji wa Mazingira ya Bahari.


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (sekta ya uchukuzi) Dkt. Ally Possi akizungumza katika warsha hiyo leo jijini Dar es Salaam amesema kuwa Mwitikio wa nchi mwanachama umekuwa mkubwa na ni jambo ambali dunia imeanza kuipa kipaumbele mkataba wa kimataifa kwaajili ya kulinda mazingira ya bahari ili kuhakikisha viumbe vitakavyo zaliwa majini vinakuwa hai.

Akizungumzia kuhusiana na hali ya bahari kwa sasa amesema kuwa Mazingira ya Bahari kwa sasa ni manzuri lakini tahadhari mbalimbali lazima zitolewa kwaajili ya Vizazi vya vijavyo.

"Ifahamike kuwa vyanzo vya maji hususani bahari vinasimamia sera ya uchumi wa bluu, sasa bahari inapochafuka na inapoharibiwa kimazingira, sera ya uchumi wa bluu inakuwa ngumu kwani kwa sababu ya viumbe ambavyo vinafanyika kuwa uchumi vitapotea pamoja na vyombo vya usafiri majini vitaharibika na kushindwa kufanya kazi inayotakiwa."
Amesema Dkt. Possi

Amebainisha kuwa  mkutano huo utatilia mkazo wa uridhiaji wa Itifaki ya sheria ya Bahari kwaajili ya kuendeleza uelewa mpana wa wadau wote.

Washiriki wa mkutano huo ni Wafanyakazi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Bandari, Taasisi ya Bahari ya Dar es Salaam (DMI) wa Wawakilishi wa Nchi 14 za Afrika.

Kwa upande  wake, Mkurugenzi Mkuu wa TASAC, Kaimu Abdi Mkeyenge amesema Shirika hilo limekasimiwa mamlaka ya kudhibiti mazingira ya majini na Maji yanayotokana na uchafunzi wa vyombo vya Usafiri Majini hivyo madhumuni ya warsha hiyo ni uelewa wa pamoja wa Jinsi ya kudhibiti maji, kusimamia masuala ya usafiri majini.

.....kwa kukaa sana yale maji inawezekana kuna viumbe ambavyo vinazaliwa na yale maji yaliyokuwa kwenye meli hakishushwa baharini katika maji ya kitaifa au eneo lolote la bahari kunauwezekano wa kushushwa na viumbe wengine ambao wamezaliwa baada ya yale maji kukaa muda mrefu

Hivyo basi yale maji yakishushwa yanaweza kuzalisha viumbe wengine ambavyo vitakuwa hatarishi kwa uendelevu viumbe ambao wapo baharini na tunavihitaji.

Amesema uchumi wa bluu unaweza usifikiwe kama maji yanakuwa hayadhibitiwi. Kwahiyo hatutaufikia uchumi wa bluu kama mikataba hii hatutairidhia na kuzingatia ni jinsi gani tunaweza kujikinga na hivyo viumbe ambavyo vinaweza kuzalishwa.

Shirika la Kimataifa la Bahari linatoa elimu kwa Taasisi mbalimbali zinazohusika na masuala ya usafiri kwa njia ya maji, taasisi zinazohusika na masuala ya bahari zimeshiriki warsha hiyo ili kuwa na uelewa wa pamoja ili mkataba utakaporidhiwa na kutengeneza kanuni za Kutumika hapa nchini.

Nae,  Mkurugenzi wa Usalama na Mazingira Baharini kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Sekta ya Uchukuzi Stela Katondo amesema kuwa maji yanahobebwa na meli yanasaidia meli pale ambapo inakuwa haina mzigo pia ikiwa na mzigo mdogo yanapunguzwa au kuongezwa ili kuweka uzito sawa katika meli na Maji hayo watu wenye meli wamekuwa wakiyamwaga baharini jambo ambalo sio zuri.

"Maji hayo yanaviumbe na mimea ambayo sio asili ya huku kwetu kwa hiyo ikitokea yanamwagwa baharini yatakuwa na viumbe wavamizi wataleta namna tofauti ya kimazingira Shirika la Kimataifa la Bahari (IMO) liliona umhimu wa kuweza kudhibiti hali hiyo kwa sababu kimazingira sio sawa, kinachotakiwa ni kuto kumwagwa baharini kama nchi mwanachama wa IMO tunatakiwa kuridhia mkataba huo ili kuweza kusimamia kuwa haitakiwi ukifika bandarini kumwaga maji inatakiwa kwenda kumwagwa katika kati ya habari ili yasiweze kuleta shida katika eneo letu la mazingira ya maji.

Amesema kwa Tanzania Sasa hivi tupo katika hali nzuri kwa sababu tumeshaanza kuridhia mkataba pia amesema Kama wizara wameshatoa maoni na mapendekezo kwa wadau mbalimbali wanaohusika na mkataba huu. Na mpaka sasa wameshaanza kupokea maoni yao.
Viewing all 19659 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>