Quantcast
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Article 15

SERIKALI IWABANE WACHINA WA KARIAKOO

Na Mwandishi Wetu

UMOJA wa Wafanyabiashara wa Kariakoo jijini Dar es Salaam, wameitaka serikali kutoa ufafanuzi kuhusu vibali vya Wachina wanaofanya biashara za kimachinga baadala ya uwekezaji mkubwa.

Kauli hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam na Katibu wa Umoja huo, Peter Kyando wakati alipokuwa akizungumza na kuhusu muingiliano huo wa biashara.

Alisema umoja huo unaitaka serikali kufanya hivyo kutokana na wachina hao kuingilia biashara ambazo zingeweza kufanywa na Wafanyabiashara wadogo wa Tanzania, anaamini vibali vyao haviwaruhusu kufanya hivyo.

Kyando alisema ingawa ni kweli wafanyabiashara wa hapa nyumbani wanalalamikia Wachina hao lakini bado wanaowajibika kutoa taarifa zao ni Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Viwanda na Biashara ambazo zinajua taarifa za vibali vya uingiaji wa watu hao.

Aliongeza kuwa baadhi ya wafanyabiashara wanahoji iwapo serikali imewaruhusu Wachina hao kufanyabiashara hizo baadala ya kukaa kimya. 


Kyando alisema inasikitisha kuwaona wachina waliodhaniwa kuwa ni wawekezaji wakubwa wakiuza barafu, maua, sufuria, mifuko ya kike na simu kwa mtindo wa kimachinga.

Kyando alisema yote hayo yanafahamika na wizara husika lakini kwa sababu malalamiko hayo yalikwisha wafikia na isitoshe hata watendaji wake wakipita maeneo ya Kariakoo wanajione lakini cha kushangaza wizara hizo zimekaa kimya.

“Unajua serikali yetu nayo inawakatisha tamaa wananchi wake kwa sababu wanajua kinacho lalamikiwa laikini wamekaa kimya sasa labda wanagoja wananchi wandamane”alisema Kyando.

Aidha, Kyando alisema ni jambo la ajabu kuwaona Wachina hao wakifanya wanavyotaka wakati Watanzania wanapokwenda China wanaulizwa maswali kuwa kilichowapeleka huko pia hawaruhusiwi kuendesha biashara ambazo wanaweza kuzifanya wenyeji wa huko.

Ni hivi karibuni wananchi mkoani Dodoma na Pwani walishangaa kuwaona wamachinga wa kichina waliokuwa wakipita kila mgahawa, baa na kwenye mikusanyiko ya watu wakiuza simu za viganjani.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>