Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all 19659 articles
Browse latest View live

BENKI YA CRDB KUFANYA MKUTANO WA ISHIRINI WA WANAHISA JIJINI ARUSHA MEI-8

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akiongea na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari jijini Arusha akitoa taarifa ya mkutano mkuu wa ishirini  wa wanahisa wa Benki ya CRDB  unaotarajia kufanyika May 8  jijini Arusha.
SAM_2456Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, akizungumza na waandishi wa habari. Kushoto ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji Huduma Mtambuka Benki ya CRDB Bi.Esther Kitoka na kulia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji Uendeshaji na Huduma kwa Wateja Benki ya CRDB, Saugata Bandyopadhyay
SAM_2443Baadhi ya waandishi wa habari kutoka jijini Arusha wakiwa katika mkutano huo.
SAM_2437Meneja Mahusiano wa Benki ya CRDB, Godwin Semunyo akiwa katika mkutano huo.
SAM_2432Mkurugenzi wa Masoko,Utafiti na Huduma kwa Wateja, Tully Esther Mwambapa akiongea katika mkutano na waandishi wa habari katika maandalizi ya mkutano mkuu wa ishirini wa wanahisa wa Benki ya CRDB
SAM_2450Kulia ni Katibu wa Bodi ya CRDB, John Baptist Rugambo, katikati ni Mkurugenzi wa Fedha Frederick Nshekanabo, Kushoto Tully Esther Mwambapa ambaye ni Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja.
SAM_2454Mwandishi kutoka TV1, Arusha Jane Edward akijaribu kuchukua taswira katika mkutano huo.
SAM_2447 Meneja Kitengo cha Huduma kwa Wateja kwa njia ya simu, Ena Mwangama (kulia) na Edwin Nchimbi Ofisa Masoko wakifutilia mkutano huo.
SAM_2458Kulia ni Meneja Usajili wa Hisa kutoka Benki ya CRDB Emmanuel Ng’ui na Dorice Ngikari kutoka ofisi ya Katibu wakifatilia jambo
SAM_2460Mwandishi wa habari kutoka Mwananchi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Arusha Media Mussa Juma akiuliza swali kwa Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Crdb Dk. Charles Kimei.
Na Pamela Mollel, Arusha

Airtel yatoa punguzo kabambe la gharama za mawasiliano

$
0
0
 Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa huduma mpya inayotoa punguzo kabambe kwa gharama za kupiga simu ijulikanayo kama ‘Airtel Zone’, katika hafla iliyofanyika kwenye makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel, Levi Nyakundi na (kulia) ni Meneja Masoko wa Airtel, Ravi Agarwal.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya (katikati),  Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel, Levi Nyakundi (kushoto) na Meneja Masoko wa Airtel, Ravi Agarwal, wakionyesha bango kama ishara ya uzinduzi wa huduma mpya inayotoa punguzo kabambe kwa gharama za kupiga simu ijulikanayo kama ‘Airtel Zone’, katika hafla iliyofanyika kwenye makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.

·         Kufurahia punguzo la hadi asilimia 99 za kupiga simu ndani ya nchi
·         Pungunzo kwa wateja wa Airtel Nchi nzima
xxxxxxxxxxxxxxxxxx

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel inayoongoza kwa kutoa huduma bora na zenye ubunifu nchini leo  imeendelea kudhihirisha hilo kwa kuzindua huduma mpya inayotoa  punguzo kabambe kwa gharama za kupiga simu (Dynamic Tariffing) Itakayojulikamana kama “Airtel Zone”. Sasa wateja wa Airtel wa malipo ya awali sasa watafaidi kupiga simu kwa gharama ndogo yenye punguzo la hadi asilimia 99 kwa simu za nchini.

Huduma hii ya Airtel Zone imezinduliwa kwa mara ya kwanza na Airtel ili kuendeleza dhamira yake ya kutoa huduma nafuu za mawasiliano ya simu za mkononi na kutoa fursa kwa wateja wake kuongea zaidi kwa gharama nafuu mara tu watakapo jiunga kwa kupiga namba 107 na kufuata maelekezo au kupiga *149*39# kisha kuchagua ‘0’.

Akiongea wakati wa uzinduzi Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Bwana Levi Nyakundi alisema” uzinduzi wa punguzo la gharama za kupiga simu  ni uthibitisho wa dhamira ya kampuni ya Airtel kuwapatia watanzania dili lenye thamani halisia ya fedha zao na kuwawezesha watu wengi zaidi nchini kuwasiliana kirahisi. Lengo letu ni kuendelea kutoa huduma za kibunifu na zenye gharama nafuu ili kukithi mahitaji ya watanzania wote. Wateja wetu watakaojiunga na huduma ya “Airtel Zone” kuanzia leo, sasa hivi wataweza kupiga simu na kupata punguzo la hadi asilimia 99 na punguzo hili litategemea mahali alipo mteja”

“Hii ni punguzo litakalosaidia sana wateja wa Airtel kupata unafuu wa kuwasiliana kibiashara, masomo au kwa kuwasiliana na ndugu jamaa au wapendwa wao bila kuwa na wasiwasi juu ya gharama zao za simu” alieleza bw, Nyakundi

Tunaamini huduma hii ya “Airtel Zone” imekuja kwa wakati muafaka wakati mawasiliano ya simu za mkononi ni nyenzo muhimu katika ukuzaji wa shughuli za kiuchumi na za kijamii aliongeza Nyakundi
Akifafanua zaidi kuhusu huduma hii Mkurugenzi wa Mawasilaiano Bi Beatrice Singano Mallya, alisema” punguzo la gharama litategemea mahali mteja alipo na muda anaopiga simu, mteja atapata ujumbe utakaomuonyesha kiwango cha punguzo anachopata kwa mahali alipo, alikadhalika mteja anaweza  kupiga *149*39*0# ili kuangalia kiwango cha gharama ya kupiga simu. Huduma hii ya “Airtel Zone” ni kwa wateja wa malipo ya awali  na punguzo hili litatumika kupiga simu za ndani tu .

Sambamba na hilo mteja atakayekuwa na kifurushi cha muda wa maongezi kama vile Airtel yatosha na vifurushi vingine punguzo litaanza pale tu kifurushi chake cha muda wa maongezi kitakapoisha.

Kuujiunga ni rahisi, bure na mara moja tu, piga 107 ufate maelekezo au piga *149*39#” aliongeza, Singano Mallya

KOCHA WA STARS NOOIJ AITA 28 KUELEKEA COSAFA CUP

$
0
0
Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Mart Nooij leo ametangaza kikosi cha wachezaji 28 watakaoingia kambini katika hoteli ya Tansoma iliyo eneo la Gerezani jijini Dar es salaam, kujiandaa na michuano ya kombe la COSAFA na kuwania kufuzu kwa AFCON na CHAN mwezi Juni mwaka huu.

Akiongea na waandishi wa habari leo makao makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF amesema, wachezaji 28 aliowaita, amewaona kwa macho yake wakicheza, na katika wachezaji aliowaita amechanganya wanaochipukia (damu changa) na wenye uzoefu wa michuano ya kimataifa.

Nooij amesema katika orodha hiyo ya wachezaji 28 watakaoripoti kambini jumatatu mchana, watapimwa afya zao na madakatari wa timu ya Taifa, na kisha watakaokuwa fit atachagua wachezaji 20 watakaokwenda kwenye michuano ya COSAFA nchini Afrika kusini.

Aidha Nooij ameongeza wachezaji 8 watakaobakia nchini wanapaswa kuwa tayari wakati wowote wanaweza jumuishwa katika kikosi kutokana na Taifa Stars kukabiliwa na michuano mbalimbali ambayo pia inahitaji kuwa na wigo mpana wa wachezaji.

Wachezaji walioitwa na kocha Nooij ni magolikipa: Deogratius Munish (Yanga), Aishi Manula, Mwadini Ali (Azam), walinzi: Shomari Kapombe, Aggrey Morris, Erasto Nyoni (Azam), Nadir Haroub, Oscar Joshua, Kelvin Yondani (Yanga), Abdi Banda, Hassan Isihaka (Simba), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar) na Haji Mwinyi (KMKM).

Wengine ni viungo: Amri Kiemba, Salum Abubakar, Frank Domayo (Azam), Said Juma, Salum Telela, Hassan Dilunga (Yanga), Said Ndemla (Simba), Haroun Chanongo (Stand United) na Mwinyi Kazimoto (Al Markhira).


Washambuliaji ni Ibrahim Ajib (Simba), Mrisho Ngasa, Saimon Msuva (Yanga), John Bocco, Kelvin Friday (Azam) na Juma Luizio (Zeco United).

Taifa Stars inatarajiwa kuondoka nchini siku ya jumatano, Mei 13 saa 1 jioni kwa shirika la ndege la Fastjet kuelekea nchini Afrika Kusini katika mji wa Rusterburg - North West Province ambapo ndipo michuano ya COSAFA CUP itafanyika kuanzia Mei 17 mpaka Mei 31 mwaka huu.

Mchezo wa kwanza wa Taifa Stars iliyopo katika kundi B katika michuano ya COSAFA, itacheza dhidi ya Swaziland Mei 18, Mei 20 (Madagascar Vs Tanzania) na Mei 22 ( Tanzania vs Lesotho), mshindi wa kundi B atacheza robo fainali dhidi ya timu ya Taifa kutoka Ghana.

Mara baada ya kumalizika kwa michuano hiyo, Taifa Stars itarejea nchini kujiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu kwa AFCON 2017, dhidi ya Misri utakaopigwa Juni 13 nchini Misri, kisha kurejea nchini kucheza na Uganda Juni 21 kuwania kufuzu kwa fainali za wachezaji wa ndani CHAN.

Mart Nooj amesema ataitumia michuano ya COSAFA kama sehemu ya maandalizi ya michezo ya kuwania kufuzu kwa AFCON na CHAN.


IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

YANGA YAKABIDHIWA RASMI KOMBE

$
0
0
 Wachezaji wa Yanga wakishangilia Kombe la Ubingwa wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara (VPL), baada ya kukabidhiwa rasmi katika mchezo wao na Azam FC uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa.
 Wachezaji wa Yanga wakishangilia.
 Mashabikiwa Yanga wakishangilia baada ya kulioana kombe la VPL.
  Mashabikiwa Yanga wakishangilia baada ya kulioana kombe la VPL.

BODI YA NHC YATEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI YA UJENZI WA NYUMBA JIJINI ARUSHA

$
0
0
Ujumbe wa wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya NHC ukiwa eneo linalomilikiwa na  NHC ambalo ujenzi wa Mji wa kisasa umeanza wakionyeshwa na Meneja wa NHC Mkoa wa Arusha Bw. James Kisarika chemchemu za maji yanayotiririka walipotembelea eneo hilo lenye hali ya hewa ya aina yake Jijini Arusha jana.
Usariver ni Arusha Tanzania ambapo NHC Shirika lenye dhamana ya kujenga nyumba bora hapa nchini limeanza kupanga mji huo wenye mandhari na hali ya hewa ya kuvutia. Hapa wajumbe wa Bodi ya NHC na watendaji wa NHC wanafurahia mpango wa kuendeleza eneo hilo lenye ekari 300 linalomilikiwa na NHC.
Hii ndiyo hatua ya ujenzi iliyokwishafikiwa hivi sasa katika ujenzi wa nyumba za gharama ya kati aina ya “town houses” zinazojengwa na NHC Wilayani Monduli kwa ajili ya watumishi wa Halmashauri hiyo.

MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF IDD AKUTANA NA BALOZI, BATILDA BURIANI, GAVANI MKUU WA JAMHURI YA KIISLAMU YA IRAN

$
0
0
 Balozi Mpya wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Nchini Japan Balozi Batilda Buriani akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipofika kuaga rasmi baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo na Rais wa Jakaya Mrisho Kikwete. Picha na – OMPR – ZNZ.
Balozi Seif akibadilishana mawazo na Gavana Mkuu wa Jimbo la Siustan na Balachestan Nchini Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran Bwana Ali Osat Hashemi  ambae yupo Zanzibar na Ujumbe wake kwa ziara ya siku mbili.

XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX

Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran ina wajibu  wa kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika harakati za maendeleo kutokana na Historia ndefu iliyopo ya muingiliano wa kibiashara baina ya baadhi ya Wananchi wa pande hizo mbili.

Gavana  Mkuu wa Jimbo la Sistan na Balachestan Nchini Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran Bwana  Ali Osat Hashemi akiuongoza Ujumbe wa Viongozi saba wa Jimbo hilo alieleza hayo wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.

Gavana  Ali Osat Hashemi alisema muingiliano huo wa biashara kati ya Irani na Zanzibar na Tanzania kwa ujumla umepelekea watu wa pande hizo mbili pia kuwa karibu zaidi kwa kuchanganya damu.

Alisema wiki chache zijazo pande hizi mbili zinatarajia kusaini Mkataba wa ushirikiano katika kuendeleza mradi wa mafunzo ya amali   ambao utagharimiwa na Iran kwa kiasi cha Dola  za Kimarekani Laki 500,000 zitakazotumika katika ununuzi wa vifaa vya kufundishia.

Gavana huyo wa Jimbo la Sistan na Balachestan Nchini Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran alifahamisha kwamba sekta binafsi hasa miradi ya amali inafaa kuungwa mkono kwa vile inasaidia kutoa ajira kubwa kwa Jamii hasa Vijana.

Alimuhakikishia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba Iran itaendelea kutoa fursa za masomo ya Elimu ya juu kwa Wanafunzi wa Tanzania na Zanzibar katika vyuo vikuu mbali mbali vilivyomo nchini humo.

Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi  alisema miradi ya Amali na Sekta ya Afya inayofadhiliwa na Iran kwa Zanzibar ni uthibitisho wa uimarishaji wa uhusiano uliopo kati ya pande hizo mbili.

Balozi Seif aliiomba Jamuhuri ya Kiislamu ya Irani kuendelea kuongeza fursa za mafunzo kwa Vijana wa Zanzibar ili elimu watayoipata hasa katika miradi ya amali iweze kusaidia kupunguza wimbi kubwa la ukosefu wa ajira hapa Nchini.

 Alieleza kwamba fursa za ajira bado zinaendelea kuwa changamoto kubwa kwa Mataifa mbali mbali Duniani zikiwemo pia zile Nchi  ishirini zilizoendelea kiviwanda  Ulimwenguni  { yaani G 20 }.

Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alikutana kwa mazungumzo na Balozi Mpya wa Malawi Nchini Tanzania  Bibi Hawa O. Ndilole aliyefika kujitambulisha rasmi Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.

Katika mazungumzo yao Balozi huyo Mpya wa Malawi Bibi Hawa Ndilole alisema Historia kubwa ya Utamaduni na Elimu inayofanana kati ya Malawi na Tanzania inafaa kuendelezwa zaidi kwa maslahi ya mataifa hayo mawili jirani.

Bibi Hawa alifahamisha kwamba muingiliano wa mafunzo ya elimu ya juu ambao unatoa fursa kwa wanafunzi wengi wa Malawi kupata elimu ya vyuo vikuu nchini Tanzania ni moja kati ya uthibitisho huo wa  uhusiano mwema.

Naye Balozi Seif alisisitiza umuhimu wa wataalamu wa kilimo wa Malawi na Zanzibar kufanya utafiti wa pamoja kwenye sekta hiyo ili kusaidia kutoa matunda bora yatakayoimarisha ustawi wa Wananchi wa pande hizo mbili.

Balozi Seif alisema Mataifa ya Bara la Afrika yamebarikiwa kuwa na Utajiri mkubwa wa  rasilmali tofauti zinazopaswa kufanyiwa utafiti wa pamoja na wataalamu wazalendo wa Bara hili ili ziendelee kufaidisha Bara hili.

Akizungumza na Balozi Mpya wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Nchini Japani Balozi Batilda Buriani aliyefika Ofisini kwake Vuga kumuaga rasmi baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo Balozi Seif  alimuomba Balozi Batilda kuhakikisha kwamba Tanzania inafaidika kutokana na ushirikiano wake wa Kidiplomasia ya Japan.

Balozi Seif alisema ipo miradi kadhaa ya maendeleo kama huduma za Umeme, Maji pamoja na masuala ya kukabiliana na maafa na majanga inayoendelezwa na Zanzibar ambayo  imekuwa ikipata nguvu na ufadhili katika utekelezaji wake kutoka Japan suala ambalo Balozi Batilda atapaswa kulifuatilia ili kuona utekelezaji wake unafikia ufanisi uliokusudiwa.

Alifahamisha kwamba  kazi kubwa ya Balozi Batilda Buriani ambayo amekabidhiwa na Taifa katika kusimamia Diplomasia ya Tanzania Nchini Japan ni kuchangamkia fursa zote za Maendeleo ambazo zinaweza kuisaidia Tanzania kupitia taasisi na mashirkia yote yatayokuwa ytayri kujitolewa kusaidia nguvu zao.

Balozi Mpya wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Batilda Buriani  amepata uteuzi huo aliokabidhiwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete wadhifa ambao aliwahi kuutumikia kabla Nchini Jamuhuri ya Watu wa Kenya.


Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
7/5/2015.

Chadema yavamia Majimbo na Kata za CCM Morogoro.

$
0
0
Na Bryceson Mathias, Morogoro

WATIA Nia wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wamevamia Majimbo na Kata zinazoshikiliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM), kiasi cha kuwaweka Roho juu wanaokalia Viti hivyo,  wakihofu kwamba, mwaka huu wa Uchaguzi watapoteza nafasi zao.

Akizungumza na Habari Mseto, Katibu wa Chadema Mkoa wa Morogoro, Samwel Kitwika, amesema, Majimbo yote 10 ya Morogoro, yamevamiwa na Watia Nia ya Kugombea Ubunge kwa Tiketi ya Chadema.

Mbali ya Majimbo 10 kuvamiwa, Kitwika  amesema, Kata 212 za Morogoro, nazo ziko kwenye Mtikisiko, ambapo wanaowania Udiwani wa Kata hizo, Wanashambulia kwa Mikutano ya hadhara kwa lengo la kutoa Elimu kwa wananchi, ili wakati ukifika; Waungwe Mkono.

Kitwika alibainisha idadi ya Watia Nia wa Chadema na jinsia yao kwenye mabano kuwa, “Jimbo la Kilombero lina Watahini 11, Me(9), Ke(2), Mikumi Wanne (Me),  Kilosa Kati Watano(Me), Gairo Watatu(Me), Mvomero Wanne(Me), Manispaa ya Morogoro Saba, Me(6), Ke(1),

“Morogoro Kusini Mashariki –Watatu, Me(2), Ke(1), Ulanga Magharibi-Saba, Me(6), Ke(1) na Ulanga Mashariki-Wawili, Me(1), Ke(1), Ulanga Magharibi tuna asilimia 100%, tutashinda.alisema Kitwika.

Mwenyekiti wa Chadema Kata ya Kihonda Maghorofani’A’, Elizeus Rwegasira, baada ya kuibwaga CCM mahakamani Morogoro, sasa ametia Nia ya kuutaka Udiwani wa Kata hiyo, ili apambana na Diwani, anayeshikilia Kata hiyo, Lyidia Mbiaji (CCM,) aliyeapa atashinda.   

Aidha Kati ya Wachungaji wawili wanaowania kupitishwa na Chadema kugombea Ubunge kwa Tiketi ya Chama hicho, James Samson Mabula, alimaarufu Power Mabula, wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God (EAGT), alikiri kuwa yumo kwenye Kinyang’anyiro cha kuwania kukubaliwa kugombea Ubunge wa Manispaa ya Morogoro.

SEMINA YA WANAHISA WA BENKI YA CRDB YAFANYIKA ARUSHA

$
0
0
 Mkurugezi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akifungua semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB katika ukumbi wa AICCjijini Arusha leo. 
 Mwrnyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya CRDB, Martin Mmari akizungumza wakati wa semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB.
 Mwanahisa akiuliza swali.
Wajumbe wa bodi.
Katibu wa Benki, John Rugambwa akizungumza wakati wa semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB.

Wanahisa.
Baadhi ya maofisa wa Benki ya CRDB wakiwa katika semina hiyo.
Wanahisa.
Wanahisa wakifuatilia semina hiyo.
Meneja Mwandamizi Huduma za Uwakala, Jessica Nyachiro akitoa mada kuhusu Fursa kupitia Uwakala wa Benki ya CRDB, wakati wa semina ya Wanahisa wa benkihiyo iliyofanyika katika ukumbi wa AICC jijini Arusha.
Mkurugenzi wa Masoko Huduma kwa Wateja, Tully Mwambapa (kushoto) akifuatilia semina hiyo.
Prof. Mohamed Warsame kutoka Kmpuni ya Dhow Financials akitoa mada kuhusu Ukuzaji wa Mitaji kwa Kampuni iliyoorodheshwa Soko la Hisa.
Washiriki wa semina hiyo.

RAIS TFF AAGIZA USIMAMIZI MECHI ZA MWISHO VPL

$
0
0
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amewaagiza wasimamizi wa vituo vya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuhakikisha sheria na taratibu zote za mechi zinafuatwa.

Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu huu 2014/2015 inafikia tamati kesho (Mei 9, 2015) ambapo timu zote 14 zitakuwa viwanjani katika mechi ambazo ndizo zitakazotoa hatma ya timu zinazoshuka daraja.

Mechi hizo zitakuwa kati ya Ndanda na Yanga (Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara), JKT Ruvu na Simba (Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam), Azam na Mgambo Shooting (Azam Complex, Dar es Salaam), Stand United na Ruvu Shooting (Uwanja wa Kambarage, Shinyanga), Kagera Sugar na Tanzania Prisons (Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza), Mbeya City na Polisi Morogoro (Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, Mbeya), na Mtibwa Sugar na Coastal Union (Uwanja wa Manungu, Morogoro).

JERRY MURO APIGWA FAINI MILIONI 5
Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF iliyoketi jumanne tarehe 5 Mei, 2015 imempiga faini ya sh. 5,000,00 (milioni tano), Afisa Habari wa klabu ya Yanga SC Jerry Muro kwa kutoa kauli za chuki, kisirani na uchochezi dhidi ya uongozi wa Bodi ya Ligi (TPLB) nchini na TFF.

Akitoa utetezi wake mbele ya Kamati ya Nidhamu, Jerry Muro alikiri na kujutia kufanya kosa hilo na kudai ilitokana na ugeni wake katika uongozi wa michezo, kwa kuzingatia hilo kamati ilimuepusha na adhabu ya kufungiwa..

Kwa mujibu wa Ibara ya 53 (2)ya Kanuni za Nidhamu za TFF toleo la 2012, kwa kuidhalilisha TFF na Bodi yake ya Ligi mbele ya umma, kamati imemtoza faini ya sh. 5,000,000 (millioni tano), Jerry Muro na kuwaonya viongozi wengine wa familia ya mpira wa miguu kutojihusisha na vitendo vya matamshi ya aina hiyo.

Shitaka linalomhusisha mchezaji wa Yanga, Amissi Tambwe kumshika kwa kumdhalilisha mchezaji wa Simba SC Juuko Mursheed, na kiongozi wa Friend Rangers Hery Chibakasa wa Friends Rangers kuhamasisha vurugu katika mchezo wa timu yake na dhidi ya Majimaji ya Songea Januari 29, 2015, kamati imeahirisha mashitaka hayo mpaka tarehe nyingine itakapopangwa.

Kamati iliahirisha malalamiko dhidi ya Mohamed Hussein, Muhibu Kanu, Manfred Luambano, Venance Joseph, Mussa Senyange, Saleh Ali, Shafii Maganga na Ismail Salim baada ya kupokea taarifa za udhuru zilizosbabishwa na mgomo wa madereva wa mabasi ya abiria ya mikoani.

KUMRADHI WANAHABARI
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF, Mwesigwa Selestine ameomba radhi kwa vyombo kufuatia madai ya waandishi wa habari kupata usumbufu wakati wa utoaji wa Zawadi kwa Mabingwa na washindi wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom.

Mwesigwa alisema kwa niaba ya TFF anaomba radhi kwa usumbufu wowote uliowapata waandishi na wadau wote walioshindwa kushuhudia vema tukio hilo.

“TFF na FIFA vinatambua umuhimu na nafasi ya wanahabri na vyombo vya habari si tu katika kuutangaza mchezo, bali pia katika kutia chachu maendeleo ya mchezo wenyewe “ alisema Mwesigwa.

Hali mbaya ya hewa ilivuruga utaratibu uliokuwa umepangwa awali kuanzia itifaki ya shughuli za kabla na wakati wa mchezo na zile za utoaji tuzo.

Aidha Mwesigwa alisema TFF itaendelea kushirikiana vema na jumuiya ya wanahabari ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kwamba wana mazingira mazuri wanapofanya kazi kwenye matukio ya mpira wa miguu.


IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF

TBL YATOA MSAADA WA VIFAA TIBA VYA SH. MIL. 22 KITUO CHA AFYA KAMBI YA SIMBA,KARATU

$
0
0
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Bia Tanzania, (TBL), Robert Jarrin akipokea zawadi ya fimbo kutoka kwa mmoja wa viongozi wa kijiji wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya Kituo cha Afya cha Kijiji cha Kambi ya Simba kilichopo Kata ya Mbulumbulu wilayani Karatu ivi karibu, ambapo Kiwanda hicho kilikabdhi vifaa vyenye thamani ya Sh. Milioni 22.
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Bia Tanzania, (TBL), Robert Jarrin akikabidhi baadhi ya vifaa vya Kituo cha Afya cha Kijiji cha Kambi ya Simba wilayani Karatu mkoani Arusha kwa baadhi ya viongozi wa Serikali ya Kijiji hicho, ambapo Kampuni hiyo ya Bia ilitoa vifaa vyenye thamani ya Sh.Milioni 22.

 Mkurugenzi wa Kampuni ya Bia Tanzania, (TBL), Robert Jarrin Robert Jarrin akipokea zawadi ya fimbo kutoka kwa mmoja wa viongozi wa kijiji wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya Kituo cha Afya cha Kijiji cha Kambi ya Simba kilichopo Kata ya Mbulumbulu wilayani Karatu ivi karibu, ambapo Kiwanda hicho kilikabdhi vifaa vyenye thamani ya Sh. Milioni 22.



 Afisa Uhusiano wa TBL Dorris Malulu akizungumza na baadhi ya viongozi Serikali ya Kijiji pamoja na uongozi wa Kituo cha Afya cha Kijiji cha Kambi ya Simba kilichopo Kata ya Mbulumbulu wilayani Karatu mkoani Arusha wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa mbalimbali vya kituo hicho vyenye thamani ya Sh. Milioni 22, Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Bia Tanzania, (TBL), Robert Jarrin na kushoto kwake ni Meneja Mradi Kilimo cha Shayir Dk. Basson Bennie.

 Mwananchi wa Kijiji cha Kambi ya Simba kilichopo Kata ya Mbulumbulu wilayani Karatu ambacho ni maarufu kwa ulimaji wa zao la Shayiri akimkabidhi Mkurugenzi wa Kampuni ya Bia Tanzania, (TBL), Robert Jarrin mara baada ya kukabidhi Kituo  cha Afya cha Kijiji hicho vifaa mbalimbali vya matibabu.
 Maofisa wa TBL wakibadilishana mawazo wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa kwa Kituo cha Afya cha Kijiji cha Kambi ya Simba kilichopo wilayani Karatu, katikati ni Afisa Uhusiano Dorris Malulu, kushoto kwake ni Mkurugenzi Jarrin na kulia kwake ni Meneja mradi wa Kilimo cha Shayiri Dk. Basson

 Mkurugenzi wa Kiwanda cha TBL Robert Jarrin akiwa anangalia baadhi ya vifaa na Mganga wa Hospitali ya wi;aya ya Karatu Dk. Lucas wakati wa makabidhiano ya vifaa vya Kituo cha Afya cha Kijiji cha Kambi ya Simba Kata ya Mbulumbulu.
 Mwenyekiti wa Kijiji cha Kambi ya Simba Damian Anatholi akisalimiana na Mkurugenzi wa Kampuni ya Bia Tanzania, (TBL), Robert Jarrin wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa mbalimbali vya Kituo cha Afya cha Kijiji hicho ambacho ni maarufu sana kwa kilimo cha Shayiri.

 Mwenyekiti wa Kijiji cha Kambi ya Simba Damian Anatholi akisalimiana na Mkurugenzi wa Kampuni ya Bia Tanzania, (TBL), Robert Jarrinwakati wa hafla ya kukabidhi vifaa mbalimbali vya Kituo cha Afya cha Kijiji hicho ambacho ni maarufu sana kwa kilimo cha Shayiri.

 Mganga wa Mfawidhi wa wilaya ya Karatu Dk. Lucas akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya vifaa vya hospitali kwa ajili ya kituo cha Afya cha Kijiji cha Kambi ya Simba kilichopo Kata ya Mbulumbulu wilayani Karatu mkoani Arusha.

 Mkurugenzi wa TBL Robert Jarrin akiwa pamoja na Meneja Mradi wa Kilimo cha Shayiri Dk. Basson wakitembelea jengo la Kituo cha Afya cha Kijiji cha Simba kilichopo Kata ya mBULUMBULU wilayani Karatu wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya hospitali kwenye kituo hicho.
Mganga wa wilaya ya Karatu Dk. Lucas akibadilishana na mawazo pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya Bia Tanzania, (TBL), Robert Jarrin wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya hospitali kwa Kituo cha Afya cha Kijiji cha Simba kilichopo Kata ya Mbulumbulu wilayani Karatu mkoani Arusha.

MAGARI AINA YA NISSAN MURANO NA TOYOTA LAV4 YANAUZWA

$
0
0
Gari zinauzwa kwa bei nzuri tu na zipo Dar kwa atakayeipenda tuwasiliane kupitia namba hizi 0713327106/0756673327

Fedha za Bayport zazidi kupata wenyewe

$
0
0
Meneja Masoko na Mawasiliano wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mikopo, Ngula Cheyo, katikati akizungumza jambo wakati wa droo ya pili ya Kopa Bayport kwa njia ya mtandao.


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

SHINDANO la Kopa Bayport kwa njia ya mtandao linaloendeshwa na taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, limezidi kuchanja mbuga, baada ya wateja watatu wa mwezi Mei kuibuka na Sh Milioni moja kwa kila mmoja, huku mikoa ya Bukoba, Njombe na Dar es Salaam ikichanua katika droo iliyochezeshwa jijini Dar es Salaam.

Wateja hao walioshinda katika shindano hilo ni Tryphone Mashamba mkoani (Njombe), Kisa Mboya (Dar es Salaam) na Oscar Gadawu (Bukoba) ambao wote kwa pamoja wameibuka na Sh Milioni moja baada ya kukopa kwa njia ya mtandao wa www.kopabayport.co.tz, ikiwa ni huduma nzuri kutoka kwenye taasisi hiyo ya Bayport Financial Services.

Akizungumza katika droo hiyo iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam, Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo, alisema shindano lao limepokewa vizuri na wateja wao, waliopata urahisi wa upatikanaji wa huduma za mikopo kutoka kwenye taasisi hiyo.


Alisema awali wateja walilazimika kusafiri kuelekea kwenye tawi lao, lakini kuanzishwa kwa tovuti hiyo, kumetoa urahisi wa ukopaji kwa kiasi kikubwa mno, huku kila mmoja akiwa na uwezo wa kushinda endapo ataamua kutumia huduma hiyo.

“Tunashukuru kuona Watanzania wenzetu wameendelea kupata urahisi wa huduma zetu za mikopo, maana anaweza kukopa mahala popote alipokuwapo, endapo ana kifaa kitachomuwezesha kuingia katika mtandao wetu wa www.kopabayport.co.tz, kama vile simu ya mkononi na kompyuta” alisema Cheyo.

Meneja Masoko na Mawasiliano wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mikopo, Ngula Cheyo, katikati akizungumza jambo wakati wa droo ya pili ya Kopa Bayport kwa njia ya mtandao wa www.kopabayport.co.tz, ambapo jumla ya washindi watatu kila mwezi wanapatikana na kila mmoja kujishindia jumla ya Sh Milioni moja. Kulia ni Afisa wa Huduma kwa Wateja wa taasisi hiyo, Gladys John, huku kushoto akiwa ni bwana Humud Abdulhussein, Msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha Tanzania.



Naye Msimamizi wa Michezo ya Kubahatisha kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Humud Abdulhussein, alisema promosheni hiyo ya kopabayport ni nzuri kwa wateja na Watanzania wote wanaoweza kujikwamua kwa kupata mikopo isiyokuwa na dhamana wala amana kutoka Bayport.
“Sisi Bodi tunachoangalia ni kanuni na vigezo vya michezo ya kubahatisha kufuatwa, ikiwa ni upatikanaji wa washindi na namna walivyoweza kujiunga kwenye huduma hii ambayo kila mtu anaweza kuingia anapohitaji huduma yoyote,” alisema Abdulhussein.

Naye Meneja Huduma kwa Watejanwa Bayport Financial Services, Gladys John, aliwataka Watanzania kuendelea kuiunga mkono Bayport kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi kutokana na fursa mbalimbali za mikopo isiyokuwa na amana wala dhamana, bila kusahau Kopa Bayport inayoendelea kutolewa kwa ajili ya kuwapongeza wanaomua kutumia huduma hiyo nzuri.

Wateja hao watatu waliojinyakulia sh Milioni moja kila mmoja, wanaungana na Hyasint Mbunda Songea, Phaustine Mbilinyi Dar es Salaam na Allen Bishubo Bukoba ambao walishinda katika droo ya mwezi wa nne, ambapo Bayport Financial Services, imeshawapatia fedha zao za ushindi.

JK; Umechimba Kaburi la Vyombo vya Habari?

$
0
0
 Na Bryceson Mathias

WAKATI Serikali ikionesha kama inatengeneza Mazingira ya Ukiritimba wa kuvichimbia Kaburi Vyombo vya habari kwa kupitisha Sheria ya Takwimu na Makosa ya uharifu wa Kimtandao;  

Wananchi wa Kada mbalimbali nchini, na Wadau wa Habari, wanahoji, Rais Jakaya Kikwete, kusaini Miswada hiyo, anavichimbia Kaburi Vyombo vya Habari na Waandishi?.

Wana Zuoni na Waswahili wa Medani za Semi, husikika wakisema, Kwa kawaida, Ng’ombe, anaweza kutikisa Mkia wake; Lakini kwa dhati, ni agharabu, Mkia hauwezi kumtikisa Ng’ombe.

Sheria hizo ambazo zimelalamikiwa na Wadau, kwamba ni Umangimeza wa Kisiasa wa Watawala,  kuvinyanyasa na kuviziba mdomo vyombo vya habari na Waandishi; Wamesema, kama ilivyokuwa kwa Mordekai; Wanatafsiri Sheria hiyo itawafunga Mawaziri na Serikali yenyewe.

Katika nyakati za Utawala wa Mfalme Ahasuero kwenye Biblia Sura ya 7:6-10, Mordekai alikwenda kwa Mfalme kinyume cha utaratibu, ili kuwanusuru wananchi waliouzwa ili Waharibiwe, Wauawe, Waangamizwe na kuwa Watumwa na Wajakazi.

Mbinu hizo zilipangwa na Akida Mkuu wa Mfalme Ahasuero, Hamani, ambaye alitaka, Mordekai anayewatetea Wananchi Wasiharibiwe, Wasiuawe, Wasiangamizwe na kuwa Watumwa na Wajakazi; Atundikwe kwenye Mti, ukombozi wao usifanikiwe, na watu waendelee kuteseka!. Je iwe hivyo na kwa Watanzania?.

Hamani alimwambia mfalme Ahasuero, “Kuna taifa moja waliotawanyika na kukaa mahali mahali katikati ya mataifa walioko katika majimbo yote ya ufalme wako; Nao sheria zao zimefarakana na sheria za kila taifa; wala hawazishiki amri za mfalme; kwa hiyo haimpasi mfalme kuchukuliana nao.

Basi, mfalme akiona vema, na iandikwe kwamba waangamizwe; nami nitalipa talanta kumi elfu za fedha mikononi mwao watakaosimamia shughuli hiyo, waziweke katika hazina ya mfalme. Ndipo mfalme alipoivua pete yake mkononi, akampa Hamani bin Hamedatha, Mwagagi, adui ya Wayahudi”.Esta 3:8-9.

Basi, Waandishi wa mfalme wakaitwa, siku ya 13 ya mwezi; na barua zikaandikwa, kama vile Hamani alivyoagiza vyote, kwa maakida wa mfalme, na maliwali waliokuwa juu ya kila jimbo, na wakuu wa kila taifa; kila jimbo kwa mwandiko wake, na kila taifa kwa lugha yake; zikaandikwa kwa jinsi la mfalme Ahasuero, na kutiwa muhuri kwa pete yake. 

Barua zikapelekwa kwa mikono ya matarishi mpaka majimbo yote ya mfalme kuwaangamiza Wayahudi wote, na kuwaua, na kuwafisha, vijana kwa wazee, watoto wachanga na wanawake pia, siku moja, yaani, siku ya 13 ya mwezi wa 12 ndio mwezi wa Adari; na kuyachukua mali yao kuwa nyara

Nakili ya andiko, ya kupigwa mbiu katika kila jimbo, ilitangazwa kwa mataifa yote wawe tayari siku ile ile. Matarishi wakaondoka wakaenda haraka kwa amri ya mfalme; kukapigwa mbiu huko Shushani ngomeni. 

Mfalme na Hamani wakaketi ili kunywa divai na kujifurahisha (kama vile Waziri wa MawasilianoSayansi na Teknolojia Prof Makame Mbarawa akifurahi kusainiwa kwa Miswada hiyo); bali mji wa Shushani ukafadhaika. 

Wadau wa Habari wanadai, yawezekana hivyo ndivyo Bunge lilivyopelekewa Miswada ya Sheria ya Takwimu na Makosa ya uharifu wa Kimtandao kwa kutumia Hati ya Dharula, isainiwe na Rais, ili kuwakomoa Waandishi na Vyombo vya habari, ikilengwa Uchaguzi Oktoba 2015, ili kuwatisha Waandishi, Wananchi wasipate nafasi ya kutoa na kupokea habari.

Kama ulivyotokea uovu wa Hamani kwa Wayahudi, Mordeikai alipojua mambo yote yaliyofanyika, alizirarua nguo zake, akajivika gunia pamoja na majivu, akatoka hata kufika katikati ya mji, akalia kwa sauti kuu ya uchungu.

Mordekai pia alifika hata mbele ya mlango wa mfalme; maana hakuna awezaye kuingia ndani ya mlango wa mfalme hali amevaa magunia. Na katika kila jimbo, ambako amri ya mfalme na mbiu yake iliwasili, palikuwako msiba mkuu kwa Wayahudi, na kufunga, na kulia, na kuomboleza; hata na wengi wakalala juu ya gunia na majivu, kama ilivyo kwa Wandishi, Wananchi na Wadau wake.

Basi tunaamni, Wananchi wasio na Sauti (Voiceless), ambao vyombo vya habari ni Mhimili wao wa Nne wa kutetea Kodi na Rasilimali zao, ambao wamewaibulia Maovu na Machafu Mengi, (Richmond, Dowans, EPA,  wa Wanyama Pori, na hivi karibuni Escrow), watapiga Kelele.

Wanahabari tunaamini, Kelele zinasikilizwa, na tuna mifano ya kelele kusikilizwa, ‘Migomo ya Wafanya Biashara, Migomo ya Madereva, Wanavyuo, Walimu, Madaktari na Wauguzi, Wakulima, Wananchi wanaodai Ardhi, Matokeo ya Uchaguzi ya kughushi, yameiipa Serikali wakati Mgumu.

Mordekai aliagiza wampelekee Esta jibu la kusema, “Wewe usijidhanie kuwa utaokoka nyumbani mwa mfalme, zaidi ya Wayahudi wote. Kwa maana wewe ukinyamaza kabisa wakati huu, ndipo kutakapowatokea Wayahudi msaada na wokovu kwa njia nyingine; hivyo wanadishi na wadau, msidhani mtaokoka.

“Ila wewe utaangamia pamoja na mlango wote wa baba yako; walakini ni nani ajuaye kama wewe hukuujia ufalme kwa ajili ya wakati kama huo?tusaidiane kupiga kelele ya kupinga uovu huu!.

Esta aliingia kwa Mfalme bila Utaratibu, akakubalika, na akahakikisha badala ya Mordekai kutundikwa kwenye Mti aliouandaa Hamani, akatundikwa yeye. Waandishi tushikamane kukataa unyannyaswaji huu wa kutuziba mdomo!

katika Esta 7:8-10 inasema,  Kisha mfalme akarudi kutoka katika bustani ya ngome hata mahali pa karamu ya divai. Ikawa Hamani amejitupa chini penye kitanda alipokuwapo Esta. Mfalme akasema,
‘Namna gani! Je! Atamfanyia malkia jeuri hata machoni pangu nyumbani mwangu? Na neno lilipotoka kinywani mwa mfalme, wakamfunika uso Hamani’. 

Ndipo aliposema Harbona, msimamizi-wa-nyumba mmojawapo wa wale waliohudhuria mbele ya mfalme, Tazama, basi, mti wa mikono hamsini urefu wake, Hamani aliomwekea tayari Mordekai, ambaye alinena vema kwa ajili ya mfalme, upo umesimamishwa nyumbani kwa Hamani. Mfalme akasema, 

Mtundikeni juu yake. Basi wakamtundika Hamani juu ya mti aliomwekea tayari Mordekai. Ghadhabu ya mfalme ikatulia; Hivyo pamoja na kwamba Sheria hizo zimelenga kuwakomoa Waandishi na Vyombo vya habari; Sheria ya Takwimu  kisiasa, zitawafunga Mawaziri.

Kwa nini nasema na kurudia hayo; kwa sababu watatoa bungeni taarifa za wizara zisizo sahihi, na itakapofuatiliwa, wataonekana wamesema Uongo.

MAAMUZI YA KAMATI YA RUFAA YA NIDHAMU

$
0
0
Baada ya mahojiano kati ya mrufani Dk. Damas Ndumbaro na Wakili wa TFF     Nd Emmanuel Muga, pamoja na Wajumbe wa Kamati ya rufaa ya nidhamu kuwahoji wote, Mrufani na Wakili wa TFF, Kamati ya rufaa ya nidhamu ilichukua uamuzi ufuatao:- 

  1. Hoja ya kwanza cha rufaa, kwamba kamati ya nidhamu haikuwa na nguvu za kisheria kusikiliza shauri lake, Kamati ya rufaa ya nidhamu baada kusikiliza hoja za pande zote mbili, kwa uamuzi wa Wajumbe wote kwa maana ya kuwa zote nne za Wajjumbe wa kamati ya rufaa ya nidhamu, ilitupilia mbali hoja hiyo na kuona kwamba kamati ilikuwa na mamlaka ya kusikiliza shauri hilo kwa kuwa mkata rufaa ni afisa wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF kwa mujibu wa Katiba ya TFF ya 2013. Uamuzi katika hoja hii uliamuliwa kwa kura 3 dhidi ya moja.
  2. Hoja ya pili inayosema kwamba kamati ilikosea kisheria kwa kutompa muda wa kuleta utetezi wake wala vielelezo vyovyote vile kwenye shauri lake.
Kamati ya rufaa ya Nidhamu kwenye Shauri hili, baada ya kufanya maamuzi kwa kupiga kura, kura za Wajumbe watatu zilitupiliwa mbali hoja yake na kura moja kati ya kura nne ilikubaliana na hoja yake kwa uamuzi huo, kamati ya rufani ya nidhamu ilitupilia mbali hoja hiyo kwa uamuzi wa wingi wa kura kwa maana ya kuwa tatu dhidi ya kura moja.

Sababu za kutupilia mbali hoja hizo ni kwamba mrufani alipata wito wa kwenda kwenye shauri, na akawakilishwa na wakili wake ( Nestory Peter Wandiba ) kwenye Shauri hilo. Shauri liliposikilizwa kwa mara ya kwanza tarehe 10/10.2014 shauri lilipangwa kusikilizwa tarehe 11/10/2014 Lakini siku hiyo ya pili si wakili wala Dr Ndumbaro alifika kwenye shauri hilo kwa maana hiyo basi shauri lililazimika kusilikizwa upande mmoja kwa mujibu wa kanuni za nidhamu za TFF ibara ya 94 (3).

3. Hoja ya tatu linalosema kwamba kamati ilikosea kusiliza shauri upande mmoja bila ya mtuhumiwa kuwepo, ni kukiuka haki yake ya msingi ya  kusikilizwa.

Kamati baada ya kusikiliza utetezi kutoka pande zote mbili kamati ilifanya uamuzi kwa kupiga kura, na kura tatu (wajumbe watatu) walitupilia mbali hoja hiyo, dhidi ya kura moja (mjumbe mmoja) aliyeikubali hoja hiyo. Sababu za kutupilia mbali hoja hiyo ni kutokana na ukweli kwamba mrufani alipata wito wa kuhudhuria shauri hili na akamtuma wakili wake, lakini mrufani alishindwa kuonyesha vielelezo vya kuonyesha kwamba angesafiri kwenda nje ya nchi ili kamati ya nidhamu iweze kuahirisha shauri mpaka wakati ambao angekuwa amerejea lakini hakufanya hivyo.

Hata hivyo kwa mujibu wa Ibara 144(2) (3) za kanuni ya nidhamu za TFF, mrufani  angeweza pia kuomba kamati ya nidhamu ibatilishe uamuzi iliyoutoa dhidi yake ili aweze kusikilizwa utetezi wake pia hakufanya hivyo na aliamua kukata rufaa.

4. Hoja ya nne inayosema kwamba kamati ilikosea kisheria katika uchambuzi wa ushahidi wa mlalamikaji na hatimaye kutoa uamuzi uliomtia hatiani.

Kamati ya rufani ya nidhamu ilisikiliza kwa umakini hoja za pande zote mbili na kujiridhisha kwamba mrufani alifanya makosa kwa kutoa taarifa isiyosahihi na kupotosha maamuzi ya TFF kinyume na kanuni ya 41 (6) ya kanuni za ligi kuu ya Tanzania toleo la 2014 (4) na pia kushawishi, kupotosha au kuzuia maamuzi/utekelezaji wa maamuzi ya TFF kinyume na kanuni ya 41(16) ya kanuni za ligi kuu za Tanzania ya (2014).

Wakati wa kufanya maamuzi, wajumbe watatu(3) kwa maana ya kura tatu zilitupilia mbali hoja hiyo, na kura moja, kwa maana ya mjumbe mmoja alikubaliana na hoja hiyo. Kwa maana hiyo, kamati ya rufaa ya nidhamu ya TFF imetupilia mbali hoja hiyo.

Kwa uamuzi huu kamati inadhibitisha uamuzi wa kamati ya nidhamu iliyosomwa tarehe 13/10/2014, uamuzi huu umefikiwa baada ya wajumbe kupiga kura na uamuzi kupitishwa kwa wingi wa kura za wajumbe watatu, dhidi ya mjumbe mmoja wa kamati hii kwa hoja ya 2,3 na 4 na wajumbe wote 4 walikubaliana kutupiliwa mbali hoja ya kwanza.

Kwa hiyo Dr Damas Ndumbaro ataendelea kutumikia adhabu yake kwa kutojihusisha na shughuli yoyote ya Mpira wa Miguu (Soka) kwa kipindi cha miaka saba.

Hata hivyo mrufani Dr Damas Ndumbaro anayohaki ndani ya siku 10 kuanzia leo tarehe 10/05/2015 ya kuomba marejeo ya uamuzi huu mbele ya kamati ya Rufaa ya Nidhamu ya TFF chini ya Ibara 142 ya kanuni za nidhamu za TFF ya mwaka.

Kila upande utabeba gharama zake Hukumu inasomwa leo tarehe 10/05/2015/


Revocatus L. K. Kuuli.
MAKAMU MWENYEKITI.


IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Uzinduzi wa Huduma Mpya ya MaxMalipo kwa kutumia Simu ya Kiganjani

$
0
0
Mkuu wa Kitengo cha Biashara Maxcom Africa Bw. Deogratius Lazari (Katikati) Akifafanua Jambo kwa waandishi wa habari ambao hawapo katika picha wakati wa Uzinduzi wa Mfumo Mpya wa kutoa huduma za Maxmalipo kwa kutumia simu ya kiganjani, wengine katika picha ni  Maasifisa wa Kampuni Kulia msimamizi mauzo na Usambazaji kanda ya mashariki Bwan Bw. Thomas Mwakalembile na Geofrey Mwakamyanda.

Maxcom Africa maarufu kama MaxMalipo ni kampuni ya kitanzania iliyoanzishwa mwaka 2010 ambayo imewekeza katika kurahisisha maisha ya Watanzania na Waafrika kwa ujumla kiuchumi na kijamii kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya mawasiliano (ICT Technology).

Ili kufikia malengo na Sera ya Taifa ya kutumia mifumo ya kielekroniki kutoa huduma na pia kuwezesha Watanzania walio wengi kufikiwa na huduma hizi (Financial Inclusion)  na pia  kurahisisha ukusanyaji wa kodi na kuongeza ajira, MaxMalipo imeanzisha huduma  mpya itakayomuwezesha mtanzania kulipa bili zote kwa kutumia simu ya kiganjani  aina ya  Smart phone yenye Mfumo utakaojulikana kama SmartMalipo.

Huduma hii inatarajiwa kutoa ajira kwa watanzania takribani laki mbili (200,000)  nchi nzima kufikia mwaka 2016  na hivyo kuchangia ukuaji wa sekta isiyo rasmi ya ajira na kunyanyua uchumi wa Nchi.  Mfumo huu utaweza kurahisisha ulipaji wa bili mbalimbali Mfano; Umeme (Luku), Ving’amuzi vya Televisheni, Vocha za Mitandao yote, Kulipia Kodi za TRA na Baadae Kufanya Miamala ya Kibenki  inayohusisha Kuweka na Kutoa fedha, huduma ambazo kwa sasa zinalipwa kupitia mashine za MaxMalipo.

Huduma hiyo inapatikana kwenye mfumo wa simu ya kiganjani ambapo mtumiaji atalazimika kuweka  mfumo wa SmartMalipo (Download Smart Wakala Application) kutoka tovuti ya Google play au tovuti ya Maxmalipo kwa  kuandika neno ‘SmartMalipo  au Maxmalipo’. Kisha mtumiaji atapata maelekezo ya  jinsi ya ku-install mfumo huu kwenye simu yake na jinsi ya kutumia. Mfumo huu utamwezesha mtumiaji yeyote kuwa Wakala na kulipia huduma zilizo orodheshwa. Mtumiaji  wa  mfumo huu  atajipatia kamisheni kama alivyo wakala mwingine wa Maxmalipo kwa Huduma atakazofanya. 

Watumiaji wa mfumo huu wa SmartMalipo watatambulika kwa jina la ‘Smart Wakala’ popote walipo na kufanya biashara kupitia simu zao za kiganjani. MaxMalipo imeanzisha huduma hii mpya kwa lengo la kuwawezesha watanzania walio wengi kufikiwa zaidi na  huduma za malipo kwa haraka wakiwemo wafanyabiashara wadogo na wenye mitaji midogo  ambao kwa mazingira yao ni vigumu kuwa na Mashine za Maxmalipo. 

 MaxMalipo imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza matatizo ya foleni kwenye malipo ya huduma mbalimbali kama bili za TRA, LUKU, DAWASCO, huduma za kibenki na hata katika mifuko ya Hifadhi ya jamii Mfano PSPF.

Mwisho kampuni ya Maxcom Africa - Maxmalipo inatoa rai kwa watanzania hasa wafanyabiashara  kuchangamkia huduma zinazotolewa na kampuni hii ili kuendana na kasi ya maendeleo ya teknolojia katika mifumo ya utoaji huduma.

WAKUU WA TAASISI ZA KUZUIA RUSHWA BARANI AFRICA WAKUTANA ARUSHA KUANGALIA JINSI WATAWEZA KUPAMBANA NA KUFIKIA MALENGO YA KUTOKOMEZA RUSHWA NDANI YA BARA LA AFRICA

$
0
0

SAM_2509Mwenyekiti wa bodi ya ushauri ya kupambana na maswala ya rushwa katika umoja wa Africa kutoka Ghana Mh.Daniel Batidam akizungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari jijini Arusha  katika ukumbi wa mikutano AICC katika kuangalia jinsi gani wataweza kupambana na kufikia malengo ya kutokomeza Rushwa ndani ya Bara La Africa. (Habari Picha na Pamela Mollel wa Jamiiblog)
SAM_2498Makamu Mwenyekiti bodi ya ushauri ya kupambana na maswala ya rushwa katika umoja wa Africa Mh.Florince Ziyambi kutoka Zimbabwe
SAM_2494Muongoza vikao kutoka Kenya Mh.John Tuta akitambulisha wajumbe
SAM_2497
SAM_2499SAM_2503
SAM_2514Mwaandishi wa habari Merry Mwita akiuliza maswali katika mkutano huo
SAM_2504Muonekano ndani ya ukumbi
SAM_2506
SAM_2522
Picha ya Pamoja

Na Mwandishi Wetu, Arusha

Wakuu wa taasisi za kuzuia Ruswa barani Africa wamekutana  katika ukumbi wa mikutano AICC katika kuangalia jinsi gani wataweza kupambana na kufikia malengo ya kutokomeza Rushwa ndani ya Bara La Africa.

Wakuu hao ambao ni wajumbe wa Bodi ya Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa barani Afrika AUABC iliyopo chini ya jumuia ya muungano wa nchi za Afrika ambapo mwenyekiti wa Taasisi ya AUABC Jaji Daniel Batidam amesema kuwa wanatarajia kwa mkutano huu utasaidi kupunguza makali ya Ruswa ndani ya bara hili.

Amesema kuwa kiwango kikubwa wanaangalia jinsi gani wataweza kuondoa ruswa katika taasisi za jamii kwa maana ndio zinazochangia kwa kiasi kikubwa maenbdeleo ya nchi zetu za kiafrika.

Pamoja na hayo amesema kuwa tatizo kubwa la Rushwa ndani ya bara la Afrika ni mfumo uliopo ambao unakuwa unaweka mianya ya rushwa pamoja na hayo alisisistiza kwa wananchi kuacha kutoa rushwa ili kuiondoa kabisa.
Bodi hiyo imeundwa na watu 11 kutoka nchi mbalimbali barani Africa

BENKI YA CRDB YAPATA FAIDA YA BILIONI 95.6

$
0
0
Na Pamela Mollel, Arusha

Benki ya CRDB imepata faidi yazaidi ya shilingi bilioni 95.6 sawa na asilimia 14 kwa mwaka 2014 ambapo ongezeko hilo ni kubwa ukilinganisha na faida ya miaka ya nyuma ambapo hali hiyo imesababishwa na uboreshwaji wa mfumo wa utaoaji pesa kwa wateja wao.

Hayo yameelezwa na mkurugenzi mkuu wa Benki hiyo Dk.Charles Kimei wakati akiwasilisha taarifa ya bodi ya wakurugenzi katika mkutano wa 20 wa wanahisa wa benki hiyo jijiji Arusha.

Dk. Kimei alisema kuwa kufwatia faida hiyo benki hiyo itatoa gawiola shilingi 15 kwa kila hisa moja ya mwanahisa kwa mwaka huu ikiwa na lengo la kuwanufaisha wanahisahao nakuongezea faida ya hisa zao.

Hata hivyo  Benki hiyo iko katika mchakato wa kuweza kuongeza mtaji wa banki hiyo ili kuweza udhibiti wizi wa pesa kwenye mtandao na kuboresha mifumo ya utoaji na kuweka pesa katika banki hiyo na kuweza kuwahhakikishia usalama wa pesa zao .

Dk. Kimei aliongeza kuwa katika uboreshaji wa huduma ya benki hiyo wameweza kuongeza  mawakala 575 wa fahari huduma  na mashine za Atm 375 nchi nzima ili kuweza kuwarahishishia wateja wao kupata huduma za kibenki pindi wanapohitaji.

Kwa upande wake mmoja wa wanahisa Bw,Rashidi Materuka alisema kuwa nimmoja wa mnufaikaji wa hisa ambae anakopa fedha kuputia banki hiyo shughuli za  kilimo na zimeweza kumkwamua katika kupambana na adui umaskini katika kilimo.
Aliongeza kuwa kutokana na kunufaika na huduma za banki hiyo anatkuwa chachu ya mabadiliko kwa wakulima wenzake katika eneo analotoka.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza katika mkutano wa 20 wa wanahisa wa benki hiyo uliofanyika Arusha,Tanzania.
Katibu wa Benki ya CRDB, John Rugambo akiwa katika mkutano huo.
 Mwenyekitiwa Bodi Martin Mmari akizungumza wakati wa mkutano huo.
Naibu Mkurugezi Mtendaji waBenki ya CRDB Huduma Shirikishi, Esther Kitoka akifuatilia mkutano wa 20wa wanahisa wa benki hiyo.
Wakurugenzi wa benki ya CRDB wakiwa katika mkutano huo.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB anayeshughulika na Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyopadhyay akiwa katika mkutano huo.
 Wanahisa wakiwa katika mkutano huo.
Wanahisa.
Baadhi ya maofisa wa benki ya CRDB wakiwa katika mkutano huo.
Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye akiwa katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Benki ya CRDB, Martin Mmari akimkabidhi tuzo ya uongozi uliotukuka katika benki ya CRDB aliyekuwa Mwenyekiti wa Mkutano Mkuu wa benki hiyo kwa kipindi cha miaka 15, Damian Ruhinda, makabidhiano hayo yalifanyika wakati wa mkutano mkuu wa 20 wa wanahisa wa benki hiyo uliofanyika katika ukumbi wa AICC jijini Arusha, mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Dk. Charles Kimei.
Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Dk. Charles Kimei akimpongeza, HamisKananda aliyepokea tuzo ya uongozi uliotukuka katika benki ya CRDB aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Mkutano Mkuu wa benki hiyo kwa kipindi cha miaka 15, mama Gatty Marwa. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi, Martin Mmari.
Mwenyekiti wa Bodi, Martin Mmari (katikati) akimkabidhi tuzo, Hamis Kananda aliyepokea tuzo ya uongozi uliotukuka katika benki ya CRDB kwa niaba ya aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Mkutano Mkuu wa benki hiyo kwa kipindi cha miaka 15, mama Gatty Marwa.  Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Dk. Charles Kimei.
Wanahisa.
wanahisa wakiwa katika mkutano huo.
Mwanahisa ambaye pia ni mtangazaji nguli, Salim Mbonde akiuliza swali katika mkutano huo.
Mwanahisa akipiga kura kuchagua wakurugenzi wa bodi CRDB.
Mwanahisa akipiga kura kuchagua wakurugenzi wa bodi CRDB kuziba nafasi za waliomaliza muda wao.
Msanii Chief Omary Mwaliko akimkabidhi ramani ya Afrika, Mwenyekiti wa Mkutano Mkuu wa 20 wa Benki ya CRDB.
Wanahisa wakiwa katika mkutano huo.
Wanahisa wakifuatilia mkutano huo.
Mkurugenzi wa Masoko Utafiti, Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa (kulia) akiwa katika mkutano huo.
Mkurugenzi wa Masoko Utafiti, Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa (kushoto) akijadiliana jambo na maofisa wa benki hiyo.





JOHN GUDO NYERERE KUZIKWA BUTIAMA SIKU YA JUMATANO

$
0
0
Mtoto wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, John Guido Nyerere enzi za uhai wake ambapo mazishi yake yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumatano Butiama.
Gari lililobeba mwili wa marehemu,  John Guido Nyerere.
 mwili ulipowasili nyumbani kwa Baba wa Taifa, Msasani.
Mwili ukishushwa.
Mwili ukishushwa nyumbani Msasani.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni akimkaribisha Waziri Mkuu Mizengo Pinda alipowasili nyumbani kwa Baba wa Taifa kwa ajili ya kutoa pole.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Makongoro Nyerere na Mkuu wa  Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda wakati wa msiba wa mtoto wa Nyerere, John Nyerere. 
Waziri Mkuu, Mizengo, Pinda (wa pili kushoto) alipofika nyumbani kwa baba wa Taifa kutoa pole.
Waziri Mkuu akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza la mtoto wa baba wa taifa, John Nyerere.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimpa pole mama Maria Nyerere.
Waziri Mkuu akiwapa pole ndugu wa marehemu.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiagana na mbunge wa Afrika Mashariki, Makongoro Nyerere.
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbrod Slaa akisalimiana na Makongoro Nyerere.
Dk. Slaa akiteta jambo na Makongoro Myerere.
Makongoro Nyerere (kulia) akiwa na Dk. Slaa alipofika kutoa pole nyumbani kwa mwalimu.
Dk. Slaa akisaini kitabu cha waombolezaji.
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willbrod Slaa akimpa pole mama Maria Nyerere.
Dk. Slaa akiwapa pole ndugu wa marehemu.

Article 1

STARS KWENDA AFRIKA KUSINI KESHO

$
0
0
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kesho jumatano inatarajiwa kusafiri kuelekea nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kushiriki michuano ya kombe la COSAFA.

Michuano ya COSAFA inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Mei 17 mpaka Mei 30, 2015 katika viwanja vya Olympia Park na Moruleng  jimbo la North West Province nchini Afrika Kusini ikishirikisha nchi za Kusini mwa Afrika huku Tanzania na Ghana zikiwa ni nchi waalikwa.

Taifa Stars itaondoka jijini Dar es salaam kesho majira ya saa 1 jioni, kwa usafiri wa shirika la ndege la Fasjet na kufika jijini Johanesburg saa 5 usiku.

Mara baada ya kupimwa afya jana na madaktari wachezaji Aishi Manula, Isihaka Hassan, Haroun Chanongo, Kelvin Friday na nahodha Nadir Haroub wamekutwa na majeruhi ambayo yamepelekea kutokuwepo katika kikosi kitakachosafiri kesho, watabakia nchini wakiendelea kufanya mazoezi chini ya ungalizi mpaka timu itakaporejea kutoka Afrika Kusini na kuungana kwa ajili ya maandalizi ya AFCON, huku Amri kiemba akipewa ruhusa kutokana na kuwa na matatizo ya kifamilia.

Msafara wa Taifa Stars utaongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa TFF, Ephaphra Swai ukijumuisha wachezaji 20 na benchi la ufundi, timu inatarajiwa kufikia katika hoteli ya Sun City iliyopo pembeni kidogo ya jiji la Rusterburg.

Kesho siku ya Alhamis kuanzia saa 3 asubuhi mpaka saa 7 mchana ni muda wa mapumziko, waandishi wa habari mnakaribishwa katika kambi ya timu ya Taifa iliyopo Tansoma Hotel kuweza kuongea na wachezaji, kocha mkuu na daktari wa timu kabla ya kuanza safari jioni.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Best Regards,
Viewing all 19659 articles
Browse latest View live