Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all 19659 articles
Browse latest View live

Serikali yatakiwa kuhimiza wananchi kushiriki upigaji kura Uchaguzi Mkuu

$
0
0
Kulia mbele ni Programu Ofisa wa TGNP Mtandao, Deo Temba akiwasilisha mada kwa washiriki wa mafunzo ya kuripoti habari za wanawake katika Uchaguzi Mkuu 2015 yaliowashirikisha wachora katuni, wasanii na waandishi wa habari pamoja na baadhi ya waendeshaji wa mitandao ya jamii nchini Tanzania (bloggers) mara baada ya semina hiyo. Kulia mbele ni Programu Ofisa wa TGNP Mtandao, Deo Temba akiwasilisha mada kwa washiriki wa mafunzo ya kuripoti habari za wanawake katika Uchaguzi Mkuu 2015 yaliowashirikisha wachora katuni, wasanii na waandishi wa habari pamoja na baadhi ya waendeshaji wa mitandao ya jamii nchini Tanzania (bloggers) mara baada ya semina hiyo.Baadhi ya maofisa kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) wakifuatilia mada anuai zinazowasilishwa. Baadhi ya maofisa kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) wakifuatilia mada anuai zinazowasilishwa.Kushoto mbele ni Anna Sangai na Anna Kika ambao ni maofisa programu kutoka TGNP Mtandao wakiwasilisha mada kwa kwenye mjadala wa wachora katuni, wasanii na waandishi wa habari pamoja na baadhi ya waendeshaji wa mitandao ya jamii nchini Tanzania (bloggers). Kushoto mbele ni Anna Sangai na Anna Kika ambao ni maofisa programu kutoka TGNP Mtandao wakiwasilisha mada kwa kwenye mjadala wa wachora katuni, wasanii na waandishi wa habari pamoja na baadhi ya waendeshaji wa mitandao ya jamii nchini Tanzania. washiriki wa mafunzo ya kuripoti habari za wanawake katika Uchaguzi Mkuu 2015 yaliowashirikisha wachora katuni, wasanii na waandishi wa habari pamoja na baadhi ya waendeshaji wa mitandao ya jamii nchini Tanzania (bloggers) mara baada ya semina hiyo. washiriki wa mafunzo ya kuripoti habari za wanawake katika Uchaguzi Mkuu 2015 yaliowashirikisha wachora katuni, wasanii na waandishi wa habari pamoja na baadhi ya waendeshaji wa mitandao ya jamii nchini Tanzania (bloggers) mara baada ya semina hiyo.washiriki wa mafunzo ya kuripoti habari za wanawake katika Uchaguzi Mkuu 2015 yaliowashirikisha wachora katuni, wasanii na waandishi wa habari pamoja na baadhi ya waendeshaji wa mitandao ya jamii nchini Tanzania (bloggers) mara baada ya semina hiyo. washiriki wa mafunzo ya kuripoti habari za wanawake katika Uchaguzi Mkuu 2015 yaliowashirikisha wachora katuni, wasanii na waandishi wa habari pamoja na baadhi ya waendeshaji wa mitandao ya jamii nchini Tanzania (bloggers) mara baada ya semina hiyo.

Na Joachim Mushi

WANAHARAKATI Ngazi ya Jamii nchini wametoa madai kuelekea Uchaguzi Mkuu huku wakiiomba Serikali iharakishe mchakato wa uandikishaji daftari la kudumu la wapiga kura ili vijana wengi wanaostahili waweze kuitumia haki yao ya msingi ya kushiriki mchakato wa uchaguzi na ule wa kura ya maoni. 

 Madai hayo yametolewa katika tamko lao lililotolewa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP Mtandao) kwenye warsha ya majadiliano kati ya waandishi wa habari, wachora katuni na waandishi wa habari za mitandao ya jamii iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

 Katika madai hayo wanaharakati ngazi ya jamii pia wameomba elimu ya uraia na ya mpiga kura itolewe kwa wingi ili iwafikie vijana wapate hamasa ya kujitokeza kugombea na kupiga kura, ikiwa ni pamoja na kuvitaka vyama vya siasa kuweka mfumo wa uwiano kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu waweze kupata nafasi sawa kama wagombea kwenye uchaguzi bila upendeleo wala woga. 

 Aidha imetaka vijana wanaojitokeza kama wagombea wawekewe mazingira rafiki ikiwezekana wapewe ruzuku ya kuwasaidia kushindana kwenye uwanja wa demokrasia, pamoja na kushauri Sera ya Taifa ya Vijana pamoja na Mkataba wa Vijana wa Afrika unalitambua kundi la vijana kama rasilimali mojawapo muhimu sana kwenye maendeleo na pia katika kulinda amani na utulivu kwenye Bara la Afrika. "

Hata hivyo pamoja na kwamba vijana ni zaidi ya 60% bado mchango na thamani ya vijana haujatumika ipasavyo kwenye demokrasia ya Tanzania, huku thamani yao ikionekana tu nyakati za uchaguzi kwa kutumiwa kama walinzi au wapambe wa wagombea," imeeleza sehemu ya tamko hilo. 

 Limebainisha kuwa pamoja na uanzishwaji wa Mabaraza ya Vijana kwa vyama vingi, mengi hayana nguvu ya maamuzi kwa kuingiliwa na vyombo vya juu vya Chama, ikiwa ni pamoja na kukumbusha kuwa mwaka 2010 ulikuwa ni mwaka ambao vijana wengi waliingia Bungeni na wamekuwa chachu kubwa ya kuchangia na kuibua mijadala yenye tija Bungeni.

 Hata hivyo imeeleza kuwa bado idadi ya vijana wanaojitokeza kupiga kura hasa wasichana bado ni ndogo ukilinganisha na ile ya wanaojiandikisha na wanaoshiriki kwenye kampeni, vijana wengi wanaojitokeza kwa kuweka nia ya kugombea wamekumbana na kigingi cha uteuzi kwa kutokubalika ndani ya vyama kwa mawazo mgando kwamba umri wao hauwawezeshi kufanya uchambuzi wa masuala makubwa ya kitaifa, kadhalika changamoto ya nguvu yao ndogo kiuchumi ajira ambayo inawafanya wasiweze kushindana kikamilifu katika uwanja usio na usawa wa siasa. 

 Kwa upande wa vyama vya siasa tamko hilo limetaka watu wenye ulemavu waingizwe kwenye sera na mipango ya nchi kwa vitendo kwani bado ushiriki wao kwenye masuala ya uchaguzi na uongozi uko chini. 

 Madai mengine ni pamoja na Vyama vya siasa kuweka mfumo wa uwiano kuhakikisha zinazingatia ushiriki wa watu wenye ulemavu kwenye uchaguzi kama wagombea na wapiga kura, Serikali kuweka mazingira rafiki kwa watu wenye ulemavu ili washiriki kikamilifu kwenye michakato yote ya maendeleo, hii ni pamoja na uchapishaji wa sheria na kanuni kwa lugha rahisi ikiwemo maandishi ya nukta nundu, vituo rafiki vya kampeni na kupiga kura kwa watu wenye ulemavu.

 Mengine ni pamoja na watu wenye ulemavu wa ngozi, kudai ulinzi na usalama wa maisha yao, kama raia wa taifa hili, uwepo wa mikakati ya kuelimisha umma uondokane na mawazo potofu yanayoashiria kutishia uhai na usalama wa kundi hili na hasa wenye ulemavu wa ngozi. Hatua kali za kisheria zichukuliwe kwa wote watakaohusika."

..Serikali ihakikishe upatikanaji wa taarifa na maarifa kwa njia rahisi ikiwemo lugha ya alama na maandishi ya nukta nundu kutoa elimu ya mpiga kura na pia vyombo vya habari kama vile TV ziweke wakalimani hasa katika vipindi vya taarifa ya habari na vipindi vyote vyenye mijadala ya kitaifa.

 Mgombea tutakayempa kura ni Yule ambaye miongoni mwa sera zake itakua ni kupinga ukatili wa kijinsia kwa hali zote bila woga wala upendeleo, aidha mengine ni pamoja na Serikali itakayoingia madarakani kuhakikisha inaunda Tume ya Kughulikia Ukatiki wa Kijinsia kama zilivyo Tume nyingine, kuunda mahakama maalum ya kushughulikia kesi za ukatili wa kijinsia ngazi ya familia na kuweka mikakati halisi ya kuhakikisha kwamba kila mwanamke ana haki ya uchumi na haki ya maisha endelevu/ajira akiwa kijijini au mjini, mwenye ulemavu, mzee au kijana, wanawake na wanaume wote wapate kipato kinachotosheleza kuishi maisha bora kama binadamu.

 Warsha hiyo ya siku moja iliyoandaliwa na TGNP Mtandao kwa ushirikiano na Mfuko wa Wanawake Tanzania (TWF) imejumuisha makundi mbalimbali ya wanahabari ikiwa ni lengo la kuwajengea uwezo kuandika masuala ya kijinsia kwa kina. *Imeandaliwa na www.thehabari.com

WIZARA YA WIZARA YA FEDHA YAWAPA SEMINA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU MRADI WA MABORESHO YA MATUMIZI YA FEDHA ZA UMMAA

$
0
0
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini na Msemaji wa Wizara ya Fedha, Ingiahedi Mduma akifafanua jambo wakati wa warsha ya siku tano kuhusu mradi wa maboresho ya matumizi ya fedha za umma inayoendelea katika Hoteli Njuweni Kibaha. 
Washiriki wa warsha kuhusu maboresho ya matumizi ya fedha za umma inayoendelea katika Hoteli ya Njuweni Kibaha.
 Baadhi ya waandishi wakiwa katika warsha ya siku tano kuhusu kuhusu mradi wa maboresho ya matumizi ya fedha za umma inayoendelea katika Hoteli ya Njuweni Kibaha. 


xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Public Financial Management Reform (PFMRP) ni Mradi wa maboresho ya matumizi ya fedha za umma.

Serikali ya Tanzania ilianzisha mradi huo kwa madhumuni ya kuimarisha mifumo ya matumizi ya fedha katika ngazi zote.  

Mradi huu umekuwa wa awamu 4 kutokana na mafanikio yanayojitokeza na changamoto.

Awamuya kwanza (I) ilikuwa kutoka mwaka 1998 – 2004 huu ulikuwa na malengo ya kudhibiti matumizi, kuweka nidhamu ya fedha pamoja na kukuzana kuimarisha uchumi mpana.

Awamuyapili (II) ilikuwa kutoka mwaka 2004 – 2008 malengo ya mradi huo yalikuwa ni kuimarisha na kuendeleza mifumo na njia zinazotumika katika malipo ya fedha za umma kwa kutumia njia rahisi na nyepesi.

  Aidha awamu hiyo ilizingatia pia uimarishaji wa njia ya ukusanyaji mapato na jinsi ya kuweka mbinu ya kuzitumia rasilimali fedha na kuweka mikakati ya kipi kianze kwanza.

Awamu ya tatu (III) ilikua kuanzia 2008 – 2011, mradi huu ulikua na malengo ya kuhakikisha kuna kuwa na upatikanaji rasilimali fedha kutoka katikaTaasisi mbalimbali za kifedha.

Awamu ya nne (IV) ya mradi ni kuanzia June 2012, mradi ulizinduliwa na kuanza rasmi tarehe 1 Julai, 2012.  Madhumuni ya mradi huu katika awamu ya nne umelenga katika kuonge za nguvu ambayo itawezesha kufikia malengo ya Sera ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025,

 hiyo inaenda sanjari na mpango wa maendeleo wa miaka mitano yaani 2011/2012 – 2015/2016na MKUKUTA (MkakatiwaKukuzauchumi Tanzania)/ MKUZA (Mkakati wa Kukuza uchumi Zanzibar), ili kufika malengo ya ukuaji wa uchumi.

Mafanikio ya mradi huu katika kuimarisha matumizi mazuri ya fedha za umma yatafikiwa kwa kuwa na matokeo ya maeneo makuu matanokama vile, usimaiziwaukusanyajikodi, mpangowabajeti, 

usimamizi wa bajeti, uwazi na uwajibikaji, 
usimamizi wa matumizi ya fedha zilizopangwa kutumika na kugundua matumizi ya nayoweza kujitokeza baadae na mabadiliko ya Uongozi pamoja na uangalizi na mawasiliano kwenye mambo yafedha.

Maboresho ya fedha za umma yanaenda sanjari na maboresho katika sekta za umma ambayo yanalenga kuimarisha utendaji bora na makini katika kutoa huduma  ambazo zinakuza uchumi ulioimara.

Mpango wa maboresho ya fedha za umma awamu ya nne (IV) pia utaangalia/utalenga kwenye kuwajengea uwezo wale wote wanaofanya shughuli za maboresho ya fedha za umma katika Nyanja tofauti tofauti.

Kufuatilia na kufanya tathmini katIka uwigo uliowekwa kwa kuangalia vipau mbele ambavyo vitatoa muelekeo na kufikia matokeo mazuri.

Kuhakikisha kuwa ripoti za fedha zinazotolewa zinakuwa za aina moja bila kuwa na utofauti wa aina yoyote.

Kuwa na uongozi mzuri ambao umepanga vizuri Taasisi za fedha.

Kuzilenga na kuzipa nguvu wakala ambazo zinaguswa moja kwa moja katika mifumo ya fedha za umma.

Mradi huu unafadhiliwa kwa pamoja na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB na Bank ya Dunia (WB),DfID, CIDA, DENMARK, IRELAND na KFW. Hawawote walisaini makubaliano ya kuchangia katika mradi huo.

Mpaka sasa hivi mradi huu umepata mafanikio makubwa hasa ya kuwekamfumomzuriwamalipo, muda wa kupitishwa kwa bajeti ya Taifa umeimarika na fedha zinatoka kwa wakati.  

AidhabajetiyamwananchiinatangazwakatikaTovutiyaWizarayafedha.MtandaowamalipoumefikampakakatikaSerikalizaMitaa

RAIS WA BURUNDI APINDULIWA

$
0
0
Rais Jakaya Kikwete akizungumza na waandishiwa habari jijini Dares Salaam, huku akiwa na Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza.
 Wanajesi wakiwatuliza wananchi.
 Wananchi wakiwa barabarani.
 Vifaru na magari ya Jeshi yakiwa mitaani.
Wanajeshi wakiwa katika mitaa ya Bunjumbura.

RAIS AMUAPISHA MKUU WA WILAYA MAGHARIBI B

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akimuapisha Ayoub Mohammed Mahmoud kuwa Mkuu wa Wilaya Mpya ya Magharibi "B" katika Mkoa wa Mjini Magharibi hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo na kuhudhuriwa na Viongozi mbali mbali. (Picha na Ikulu.)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi hati ya kiapo   Ayoub Mohammed Mahmoud baada ya kumuapisha kuwa Mkuu wa Wilaya Mpya ya Magharibi "B" katika Mkoa wa Mjini Magharibi hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo na kuhudhuriwa na Viongozi mbali mbali.

INSPEKTA WA POLISI ATOA USHAHIDI KESI YA ALBINO MWANZA

$
0
0
Na Daniel Mbega, Mwanza

SHAHIDI wa sita katika kesi ya mauaji ya Aaron Nongo mwenye ulemavu wa ngozi (albino), Mkaguzi wa Polisi (Inspector) David Mhanaya, ameanza kutoa ushahidi wake katika Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza.

Mbele ya Jaji Robert Makaramba anayesikiliza Shauri hilo namba 213 la mwaka 2014, shahidi huyo ametumia siku nzima kutoa ushahidi wake akiongozwa na mawakili wa serikali Emil Kiria, Esther Majaliwa na Robert Kilando.

Hata hivyo, Jaji Makaramba aliahirisha kesi hiyo hadi keshokutwa Mei 14, 2015 baada ya kutokea mgongano wa kisheria katika masuala ya vidhibiti kufuatia pingamizi la Wakili Makwega wa upande wa utetezi, hivyo siku hiyo atatoa uamuzi kuhusiana na pingamizi hilo.

Washtakiwa katika kesi hiyo ni Chacha Jeremia, Mathew Jeremia Mlimi, Paschal Lugoye Mashiku na Alex Joseph maarufu kama Bugwema Silola Jangalu.

Marehemu Nongo aliuawa Juni 26, 2009 majira ya saa tatu usiku akiwa nyumbani kwake Ibanda Relini, jijini Mwanza ambapo wauaji hao walimkata usoni na kisha kumkata miguu yake yote miwili na kutoweka nayo pamoja na meno mawili ya mbele.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

$
0
0
Ndugu Wanahabari 
Uchaguzi Mkuu wenye lengo la kuwapata Madiwani, Wabunge na Rais nchini unatarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu nchini.
Nimekuwa nikitembelea vijiji na kata mbalimbali za Wilaya ya Kilombero. Hivi karibuni nilitembelea kata zote za wilaya, nilizungumza na wananchi, wengi wao walinishauri kugombea Ubunge. Wananchi wanaamini kuwa kwa pamoja tutaweza kuendeleza vema gurudumu la maendeleo kwa kasi zaidi.
 
Wananifahamu kama mtoto wa masikini mwenzao niliyewahi kuzunguka mitaani kupiga picha ili kuendesha maisha, mtoto wa masikini niliyewahi kuwa na ofisi ya kusafisha viatu vya watu eneo la Ubungo Maziwa kwa mzee Mrisho ili niweze kupata nauli ya kwenda shule wakati huo nasoma Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE).
 
Maisha nayafahamu vizuri na nina uchungu nayo, natamani kushirikiana na wananchi ili kuepukana na maisha duni. Katika maisha yangu kutokula au wakati fulani kutembea kwa miguu kwenda chuo CBE na kurudi nyumbani Ubungo Maziwa (nilikuwa naishi kwa dada), lilikuwa ni jambo la kawaida, kwani maisha yalikuwa magumu mno.
 
Sauti ya wananchi wa Kilombero

Kilio cha wananchi pamoja na mambo mengine ni kwamba wanahitaji kiongozi kijana mwenye nguvu za kuongoza, kiongozi mwenye ujuzi wa namna ya kuongoza na kutawala, kiongozi ambaye atakuwa bega kwa bega na wananchi katika harakati za kuwaletea maendeleo wananchi. Kiongozi ambaye anajua namna ya kuongoza, siyo namna ya kuhonga au kuwalisha yamini wapiga kura, kwani wanachohitaji watu wa Kilombero ni maendeleo, siyo zaidi. Hawahitaji kiongozi ambaye ni maarufu kwa kutembelea magari ya kifahari, wanahitaji huduma za kijamii kama shule, hospitali na wao wenyewe kusaidiwa namna ya kubuni miradi ya maendeleo.
 
Elimu yangu ya juu ni Stashahada ya Uzamili katika Uongozi na Utawala (Postgraduate Diploma in Leadership and Governance), kutoka Chuo cha Utumishi wa Umma-Dar es Salaam niliyohitimu Aprili 22, 2014. Hata hivyo nje ya elimu nimekuwa nikishughulika na masuala ya kijamii kupitia kufanya mikutano ya ana kwa ana na jamii katika masuala ya ujasiriamali, uchumba/ndoa na kadhalika.
 
Mojawapo sababu za wananchi kuamini kwamba ninaweza kushirikiana nao kwa ufanisi ni rekodi ambazo wananchi wenyewe wanazo juu yangu, kwani nimekuwa nao karibu katika mambo mengi ya maendeleo ikiwamo kushirikiana nao moja kwa moja au vikundi vyao hasa  vya walemavu, kina mama, vijana na kadhalika kama mshauri wao katika suala zima la namna ya kuviendesha na kuwaunganisha na taasisi au watu wa kusaidiana nao.
 
Kwa hivi sasa maeneo kadhaa ya Kilombero yanasaidiwa na mashirika mbalimbali yakiwamo ya nje, baadhi yake ni kutokana na jitihada zangu….nje ya uandishi wa habari, pia nimekuwa nikimiliki kampuni ya kuwaunganisha watu na vyuo vya nje ya Global Source Watch (GSW), ambayo imekuwa ikinipa fursa ya kujuana na watu wengi wa nje.

Nachukua fursa hii kutangaza rasmi kwamba nitachukua fomu ya kugombea Ubunge kutokana na kukidhi vigezo vyote ya kugombea nafasi hii kama ilivyojieleza katika Katiba ya Tanzania ibara ya 67.-(1) ambayo pamoja na mambo mengine inasema  “Bila ya kuathiri masharti yaliyomo katika ibara hii, mtu yeyote atakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge endapo-
(a)    ni raia wa Jamhuri ya Muungano aliyetimiza umri wa miaka ishirini na moja, na ambaye anajua kusoma na kuandika katika Kiswahili au Kiingereza;
 
Mimi ni mzaliwa wa Kijiji cha Mofu, wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro, Juni 26, 1976. Nimewahi kufanya kazi katika vyombo mbalimbali vya habari ndani na nje ya nchi ikiwamo the Guardian Limited kama mwandishi wa kujitegemea, Uwazi kama Mhariri, Leo ni Leo kama Mhariri wa Makala, Mwananchi kama Mwandishi wa makala baadaye mhariri wa jarida la ndani ya biashara, the Media Project (Marekani) kama mchangiaji nk.
 
Kwa sasa ni Kiongozi wa Utafiti hapa nchini (National Lead Researcher) wa taasisi ya kimataifa iitwayo Global Integrity yenye makazi yake Marekani, pia ni Mhariri Mtendaji wa gazeti la Mwanahabari, lakini maamuzi haya ya kugombea ubunge ni yangu binafsi hayana uhusiano wala hayataingiliana na sehemu yoyote ninayofanyia kazi.
 
Nimewahi kutembea katika nchi mbalimbali kwa lengo la kwa kusoma na kutembea, baadhi yake ni Marekani, Kenya, Uganda, Dubai, Thailand, India.
 
OMBI KWA WASAMARIA WEMA
Napenda kuchukua fursa hii pia kuwaomba wasamaria wema kuangalia namna ya kusaidiana na wananchi wa Kilombero kwani wakati huu njia nyingi hazipitiki kwa sababu barabara zimejaa maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha. Magari yamekuwa hayapitiki katika maeneo mengi ya Kilombero kwa sasa.
 
Kwa mfano sehemu kubwa ya barabara ya kutoka  Ifakara kwenda Mofu haipitiki, kiasi kwamba wagonjwa wamekuwa hawawezi kubebwa kupelekwa Ifakara ambako ndiko pekee kuna hospitali ya Wilaya, St Francis. Wapo baadhi ya wagonjwa wamekuwa wakibebwa kwa kutumia baiskeli na hata pikipiki, jambo ambalo limekuwa gumu hasa kwa wajawazito.
 
Magari ya abiriia hasa Noah zilizokuwa zikifanya safari kutoka na kuingia Ifakara kutoka vijiji mbalimbali vya Wilaya ya Kilombero yamesitisha safari kutokana na barabara kujaa maji. Yapo magari machache hasa ya mizigo ambayo nayo yanafika baadhi ya vijijini kwa shida yakiwa yamebeba mizigo na abiria hivyo kuhatarisha usalama wa wananchi.
 
Mvua zimeathiri pia kilimo, kwani mashamba mengi yamefurika maji, huku kukiwa na njaa kwa baadhi ya wanavijiji. Hivyo nachukua fursa hii kuiomba Serikali kuchukua hatua za haraka kusaidia wananchi wakiwamo wa vijiji vya Mofu, Ihenga, Mlimba,
 
Imetolewa Mei 12, 2014, saa saba mchana
na Dismas Lyassa                                 
(Mtangaza nia ya kugombea Ubunge Jimbo la Kilombero kwa tiketi ya CCM) 
0754 49 8972/0712183282 

STARS YAWASILI RUSTENBURG

$
0
0
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imewasili leo mchana majira ya saa 6 kamili katika jiji la Rustenburg na kufikia katika hoteli ya Hunters Rest - Protea iliyoypo pembeni kidogo ya  jiji.

Taifa Stars ambayo iliondoka jana joni jijini Dar es salaam jijini Dar es salaam na kufika OR Tambo saa 5 usiku, ilipata mapokezi mazuri kutoka kwa waandaji wa michuano ya COSAFA pamoja na watanzania wanaoishi jijini humo, ililala katika hoteli ya Southern Sun.

Safari ya kutoka Johannesburg kuelekea Rustenburg ilichukua takribani masaa mawili na msafara wa Taifa Stars unaongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF Ephaphra Swai.

Wachezaji waliopo na timu Rutsenburg ni Deogratius Munish, Mwadini Ali, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Oscar Joshua, Haji Mwinyi, Salim Mbonde, Aggrey Moriss, Joram Mgeveke, Said Juma, Hassan Dilunga, Said Ndemla, Abdi Banda, Mwinyi Kazimoto, Ibhrami Ajib, Juma Luizio, John Bocco, Mrisho Ngasa na Saimon Msuva.

Kikosi cha Taifa Stars kinatarajiwa kufanya mazoezi leo jioni katika uwanja wa Rustenburg Impala Bowling Club majira ya saa 10 kamili jioni kwa saa za Afrika Kusini sawa na saa 11 jioni kwa Afrika Mashariki.


IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

CRDB yataka BOT isishinikizwe

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu mdororo wa shilingi. Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja, Tully Mwambapa.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Dk. Charles Kimei.

Na Mwandishi Wetu

WADAU wa maendeleo nchini hususani wanasiasa, wametakiwa kuacha tabia ya kuishinikiza Benki Kuu ya Tanzania (BOT), kudhibiti mdororo wa shilingi ya Tanzania, kwani si njia sahihi na badala yake waache thamani ya fedha hiyo kukua kulingana mahitaji ya kiuchumi.

Wito huo umetolewa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei alipokuwa akizungumzia kushuka kwa thamani ya shilingi ya Tanzania na kusema mashinikizo kutoka kwa wadau hao yanaziathiri taasisi za kifedha, hususani mabenki.

Dk Kimei alisema kuwa shinikizo hilo, linailzimu kwa BOT kuyaminya mabenki, kwani njia nzuri inayotumiwa na taasisi hiyo katika kuzuia anguko hilo na mabadiliko ya fedha za kigeni ni kubana sera za kifedha na kuondoa zaidi shilingi katika mzunguko wake.

“Moja ya athari za kuondoa shilingi katika mzunguko wake ni kupanda kwa riba miongoni mwa watumiaji wa huduma za kibenki, hivyo kupunguza nia ya kukopa waliyonayo wateja wetu na kuathiri mzungunko wetu wa fedha,” alisema Dk. Kimei.

Aliwataka wadau hao, hasa wanasiasa waguswe kwa namna moja ama nyingine na ukuaji huo wa riba kwa Mtanzania wa kawaida ambao unaathiri harakati za maendeleo, na kwamba waelekeza nguvu zao katika hilo ili kupunguza ukali wa maisha na kuleta maendeleo ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Alisisitiza kuwa, thamani ya mabadiliko ya fedha ya kigeni ni muhimu katika ukuaji wa uchumi na kuwataka wadau wa maendeleo kujielekeza katika kuiacha shilingi ipande thamani yenyewe kulingana na taratibu za kiuchumi na sio kwa shinikizo.

Hata hivyo alikiri kuwa wao kama taasisi za fedha nchini wanatambua athari za kushuka kwa thamani ya shilingi ambazo ni pamoja na kupunguza wawekezaji wapya kutoka nje, lakini akaonya kuwa kulazimisha nguvu ya shilingi dhidi ya dola kunalipunguzia taifa nguvu ya ushindani kibiashara katika soko la kimataifa.

TUME YA MIPANGO YATEMBELEA BANDARI YA DAR ES SALAAM

$
0
0
Meneja wa Mipango na Mikakati wa Mamlaka ya Bandari Tanzania, Bw. Ntandu Mathayo (Kulia) akiukaribisha ugeni kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango walipokwenda kujionea maendeleo ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa katika Bandari ya Dar es Salaam. Kushoto ni Kiongozi wa Msafara huo, Bibi Florence Mwanri. Wengine pichani ni Bw. Aloyce Andrea (Wapili Kushoto), Bw. Robert Senya (Katikati) na Bw. Abel Shirima.   
Meneja wa Mipango na Mikakati wa Mamlaka ya Bandari Tanzania, Bw. Ntandu Mathayo (Wapili Kushoto) akizungumza wakati ugeni kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango walipokwenda kujionea maendeleo ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa katika Bandari ya Dar es Salaam. Wanaomsikiliza ni Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Bibi Lucy Kazibure (Kushoto) na wageni kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.
Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Bibi Lucy Kazibure (Kushoto) akizungumza na ugeni kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango walipokwenda kujionea maendeleo ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa katika Bandari ya Dar es Salaam. Ugeni huo uliongozwa na Naibu Katibu Mtendaji (Huduma za Jamii na Masuala ya Idadi ya Watu) Bibi Florence Mwanri (Wapili Kushoto).
Kiongozi wa Msafara kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kushoto) akikaribishwa na Mkuu wa Sehemu ya Kushushia Mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam, Kapteni P. R. Paul (Kulia) wakati walipotembelea kujionea maendeleo ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa katika Bandari ya Dar es Salaam.
Mkuu wa Sehemu ya Kushushia Mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam, Kapteni P. R. Paul (Kulia) akitoa maelezo kuhusu hali ya upakuaji wa mafuta kwa ugeni kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango walipokwenda kujionea maendeleo ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa katika Bandari ya Dar es Salaam.
Meli ikipakua shehena ya mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam. PICHA NA SAIDI MKABAKULI

MWENYEKITI WA VUGUVUGU NCHINI BURUNDI AONGEA NA WANAHABARI HOTEL YA SERENA JIJINI DAR

$
0
0
Kikao Kikiwa kinaendelea Juzi usiku.
Mwenyekiti wa Vuguvugu kutoka nchini Burundi Bw. Mugwengezo Chauvineau akiongea na waandishi wa Habari  Serena Hotel Dar jana usiku .
Dkt. Christine Mbunyingingo Mwenyekiti wa wanawake na wasichana katika harakati za usawa Nchini Burundi, Akiongea na waandishi wa Habari jana usiku. 

*****
Mwenyekiti wa vuguvugu za Maandamano Burundi kwa Mara ya kwanza amefika Nchini Tanzania ili kuweza kushuhudia Mkutano wa Dharula kati ya viongozi watano wa Jumuia ya Afrika Mashariki  kuhusu nchi ya Burundi ambayo sasa imeingia katika machafuko baada ya Rais aliyepo Madarakani kutaka kuongeza muda wake.

Akiongea na Waandishi wa Habari usiku huu Mkuu huyo wa vuguvugu wa Burundi amesema kuwa wananchi hawaridhiki na Rais wao kuendelea kuwa madarakani ambapo hata sheria na katiba hairuhusu na pia sasa ni wiki ya tatu ambapo wananchi wanaendelea kupinga Rais kuendelea kuwania kwa Muhura wa Tatu.

Amezungumzia juu ya waandamanaji  baada ya wiki tatu bado wapo barabarani ambapo wameweza kuwa ni kiungo, wameweza kuwa ni njia kwa sababu wanadai kumekuwa na mabadiriko kuhusu Rais wao, na kuwashukuru waandamanaji hao kwa kuonesha moyo wa uzalendo na kuwa wameweza kudhihilisha na kuwa walikuwa ni watulivu na kutulia kungoja utekelezaji wa mambo ambayo yamezungumziwa.

Amesema kwamba anaomba vurugu hizi zipate kwisha ambapo watu zaidi ya laki mbili wamekimbia nchi na anaomba vurugu ziishe ili wapate kurejea nchini kwao.

Pia ameiomba Jumuia ya kimatafa iweze kufuatilia kwa karibu hali inayoendelea kwa sasa  Nchini Burundi ambapo jumuia iyo tangia zamani imeweza kusimamia mambo ya usalama nchini Burundi na amani ili Burundi iweze kufikia malengo ya Mkataba wa amani wa Arusha na kufikia malengo ya katiba ambayo ndio uti wa mgongo wa taifa hilo.

Kuhusu jaribio la Mapinduzi kiongozi huyo amesema hayupo Miongoni mwa wale ambao wameandaa tukio hilo 

Kuhusu jambo baya alilofanya Rais wa Burundi Kiongozi huyo amaesema kwamba ni kuongezea Muhula wakati tayari alisha tawala kwa Miaka 10, na katika miaka hiyo alishindwa kuweka usawa baina ya warundi, hajatekereza swala la haki za Binadamu , aliongeza kuwa Muhura wake ni Muhura baki na Haramu hauko sambamba na Katiba wala Sheria ya Burundi pamoja na Mkataba wa Arusha na angetekeleza yote hayo hizi vurugu zisinge kuwepo. Pia hata makubaliano ya Arusha yanasema hakuna Rais ataenda Mihula mitatu. Pia warundi wanafanya hivyo kwa sababu hawataki shuhudia tena Damu inamwagika.

Mwisho amewaomba Marais watano wamalize salama Mkutano na kuhakikisha maamuzi yote yanafanyiwa kazi.

Nae Mwenyekiti wa wanawake na wasichana katika harakati za usawa amewashukuru kwa uvumilivu wao na kuendelea kupinga Rais wao kuendelea kuwa madarakani kwa awamu ya Tatu.

RAIS NKURUNZIZA AREJEA BURUNDI

$
0
0

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza anasema amerejea nchini humo, huku Naibu Kiongozi wa Mapinduzi akikiri kuwa jaribio la kumuangusha Nkurunziza limeshindwa. Umoja wa Mataifa umetaka kurejeshwa haraka utawala wa sheria.


Mshauri Mwandamizi wa mawasiliano wa Rais Willy Nyamwitwe, alisema Nkurunziza amerejea nchini humo, lakini hakutoa maelezo zaidi kwa kile alichosema ni sababu za kiusalama. 

Nkurunziza alikuwa nchi jirani ya Tanzania kwa ajili ya mazungumzo ya kikanda siku ya Jumanatano wakati mapinduzi yalipotangazwa na Jenerali Godefroid Niyombere, na kufunika wiki kadhaa za maandamano dhidi ya jaribio la rais kutafuta muhula wa tatu.

Taarifa za kurejea kwa rais Nkurunziza hazikuweza kuthibitishwa na duru huru hata hivyo, na uwepo wake umeendelea kuwa kitendawili usiku wa Alhamisi. Lakini tangazo kwamba amerudi lilifuatia haraka na kukiri kwa naibu kiongozi wa mapinduzi Cyrille Ndayirukiye kwamba mapinduzi hayo yameshindwa. Ndayikuriye aliliambia shirika la habari la Ufaransa AFP, kuwa binafsi anatambua kuwa vuguvu lao limeshindwa.

 Waandamanaji wanaompinga Nkurunziza wakishangalia baada ya kutangazwa kwa mapinduzi.

Waandamanaji wanaompinga Nkurunziza wakishangalia baada ya kutangazwa kwa mapinduzi.

Watiifu wadhibiti vituo muhimu

Mapema Alhamis, wanajeshi watiifu kwa rais walisema walizuwia mashambulizi mawili makubwa yaliyofanywa na wapinzani katika mapambano makali ya kudhibiti kituo chenye umuhimu wa kimkakati cha redio ya taifa. Miili ya wanajeshi watatu ilionekana ikiwa imelala mitaani karibu na eneo la mapigano hayo, ishara ya kwanza ya maafa katika kadhia hiyo ya mapinduzi. Kufikia mchana, mkurugenzi wa kituo hicho Jerome Nkokirantevye alisema wanajeshi watiifu ndiyo walikuwa wanakidhibiti kituo hicho.

Afisa mwanadamizi wa polisi alithibitisha taarifa hizo na kusema jana jioni kuwa wanajeshi wanaounga mkono mapinduzi walisambaratika baada ya mashambulizi yao dhidi ya Televisheni ya taifa RTNB na jengo la redio katika mji mkuu kukandamizwa. Alisema baadhi ya waasi tayari wamejisalimisha na wengine walikimbia.

Tangazo la mapinduzi la Jumatano lilisababisha ukosoaji kutoka sehemu mbalimbali za dunia, na kuibua hofu ya kurejea katika vurugu kubwa katika taifa hilo maskini, ambalo bado linaedelea kuhisi athari za vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka 13 vilivyomalizika mwaka 2006, na kugharimu maisha ya maelfu ya Warundi.

 Kibonzo hicho kilichorwa na Said Michael kutoka Tanzania, kuelekea mkutano wa kilele wa kujadili mgogoro wa Burundi.
Kibonzo hicho kilichorwa na Said Michael kutoka Tanzania, kuelekea mkutano wa kilele wa kujadili mgogoro wa Burundi.
Baraza la Usalama laonya.

Marekani ilisisitiza Alhamis kuwa Nkurunziza ndiye rasi halali wa Burundi bado. Nalo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lililokutana katika kikao cha dharura siku ya Alhamis, lililaani jaribio hilo la mapinduzi, na kutaka kurejeshwa haraka kwa utawala wa sheria na kufanyika kwa uchaguzi kwa kuzingatia makubaliano ya Arusha.

Katika taarifa iliyosomwa na Raimonda Murmokaite, balozi wa Lithuania katika Umoja wa Umoja wa Mataifa, na rais wa barala hilo kwa mwezi wa Mei, baraza hilo lenye wanachama 15 lilieza utayarifu wake kuchukulia hatua vitendo vya vurugu nchini Burundi vinavyotishia amani na usalama.

"Wanachama wa baraza la usalama wamelaani machafuko nchini Burundi na hasa wamewalaani wanaochochea vurugu za aina yoyote dhidi ya raia, na wale wanaotaka kutwaa madaraka kwa njia zisizohalali," alisema Murmokaite.

"Wanachama wa baraza la usalama wametoa wito kwa pande zote kutotumia vurugu na kutoa kipaumbele kwa amani na usalama. Baraza pia limerejelea uungaji wake mkono wa juhudi la mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa Said Djinnit, Umoja wa Afrika na Jumuiya ya Afrika Mashariki."

 Wakimbizi wa Burundi waliowasili nchini Tanzania kufuatia machafuko yanayoendelea nchini mwao.
Wakimbizi wa Burundi waliowasili nchini Tanzania kufuatia machafuko yanayoendelea nchini mwao.

Maelf wakimbilia nchi jirani Katika taarifa iliyotangazwa kupitia redioni, rais Nkurunziza alisema analilaani kundi la waliokula njama, na kuwashukuru wanajeshi wanaorejesha utengamano, na kwamba anawasamehe wanajeshi wanaoamua kujisalimisha. Umoja wa Mataifa unasema zaidi Warundi 70,000 wamekimbilia nchi jirani, na kuivuruga kanda hiyo yenye historia ya mapigano ya kikabila.

Wapinzani wanasema jaribio la rais kugombea muhula wa tatu linakiuka katiba na makubaliano ya amani yaliyokomesha vita vya wenyewe kwa wenyewe. Hukumu ya mahakama ya katiba hata hivyo, ilisema rais anaweza kusimama tena, ikibainisha kuwa muhula wake wa kwanza, alipochaguliwa na bunge badala ya kura ya wananchi, haukuhesabiwa. Lakini wakosaoji wanasema mahakama hiyo ina upendeleo.
Chanjo cha habari DW.

Changamoto maboresho usimamizi wa fedha za umma zatajwa

$
0
0
Kulia ni Mratibu wa Moboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (Public Finance Management Reform Progamme – PFMRP) akifafanua jambo juu ya utekelezaji wa mradi huo kwa wanahabari. Mratibu wa Moboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (Public Finance Management Reform Progamme – PFMRP) akifafanua jambo juu ya utekelezaji wa mradi huo kwa wanahabari.Baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakifuatilia mada mbalimbali. Baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakifuatilia mada mbalimbali.Msemaji wa Wizara ya Fedha Ingiahedi Mduma (katikati) akiuliza swali kwa Mratibu wa Mradi wa Moboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (Public Finance Management Reform Progamme – PFMRP) hayupo pichani. Msemaji wa Wizara ya Fedha Ingiahedi Mduma (katikati) akiuliza swali kwa Mratibu wa Mradi wa Moboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (Public Finance Management Reform Progamme – PFMRP) hayupo pichani.Kulia ni Mratibu wa Moboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (Public Finance Management Reform Progamme – PFMRP) akifafanua jambo juu ya utekelezaji wa mradi huo kwa wanahabari. Kulia ni Mratibu wa Moboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (Public Finance Management Reform Progamme – PFMRP) akifafanua jambo juu ya utekelezaji wa mradi huo kwa wanahabari.Baadhi ya washiriki wa semina ya Wizara ya Fedha kwa wanahabari juu ya utekelezaji wa mradi wa PFMRP. Baadhi ya washiriki wa semina ya Wizara ya Fedha kwa wanahabari juu ya utekelezaji wa mradi wa PFMRP.

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
 PROGRAMU ya Moboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (Public Finance Management Reform Progamme – PFMRP) imetaja changamoto zinazoukabili mradi huo licha ya mafadikio mengi iliyoyapata wakati mradi huo ukiingia awamu ya nne ya utekelezaji wake. Mratibu wa Mradi huo ametaja changamoto hizo leo mjini Kibaha alipokuwa akiwasilisha mada kwa waandishi wa habari pamoja na waendeshaji wa mitandao ya jamii ikiwa ni hatua ya kushirikisha vyombo vya habari juu ya utekelezaji wa mradi huo. 

Mratibu huyo alizitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na ugumu wa kuunganisha mifumo mbalimbali ya kifedha inayotumika serikali ili mifumo hiyo iweze kuongea kwa pamoja, ugumu wa kujenga uwezo katika maeneo ya kitaalamu kama E-procurement na ICTs, Uhaba wa fedha za ndani katika kutekeleza program na changamoto nyingine katika utekelezaji mradi. Alisema mradi huo unaofadhiliwa kwa pamoja na washirika wa maendeleo pamoja na Serikali ya Tanzania tayari umeingia awamu ya nne ambapo lengo kuu la awamu hii ni kudumisha nidhamu katika usimamizi wa Fedha za Umma na kutoa huduma bora kwa umma ili kuleta maendeleo endelevu.

 Aidha alisema licha ya changamoto zilizopo katika utekelezaji mradi huo yapo mafanikio hasa katika awamu ya nne ambayo ni pamoja na programu kufanikiwa kuunganisha mfumo wa usimamizi wa fedha nchi nzima katika serikali kuu na serikali za mitaa, kufanikiwa kufanya utafiti wa namna Halmshauri za Wilaya/Miji inavyoweza kuongeza mapato na kufanyika kwa zoezi la PEFA mwaka 2013 na hivyo kuibua mapungufu yaliyopo katika usimamizi wa fedha za umma. 


Mradi pia umefanikiwa kuimarisha ushirikishaji wa utayarishaji wa bajeti kuanzia ngazi za chini, kutumika kwa mfumo wa SBAS ambao unatoa fursa ya kuingiza mahitaji ya Mpango wa miaka mitano na kugawa rasilimali na pia kuchapishwa kwa taarifa ya utekelezaji wa bajeti, ukaguzi mbalimbali hivyo kuongeza kiwango cha uwazi. Mengine ni pamoja na kutungwa kwa sheria mpya ya Ununuzi wa Umma Na. 7 ya 2011 badala ya sheria iliyokuwepo Na. 21 ya 2004. Sheria hii pamoja na mambo mengine imeiweka PPRA kutoshughulikia masuala ya michakato ya ununuzi, na kubaki na shughuli yake kuu ya kutoa miongozo ya ununuzi wa umma. 

 Vile vile sheria imeongeza kiwango cha uwazi zaidi katika michakato ya ununuzi wa umma. "...Kujenga uwezo wa watumishi katika kufanya kazi zao zinazohusiana na usimamizi wa fedha za umma. Kwa mfano mafunzo kadhaa yalitolewa kwa wahasibu, wakaguzi, wachumi; maafisa wa ununuzi...kwa lengo la kuongeza ufanisi katika kulitumikia taifa. Kuandaa na kutoa taarifa za kifedha chini ya mfumo wa IFMS ili kufikia vigezo vya kimataifa (IPSAS), Kuwekwa kwa mfumo wa kusimamia mali za serikali (Asset tracking software) katika ofisi zote za kurugenzi ya Usimamizi wa Mali za Serikali." Alisema Mratibu huyo. 

Mafanikio mengine ni kuongezeka kwa uwezo wa NAOT hata kufikia kiwango cha hatua ya 3 ya AFROSAE, uhuishwaji wa mifumo ya fedha kama EPICOR ili iweze kufanya kazi kwa ufanisi zaidi (k.m. mfumo wa EPICOR toleo la 7.3.5 ulibadilishwa na kuingizwa toleo la 9.05 wenye modules nyingi zaidi kuliko ule wa mwanzo, Kufanyika kwa zoezi la uhamishaji wa fedha kwenda serikali za mitaa na kuweka Mpango Kazi ili kuboresha uhamishaji wa fedha toka serikali kuu kwenda kwenye LGAs. 

Mratibu alibainisha kwa sasa Ofisi ndogo za hazina zote nchini zimewekewa mfumo wa IFMS, na hivyo kuongeza ufanisi, Uandaaji na utoaji wa taarifa ya fedha za serikali kwa kutumia mfumo wa IFMS na kwa kufuata mifumo ya kimataifa ya International Public Sector Accounting Standards Cash Basis (IPSAS). Mradi wa PFMRP ulianzishwa mwishoni mwa miaka ya 1990, ukiwa na lengo la kuimarisha usimamizi, kuongeza uwazi na uwajibikaji na kujenga nidhamu ya fedha za umma katika serikali na taasisi zake, huku ikitekelezwa sambamba na programu nyingine za kitaifa katika sekta ya umma.
  *Imeandaliwa na www.thehabari.com

FOMU ZA URAIS CHADEMA SH.MILIONI MOJA

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zanzibar, Salum Mwalimu akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuhusu mchakato wa uchukuaji fomu, uchujaji na uteuzi wa wagombea ndani ya chama kwa ajili ya uchaguzi mkuu 2015. Kulia ni Mkurugenzi wa Bunge na Hakmashauri, John Mr
ema. (Picha na Francis Dande)

CHADEMA YAILALAMIKIA CCM KWA UKIUKWAJI WA SHERIA

$
0
0

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kinadaiwa kuvunja Sheria na kanuni za uchaguzi wa serikali za mitaa, kwa kujihusisha na vitendo vya rushwa ili kuwashawishi wananchi wa Kijiji cha Mtambani Kata ya Bwiringu, Chalinze mkoani Pwani, kukichagua chama hicho.

Kijiji hicho kinatarajiwa kufanya uchaguzi mdogo wa serikali za mitaa kesho, baada ya ule uliyofanyika Desemba 14 na 21 mwaka jana kukumbwa na dosari lukuki zulizosababisha kuahishwa kwa uchaguzi huo.

Akizungumza kwa njia ya simu kutokea katika jimbo hilo la Chalinze, Katibu wa Operesheni, Mikakati, Propagandi na Mafunzo Mkoa wa Pwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Juma Mwipopo, alisema wanafuatilia kwa karibu ukiukwaji huo wa sharia.

Aliitaja sheria hiyo kuwa ni ile ya uchaguzi na kanuni za uchaguzi wa serikali za mitaa na vitongoji sura namba 287 kifungu cha 201(A), tangazo la serikali namba 320 la 5/9/2014 pamoja kifungu cha 18.

Mwipopo, alisema kifungu hicho cha 18 kinaeleze kinakataza ngombea au chama kujihusisha kampeni zinazoashilia vitendo vya rushwa, kashfa, ubaguzi wa kijinsia, udini na ukabila.

Alisema pamoja na sheria na kanuni za uchaguzi wa serikali za mitaa kuwa wazi, Mei 11 mwaka huu CCM kilizindua kampeni zake, ambapo walitoa fulana, jezi na mipira katika shule na wananchi ikiwa ni kuwashawishi ili waweze kukichagua chama hicho kwenye uchaguzi huo.

“Pia waliendelea kuvunja kanuni hizo kwa kuwaambia wananchi wa kijiji cha mtambani kwamba wakikichagua Chadema watawafukuza wafugaji wote, niwaombe wafugaji kuzipuuza kauli hizo kwani Chadema ni chama makini ambacho kazi yake kubwa ni kupigania haki za wananchi wote bila ya kubagua popote pale nchini,”alisema Mwipopo.

Alisema Chadema siyo chama cha kibaguzi wala kikabila bali ni chama cha wananchi kutoka maeneo yote ya Jamhuri ya Muungano, hivyo wanaokifananisha na udini na ukabila ni watu waliofilisika kisiasa. 

Katibu huyo, alisema kuwa wananchi wa Mtambani hawahitaji fulana, mpira bali wanahitaji barabara, maji na huduma bora za afya, ambazo CCM, imeshindwa kuwafikishia tangu nchi ilipopata uhuru mwaka 1964.

STARS YAENDELEA KUJIFUA

$
0
0
 Wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' wakiwa katika mazoezi katika uwanja wa Olympia Park kujiandaa na mchezo wa fungua dimba dhidi ya timu ya Taifa ya Swaziland.

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imeendelea na mazoezi katika uwanja wa Olympia Park kujiandaa na mchezo wa fungua dimba dhidi ya timu ya Taifa ya Swaziland.

Kocha mkuu wa timu ya Taifa Stars Mart Nooij amesema vijana wake wanaendelea vizuri na mazoezi, ikiwa leo ni siku ya pili kufanya mazoezi baada ya kufanya mazoezi ya kwanza jana jioni.

Nooii amesema japokuwa kuna hali ya hewa ya baridi katika mji wa Rustenburg, wachezaji wake wameanza kuizoea na kusema kwa kuwa bado kuna zaidi ya masaa 72 kabla ya mchezo wa awali watakua wameshaizoea hali ya hewa.

Kuhusu uwanja wa mazoezi, kocha Nooij amesema hali ya uwanja ni nzuri, uwanja una nyasi nzuri hali inayopelekea kikosi chake kufanya mazoezi katika mazingira mazuri.

Akiongelea mchezo wake wa kwanza wa ufunguzi dhidi ya timu ya Taifa ya Swaziland utakaochezwa siku ya jumatatu, amesema anawajua Swaziland ni timu nzuri, mara ya mwisho katika mchezo wa kirafiki walitoka nao sare, hivyo anawaanda vijana wake kupata ushindi katika mchezo huo.

Kikosi cha Swaziland kina wachezaji mchanganyiko wakiwemo wanaocheza ligi yao ya nyumbani na baadhi wanaocheza soka la kulipwa nchini Afrika Kusini.

Taifa Stars itacheza mchezo wa kwanza dhidi ya Swaziland katika Uwanja wa Olympia Park siku ya jumatatu saa 1.30 usiku kwa saa za huku, sawa na saa 2.30 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

NB: Picha za mazoezi za Taifa Stars zimeambatanishwa

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

MBUNGE JAMES MBATIA APENDEKEZA SHULE BINAFSI ZIPEWE RUZUKU TOKA SERIKALINI

$
0
0
Wanafunzi wanaohitimu kidato cha sita katika shule ya sekondari ya Maua Seminary wakiimba wimbo wa taifa wakati wa mahafali ya kuhitimu kidato cha sita yaliyofanyika shuleni hapo.
Mkuu wa shule ya sekondari Maua seminari ,Erastus Tesha akizungumza katika mahafali ya 33 kwa wahitimu wa kidato cha sita yaliyofanyika shuleni hapo.
Mgeni rasmi katika mahafali hayo ,mbunge wa kuteuliwa na rais ,Mh James Mbatia akizungumza na wanafunzi wa shule hiyo pamoja na wageni waalikwa .
Baadhi ya wageni waliofika shuleni hapo kwa ajili ya mahafali ya ndugu zao wanaotarajia kuhitimu kidato cha sita katika shule ya sekondary ya Maua.
Mkuu wa shule ya sekondari ya Maua Seminari akimkabidhi Mbatia zawadi kutokana na kazi anayoifanya ya kutetea elimu ya Tanzania.
Mgeni rasmi katika sherehe hiyo ,Mbunge Mbatia akitoa zawadi ya keki kwa wanafunzi wanaohitimu kidato cha sita katika shule ya sekondary Maua Seminary.
Mgeni rasmi katika mahafali ya 33 ya kidato cha sita katika shule ya sekondari ya Maua,James Mbatia akiwa katika picha ya pamoja na walimu pamoja na wahitimu.
Mbunge Mbatia akiongozwa na mkuu wa shule ya sekondari ya Maua Seminary,Erastus Tesha kutembelea maeneo mbalimbali ya shule hiyo.
Baadhi ya majengo yaliyopo katika shule ya sekondary Maua Seminary.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Knada ya Kaskazini.

WAZIRI NYALANDU ADAI NASSARI MZUSHI ANAYETAPATAPA

$
0
0
Na Mwandishi wetu
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, amesema kauli zilizotolewa Bungeni na Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari, ni za kutapatapa na zimejaa ukosefu wa busara na uzushi.

Amesema mbunge kusimama bungeni na kutoa kashfa badala ya kueleza masuala ya kisera au kiutendaji ni kupungukiwa busara na jamii haina budi kumpuuza.

Akichangia hotuba ya Ofisi ya Waziri Mkuu bungeni juzi, Nassari alisema Nyalandu kazi yake kubwa ni kuzunguka katika mapori ya akiba na kupiga picha na askari pamoja na kushangaa mbwa wa kizungu na kupokea ndege, helkopta za msaada. Alisema utendaji huo na mawaziri wengine unaweza ukawa ni ishara ya serikali iliyochoka.

Hata hivyo, katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Nyalandu alisema Nassari anapaswa kuwakilisha na kutetea wapigakura wake kwa hoja badala ya kuropoka masuala ambayo hayana tija.
Alisema kauli zinazotolewa na wapinzani bungeni akiwemo Nassari kuishutumu serikali kuwa imechoka na kujaribu kuichonganisha na wananchi, kamwe hakuwezi kuikatisha tamaa kwa kuwa uzushi kwa upinzani ni jambo la kawaida.

Alikumbusha kuwa mapema mwaka huu alifanya ziara wilayani Arumeru ikiwemo jimbo la Nassari kutatua mgogoro baina ya wananchi na hifadhi, ambapo mbunge huyo alimtia moyo na kumtaka kupuuza kauli za kukatisha tamaa zinazotolewa dhidi yake.

“Hizi kauli za Nassari ni za kitoto na haziwezi kuleta tija kwa wapigakura wake…asimame kuzungumzia utendaji na masuala ya kisera sio kashfa ambazo hazipo…Namshauri awatumikie wapiga kura wake.

Nilifanya ziara jimboni kwake kutatua mgogoro na alinitia moyo kutokata tamaa na kauli za watu wanaonibeza na kunipongeza kwa utendaji kazi wangu,” alisema Nyalandu katika taarifa yake.

Taarifa hiyo pia ilikariri kauli ya Nassari aliyoitoa katika mkutano wa viongozi wa mikoa ya Arusha na Kilimanjaro, ambapo mbunge huyo na Aggrey Mwanry (Siha) walihudhuria akisema: “Naomba kukutia moyo kwani anayefanya kazi ya Mungu atapata nguvu, nikisikia mtu bungeni anasema wewe ni waziri mzigo, mimi nitaruka juu na kumwangukia vibaya.”

Imeeleza kuwa mafanikio makubwa ambayo wizara hiyo imepata kwa kumaliza migogoro ya ardhi mingi kwa muda mfupi wakati alipotembelea mapori ya akiba na hifadhi za taifa zenye migogoro ya ardhi na wananchi na kuipatia ufumbuzi.

Akiwa huko amekuwa na utaratibu wa kuzungumza na askari wa wanyamapori pamoja na wananchi kusikiliza kero zinazowakabili.

Miongoni mwa maeneo ambayo Nyalandu ametembelea ni wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya, ambako kulikuwa na mgogoro wa ardhi kati ya wananchi wa vijiji 21 na Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, uliodumu kwa miaka zaidi ya mitano bila kupatiwa ufumbuzi.

Nyalandu alimaliza mgogoro huo kwa kuruhusu wananchi wa vijiji hivyo kuendelea na maisha kama kawaida na kuagiza kufanyika kwa ukaguzi wa mipaka ya eneo hilo upya.

Awali, wananchi wa Mbarali waliishitaki serikali kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, ambaye aliitaka serikali kumaliza mgogoro huo kwa maslahi ya wananchi.

Maeneo mengine yenye mgogoro ambayo Nyalandu alifanya ziara kwa lengo la kutoa ufumbuzi ni Pori la Burigi wilayani Biharamulo, Iringa, Masasi, Lamadi ambako alikutana na wafugaji kutoka mikoa yote nchini pamoja na Hifadhi ya Taifa ya Saadani wilayani Bagamoyo ambako pia kulikuwa na mgogoro wa ardhi.

“Ninapofanya ziara natekeleza majukumu yangu kama waziri, siwezi kukaa ofisini wakati kuna mgogoro baina ya wananchi na hifadhi za taifa na mapori ya akiba…nina dhamana ya kushughulikia mambo haya hivyo, kauli za kitoto kamwe haziwezi kunikatisha tamaa,” aliongeza Nyalandu.

Aidha, aliongeza kuwa katika kuhakikisha serikali inashinda vita dhidi ya ujangili, amekuwa mstari wa mbele kushirikiana na wadau wa uhifadhi na kwa jitihada zake amefanikisha kupatikana kwa ndege, helkopta na vifaa vingine ili kukabiliana na majangili.

Alisema vifaa hivyo ikiwemo ndege, magari, helkopta, silaha na vitendea kazi vingine hukabidhiwa kwake na baadaye huvikabidhi kwa watendaji wake kwa ajili ya kukagiwiwa kwenye hifadhi za taifa na mapori ya akiba.

“Tumeanzisha vita dhidi ya majangili hivyo ni lazima tuwe na vitedea kazi vya kutosha, nimefanya jitihada za kupata helkopta, ndege, silaha za kisasa, magari na juzi Marekani imetupa mbwa maalumu ambao tutawatumia pia kwenye viwanja vya ndege na bandarini kwa usalama zaidi.

“Sasa Nassari anaumia kuona hizi jitihada zetu kama serikali katika kulinda rasilimali zetu au alitaka akabidhiwe yeye,” alihoji Nyalandu.

Akizungumza kupiga picha na askari wa wanyamapori, Nyalandu aliwapuuza watu wenye mawazo tofauti akisema si jambo baya kufurahi na wapiganaji wake, ambao wamekuwa wakitumia muda mwingi wa maisha yao msituni.

Alisema amekuwa na utaratibu wa kufurahi pamoja, kula na kunywa na askari wa wanyamapori pindi anapofanya ziara zake katika hifadhi na mapori ya akiba.

“Watu wenye nia mbaya siku zote ndio wamekuwa na imani potofu, ninapofanya ziara kwanza nawafikiria wapiganaji wetu wanaoishi msituni kukabiliana na majangili hatari…siwezi kwenda huko na kukunja sura kama tuna ugomvi bali baada ya kupeana maagizo ya kazi tunakuwa kitu kimoja, tunafurahi na kutiana moyo ili kuongeza ari ya kulinda rasilimali za taifa. Kauli zingine zinasikitisha mno,” alisema.
HABRI KATIKA PICHA
 WAZIRI Nyalandu akikagua gwaride la askari wa wanyamapori wakati akiwa
kwenye moja ya ziara zake.

 Waziri Nyalandu akikagua nyara a serikali zilizokamatwa kutoka kwa majangili alipokagua moja ya mbuga za wanyama kwenye moja ya ziara zake hivu karibuni
 NYALANDU akiwa kwenye picha ya pamoja na askari wa wanyamapori, maofisa na wafanyakazi wa Pori la Selous, muda mfupi baada ya kuzungumza nao na kupeana mikakati ya kiutendaji.

 Waziri Nyalandu akikagua meno ya tembo yaliyokamatwa kutoka kwa majangili kufuatia operesheni zinazofanywa na askari wa wanyamapori.
  WAZIRI Nyalandu (katikati) akiwa amezungukwa na wananchi wilayani Chemba alipokwenda kutatua mgogoro wa ardhi baina ya wananchi wa kijiji na hifadhi ya misitu.
 WAZIRI Nyalandu akiwa na wanafunzi wa Sekondari ya Selous wakati alipokuwa kwenye ziara ya kukagua shughuli za uhifadhi na vita dhidi ya ujangili, ambapo alipata fursa ya kuzungumza na wanafunzi shuleni hapo.
 WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akila chakula cha mchana na wanafunzi wa sekondari ya Selous, iliyopo Kijiji cha Lukuyu Sekamaganga wilayani Namtumbo, Ruvuma.
 WAZIRI Nyalandu akiwa katika picha ya pamoja na vijana wanaounda vikundi vya ulinzi kwa lengo la kukabiliana na ujangili kwenye maeneo ya Pori la Akiba la Selous wilayani Namtumbo.

WASTAAFU WA NSSF MKOA WA TEMEKE WAAGWA RASMI

$
0
0
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crescentius Magori akizungumza wakati wa hafla ya kuwaaga wastaafu wa shirika hilo kutoka ofisi ya mkoa wa Temeke.
Meneja Kiongozi mpya wa Ofisi ya NSSF Mkoa wa Temeke, Chedrick Komba akizungumza wakati wa hafla ya kuwaaga wastaafu wa NSSF.
 Mstaafu wa NSSF, Brahan Newa kutoka Kitengo cha Takwimu akisalimiana na mstaafu mwenzake, aliyekuwa Meneja Kiongozi, Ofisi ya NSSF mkoa wa Temeke, Yahya Mhamali wakati wa hafla ya kuwaaga iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Maofisa wa NSSF wakiwa katika hafla hiyo.
 Mstaafu, Brahan Newa akiwa na familia yake.
 Meneja Kiongozi mpya wa Ofisi ya NSSF Mkoa wa Temeke, Chedrick Komba (kushoto) akiwa na aliyekuwa Meneja Kiongozi wa Ofisi hiyo, Yahya Mhamali wakati wa hafla ya kuwaaga wastaafu wa NSSF ofisi ya mkoa wa Temeke.
 aliyekuwa Meneja Kiongozi wa Ofisi hiyo, Yahya Mhamali wakati wa hafla ya kuwaaga wastaafu wa NSSF ofisi ya mkoa wa Temeke.
Ofisa Mafao mstaafu wa NSSF, Margaret Mahege aakitoa neno la shukrani wakati wa hafla hyo.
Mstaafu Kitengo cha Takwimu NSSF, Brahan Newa akitoa shikrani zake wakati wa hafla hiyo. 
Ofisa Matekelezo mstaafu wa NSSF, Mohamed Kilumike akiwashukuru wafanyakazi wenzake kwa ushirikia wao wakati akiwa kazini. 
 Maofisa Waandamizi wa NSSF wakiwa katika hafla hiyo. 
Ofisa Matekelezo mstaafu wa NSSF, Mohamed Kilumike (kulia) akiteta jambo na mstaafu Kitengo cha Takwimu, Brahan Newa
Kutoka kushoto ni, Brahan New, Margaret Mahege na Yahya Mhamali wakikata keki wakati wa hafla ya kuwaaga.
Yahya Mhamali akilishwa keki wakati wa hafla ya kuwaaga wafanyakazi wa NSSF ofisi ya mkoa wa Temeke.
Margaret Mahege akilishwa keki.
Abrahan Newa akilishwa keki.
Picha ya pamoja. 
Maofisa wa NSSF.
Baadhi ya wafanyakazi wa NSSF ofisi ya mkoa wa Temeke.
Shukurani Masima (kushoto), Ummy Kimario wakifungua Shampeni.
Wastaafu wakitakiwa afya njema na maisha marefu.
 Cheers
 Cheers
  Cheers
 Cheers mama.
 Wastaafu wakiwa katika picha ya pamoja.
 Aboubakary Mshangama (kushoto) na Miraji Lipumba wakipeleka zawadi za wastaafu.
 Meneja Kiongozi mpya wa Ofisi ya NSSF Mkoa wa Temeke, Chedrick Komba akimkabidhi zawadi mstaafu wa NSSF, Mohamed Kilumike.
 Mstaafu wa NSSF, Brahan Newa kutoka Kitengo cha Takwimu akipokea zawadi yake kutoka kwa Meneja Kiongozi mpya wa Ofisi ya NSSF Mkoa wa Temeke, Chedrick Komba.
 Ofisa Mafao mstaafu wa NSSF, Margaret Mahege aakitoa neno la shukrani wakati wa hafla hyo.
Brahan Newa akishukuru kwa niaba ya wastaafu wenzake.
 Wastaafu pamoja na viongoi wa NSSF wakipata chakula.
 Wakati wa chakula.
 Ofisa Matekelezo mstaafu wa NSSF, Mohamed Kilumike akiwaongoza wafanyakazi wa NSSF kupata chakula.

Wafanyakzi wa NSSF wakipata chakula.
 Baadhi ya maofisa wa NSSF wakiwa katika picha ya pamoja.
 Wastaafu wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa NSSF
Muziki.

COASTAL UNION KUFANYA MKUTANO MKUU WA DHARURA

$
0
0

MKUTANO Mkuu wa Dharura wa Wanachama wa Klabu ya Coastal Union unatarajiwa kufanyika kesho Mei 17 mwaka huu kwenye ukumbi wa Bwalo la Polisi Mkoani Tanga.

Sababu za Mkutano huo kufanyika katika Ukumbi la Polisi Mesi ni
kutokana na makao makuu ya klabu ya Coastal Union kuendelea mchakato wa uandikishaji wa vitambulisho vya Taifa na upigaji picha wananchi kwa ajili ya vitambulisho hivyo.

Akizungumza leo, Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga  alisema maandalizi ya mkutano huo yanaendelea vizuri na unafanyika kufuatia vikao vya maridhiano ya Uhakikiwa wanachama wa Klabu ya Coastal Union ulioongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la soka nchini (TFF) Ahmed Iddi Mgoyi.

Ambapo alisema  baada ya kumalizika vikao hivyo, Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine aliiandikia barua Klabu ya Coastal Union akiiagiza klabu hiyo kuitisha mkutano mkuu wa dharura wa wanachama tarehe 17 Mei mwaka 2015.

Alisema kuwa matokeo  ya maamuzi haya yamepatikana baada ya kikao cha usuluhishi cha amani kilichoongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Ahmed Iddi Mgoi aliyekuwa ameongozana na Makamu Mkurugenzi wa Sheria na Uanachama shirikisho la soka nchini (TFF) Eliud Peter Mvella
kilichofanyika April 13 mjini hapa.

Aidha alisema kuwa tayari shirikisho la soka nchini (TFF) ilishatuma orodha tatu za majina Wanachama stahiki,Wanachama waliobainika kuwa wanadosari na inabidi wathibitishwe na wanachama stahiki.

Orodha nyengine ni waombaji wapya wa  wa uanachama watakaohakikiwa na wanachama stahiki ambapo utaratibu huo ndio ulioagizwa kutumika.

Hata hivyo alisema kuwa orodha zote zimekwisha kubandikwa kwenye ubao wa Matangazo wa Klabu ya Coastal Union tayari kwa ajili ya mkutano huo.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Coastal Union.

RAZA AWAPONDA WANAOTUMIA FEDHA KUWANIA MADARAKA

$
0
0
KADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mohammed Raza, ameshtushwa na baadhi ya wagombea wa nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano kumwaga mabilioni yafedha chafu Zanzibar ili kuwashawishi baadhi Wajumbe wa chama hicho kuwaunga mkuno katika mbio hizo.

Tanzania hivi sasa iko katika harakati za Uchaguzi Mkuu ambao unatarajiwakufanyika Oktoba mwaka huu.

Raza ambaye ni Mwakilishi wa Uzini, alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam jana, wakati alipozungumza na wandishi wa habari, kuhsu mustakakabali wa kupatikana Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa vile hilo ni suala nyeti katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.
“Suala hili lina unyeti wake kwani linagusa hadi majeshi na mahakama amabao nao wanapaswa kujua sifa za rais ajaye, hivyo haitakuwa busara kwa rais wa nchi apatikane kwa njia ya rushwa.

Alisema hivyo kwa vile kuna baadhi ya wawagombea wanafasi hiyo, wakishirikiana na wafanyabiashara tayari wanaendelea na mchezo huo mchafu wa kutoa rushwa waziwazi huku hata Kamati Kuu ya Chama Ikishindwa kukemea vitendo hivyo vya hatari kwa nchi.

“Nazungumzia chama changu, tumeingia kwenye uchaguzi mkuu, naamini bado tunakazi ya kutekeleza Ilani ya chama cha mapinduzi hatujamaliza kazi, sasa kama sisi viongozi tunaona mabilioni ya rushwa yakiingizwa dhahiri bila ya kukemewa imenishtua,”alisema.

Raza, alisema kitendo cha kupatikana rasi iliyetokana na misingi ya rushwa, itafika wakati rais huyo atashindwa kuwa na maamuzi ya kuongoza nchi na baadala yake atakuwa akitekeleza matakwa ya magenge ya watoa rushwa.

“Tunapompata rais ambaye amechaguliwa kwa misingi ya rushwa Watanzania wajue kuwa atakuwa akielezwa na waliomuingiza madarakani kwamba mchague huyu au yele ashike wizara fulani kwa ajili ya maslahi yao, lakini pia chama changu lazima kijue kuwa kuna Ukawa na CUF ambao nao wanataka kuingia madarakani,”alisema Raza.

Akizungumzia Suala Akaunti ya Tegeta Escrow, Raza, alisema kuwa Wazanzibar wanamtaka Waziri wa Fedha, atoe tamko atalifidiaje pengo Zanzibarkukosa misaada kutokuna naTanzania kuwekewa vikwazao na wahisani kutokana na kashfa ya Akaunt ya Tegeta Escrown.
Alisema, hivyo kwa vile kashfa hiyo haiwahusu  Wazanzibari, kwani halikuwa suala la muungano bali lilikuwa la Bara.

Hata hivyo, Raza, alisema bado viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibarr, wanatakiwa kuacha woga na baadala yake wajenge hoja kwa kuwaambia wahisani kuwa suala hilo haliwahusu Wazanzibari.
“Mwaka 1995  Zanzibar, iliwekewa vikwazo na huku bara ikidai kuwa iliambiwa na wahisani isiwape misaada, lakini kwa hili la Escro, viongozi wa Zanzibar walitakiwa kujenga hoja kwamba haliwahusu, angalia pale hakukua hata na Mzanzibari aliyehusika katika kashfa ya Tegeta Escro,”alisema Raza.
Raza, alisisitiza kuwa hata wakati wa EPA wazanzibari hawakuhusika lakini waliingizwa akibainisha kuwa hayo yote yanatokea kutokana na woga wa viongozi wa Serikali ya Zanzibar.
Aidha, Raza amesistiza kuwa alifuatilia suala hilo la vikwazo ili ikiwezekana Zanzibariweze kuondolewa vikwazo hivyo ambavyo anaamini haviihusu Zanzibara.
 Mwakilishi wa Baraza la Wawakilishi jimbo la Uzini (CCM), Mohamed Raza ( kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo juu ya mustakabali wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Vincent Tiganya. PICHA: MPIGAPICHA WETU
Viewing all 19659 articles
Browse latest View live