Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

DIMPOZ KUIWEKA 'TUPOGO' KIDEONI

$
0
0
Na Elizabeth John
BAADA ya kuanza kufanya vizuri na kazi yake ya ‘Tupogo’, mkali wa muziki wa kizazi kipya nchini, Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ anatarajia kuanza kupiga picha kwaajili ya video ya kazi hiyo.

Kazi hiyo aliyoisambaza wiki iliyopita katika vituo mbalimbali vya redio, kamshirikisha msanii kutoka Nigeria J Martin.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Ommy Dimpoz alisema, hivi karibuni anatarajia kwenda Nigeria kwaajili ya kutengeneza video ya kazi hiyo ambayo tayari imeanza kufanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio.

“Naomba mashabiki wangu wakae mkao wa kula kwaajili ya video hiyo ambayo naamini nayo itakua poa kama video zingine zilizotangulia,” alisema.

Dimpoz alishawahi kutamba na vibao vyake kama, Nai nai, Baadae na Me and You ambazo zilifanya vizuri na kumtambulisha katika tasnia ya muziki huo.



Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>