Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Masoko ,kijiji cha Lupando wilaya ya Rungwe ,Katibu Mkuu waliwaambia wananchi hao kuwa urasimu na umangi meza wa watendaji wa serikali ndio unachangia kwa kiasi kikubwa kurudisha maendeleo yao nyuma na kusema kamwe CCM haitokubali hali hiyo iendelee na kusisitiza CCM itahakikisha wananchi wanapata haki zao za msingi kwanza.
Mwakilishi wa Wananchi wa Kijiji cha Lupando Ndugu Wema Mwaipopo akiomba sana kwa niaba ya wananchi wake watatuliwe suala la maji,umeme na barabara kwani hizo ndio zilikuwa ahadi kubwa za Mbunge na Rais.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kata ya Masoko kijiji cha Lupando na kuwaambia wananchi kuwa wapinzani ni sawa na Jogoo hata aamke saa ngapi hawezi fungua mlango,na kuwasisitiza wananchi wa kijiji hicho ni CCM pekee inayoweza kuwazungumzia na kero zao zikatatuliwa.
Asumwisi Asagwile Mwatebela ,Mlezi wa Vijana wa Chadema wilaya ya Rungwe akirudisha kadi yake kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na kujiunga rasmi na CCM.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Kiwira Rungwe na wakati wa ufunguzi wa vikundi viwili vya wajasiriamali ambapo aliwaambia vijana maendeleo yanaletwa kwa kufanya kazi kwa kujituma na waondoe mawazo kuwa Katiba mpya ndio itakuwa mwarobaini wa matatizo yao.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia maabara ya shule ya Sekondari ya Ikuti ikiwa moja ya sehemu ya ahadi ya serikali ya kujenga maabara katika kila shule ya Sekondari ya Kata.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa Nyumba za walimu wa shule ya Sekondari Ikuti wilayani Rungwe.