Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Article 13

$
0
0
WAISLAMU WAHIMIZWA KUSHIKAMANA KATIKA ELIMU SHEIKH Athman Kaporo (kulia), wa Taasisi ya DYCCC  amewataka Waislamu nchini kushikamana katika suala la elimu ili kuleta mapinduzi ya haki kwenye mfumo mzima wa sekta hiyo muhimu.

Wito huo, aliutoa, wakati wa hafla fupi ya sherehe za kuwakabidhi vyeti na zawadi washindi wa mitihani ya Madrasa za mkoa wa Dar es Salaam, zilizofanyika katika shule ya DYCCC iliyoko Chang’ombe wilayani Temeke, jijini juzi.

Sheikh Kaporo alisema kutokana na mazingira ya dunia yalivyo, waislamu hawana budi katika kupigania  mapinduzi ya kielimu ambapo hilo sio jukumu la mtu mmoja au taasisi moja bali ni lazima kuwepo kwa mashirikiano mema na mazuri kwa wadau wote wa elimu ya kiislamu.
 
“Kazi inayofanywa na waalimu wa madrasa hapa chini ni kubwa, pia kazi inayofanywa na baadhi ya wapenda kheri ni kubwa, sasa ili tulete mapinduzi ya kweli katika elimu zote ni lazima tushirikiane kwa pamoja.

 “Leo vijana hawa wameonyesha uwezo mkubwa sana,tena wana vipaji vya hali ya juu,ninaamini iwapo tutashirikiana kuwaendeleza miongoni mwa vijana hawa watakuwa ni viongozi bora wenye hekima katika miaka ijayo”alisema.

Mwenyekiti wa Kamati ya Zakah na sadaka ya DYCCC Sheikh Abdallah Nahd ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo, alisema, kamati yake inaridhishwa na juhudi zinazofanywa na Idara ya madrasa ya DYCCC na kuahidi wataendelea kushirikiana nayo zaidi.

Katika hafla hiyo washindi wa mitihani hiyo mbali ya kukabidhiwa vyeti maalumu lakini pia walipewa zawadi mbalimbali zikiwemo vyarahani, feni, saa za ukutani na pesa taslimu.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>