Mshindi wa kwanza katika mbio za mita 10000 kwa Wanaume Fabian Nelson (Tanzania) katika Michezo ya Umoja wa wakuu wa Polisi kwa Nchi za kusini mwa Afrika (SARPPCO) Nchini Nambia akishangilia na bendera ya taifa mara baada ya kumaliza mbio hizo katika uwanja wa taifa wa Namibia (Picha zote na Frank Geofray-Jeshi la Polisi, Windhoek Namibia)
Mshindi wa kwanza katika mbio za mita 10000 kwa Wanaume Fabian Nelson (Tanzania) akivalishwa medali ya dhahabu na mmoja wa makamishna wa Polisi wa Namibia katika Michezo ya Umoja wa wakuu wa Polisi kwa Nchi za kusini mwa Afrika (SARPPCO) katika uwanja wa taifa wa Namibia.
Baadhi ya wanamichezo wa Tanzania wakishangilia ushindi wa kwanza katika mbio za mita 10000 kwa Wanaume katika Michezo ya Umoja wa wakuu wa Polisi kwa Nchi za kusini mwa Afrika (SARPPCO) katika uwanja wa taifa wa Namibia.
Wanaridaha wa mbio za mita 10000 kwa Wanaume wakikimbia katika Michezo ya Umoja wa wakuu wa Polisi kwa Nchi za kusini mwa Afrika (SARPPCO) Nchini Nambia.
Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi,Windhoek
Wanariadha wanaowakilisha Jeshi la Polisi Tanzania katika michezo ya Umoja wa wakuu wa Polisi kusini mwa Afrika SARPCCO nchini Namibia wameanza vyema mbio hizo baada ya kufanikiwa kunyakua medali za Dhahabu na fedha katika mbio za mita elfu 10000 wanaume.
Aliyenyakua medali ya dhahabu ni Mwanariadha Fabian Nelson ambaye alitumia dakika 30 na sekunde 42 huku akifuatiwa na Wilbrado Peter (Tanzania ) ambaye alitumia dakika 30 na sekunde 45 na kuwaacha wanariadha wengine nyuma kutoka mataifa ya Zimbabwe ,Namibia ,Botwasana na Angola .
Wengine walioipatia Tanzania Medali ni pamoja na Basili John mita 800 (Shaba ) na Mohamed Ibrahim mchezo wa kurusha kisahani (shaba ).
Katika mpira wa miguu mechi ya ufunguzi ilizikutanisha wenyeji Namibia na Msumbiji ambapo Namibia iliichapa Msumbiji mabao 2 kwa 0 huku kwenye mpira wa miguu wanawake Namibia na Angola zilitoka suluhu ya bila kufungana.