Na Mwandishi Wetu
KANISA la Dar es Salaam Pentecostal Church (DPC), la Kinondoni, limeandaa zawadi ya nzuri ya DVD katika msimu huu wa krismasi kwa watanzania na wapenda muziki wa Injili ya Sifa zivume.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo Kiongozi wa Kikundi cha Rivers of Life, Safari Paul amesema kuwa DVD ya Sifa Zivume imerekodiwa na kundi la Rivers of Life lenye waimbaji wazoefu wenye vipaji na uwezo wa hali ya juu kimuziki ambao wanafanya kazi chini ya kanisa hilo.
DVD hiyo imerekodiwa katika ubora wa hali ya juu na katika viwango vya kimataifa ambayo inaurefu wa masaa matatu ambapo imerekodiwa moja kwa moja ‘live’ yenyenyimbo 15 zenyeujumbe wa amani na matumaini kwa watu wote huku zikiwa na mguso wa ainayake wenyekuleta mabadiliko katika maisha.
Katika msimu huu wa siku kuu tunawaomba watu wote kuhakikisha wanapata DVD hii ya auna yake na pia kupata DVD ya Sifa Zuvume kwa ajili ya ndugu na marafiki kama zawadi ya krismasi.
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Dar es Salaam Pentecostal, Abel Majaliwa Thomas (katikati), akiwa na mchungaji Elly Mwende (kushoto) pamoja na Kiongozi wa Kikundi cha Rivers of Life, Safari Paul baada ya kuzindua DVD ya Sifa Zivume.
Kiongozi wa Kikundi cha Rivers of Life, Safari Paul akionesha DVD ya Sifa Zivume wakati wa hafla ya uzinduzi iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Dar es Salaam Pentecostal, Abel Majaliwa Thomas (katikati), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa DVD ya Sifa Zivume uliofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kutoka kulia ni Julius Kenyamanyara, Kiongozi wa Kikundi cha Rivers of Life, Safari Paul na mchungaji Elly Mwende.
Tunashuhudia uzinduzi.
Picha ya pamoja.
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Dar es Salaam Pentecostal, Abel Majaliwa Thomas akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa DVD ya Sifa Zivume.