
Na Elizabeth John
MKALI wa muziki wa kizazi kipya nchini, Naseeb Abdul ‘Diamond Platinumz’ ametangaza ajira kwa wakazi wa Dar es Salaam wenye vipaji mbalimbali.
Kwa mujibu wa Diamond kupitia ukurasa wake wa Facebook, alisema ajira yake ni kwa wale wenye uwezo wa elimu ya kupiga picha, kushuti video na kuediti picha.
Alisema kuwa muambajia natakiwa kuwa na uwezo wa kutumia kamera za zamani na za kisasa, aende na mfano wa kazi ambazo amewahi kufanya zenye ubora wa 1080 na kuendelea na pia muombaji awe tayari kusafiri popote na muda wowote.
“Mimeamua kufanya hivi kutokana na nchi yetu kuwa na tatizo la ajira kwa vijana, kwa kufanya hivyo naamini kwaasilimia fulani nitakuwa nimepunguza tatizo hilo,”.
Aliongeza kuwa, muombaji anatakiwa kuwa na umri wa miaka kati ya 20 hadi 35 anatakiwa awasiliane naye kupitia email hii diamondplatnumz@gmail.com ama kwa namba ya simu 0755-700400.