Kutoka Kulia ni Mwenyekiti wa TEHAMA Class na Msanii wa Kizazi Kipya Bongo Flave, Inspector Haorun aka Babu akiwa na watalaamu wa TEHAMA(ICT) wapili ni Diana Mtambalike ambaye ni Katibu wa kampuni hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Fahamu Campany ambao ndio waandaji na watoaji wa elimu ya TEHAMA kwa shule za msingi Bw, Mstafa Rubunda ,Mtalamu wa maswala ya TEHAMA, na Meneja wa Ufundi wa Fahamu Campany.Yusuph Kannokole wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizaka semina ya Viongozi ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya semina ya wasanii zaidi ya 100.
Na Mwandishi Wetu
Kampuni ya Fahamu inayojihusisha na utoaji wa elimu Tehama( ICT) kwa shule za msingi jijini Dar es Salaam, imeamua kuingia ndani zaidi katika kutoa elimu kwa shule za msingi kwa kushirikiana na wasanii wa muziki wa kizazi kipya bongo freva na wasanii wa filam nchini
Akizungumzia umuhimu wa utoaji wa elimu hiyo ya TEHAMA kwa shule za msingi Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Bwana Mustafa Rubunda alise ameona kuna umuhimu wa kutoa mafunzo hayo kwa watoto wa shule za msingi kuanzia darasa la pili hadi la saba hii ni kutokana na changamoto ya mabadiliko ya kisayansi na teknolojia amba vijana hao watakuwa na uwezo wa kiubunifu pamoja na kibiashara.
.Mstafa alisema kuwa ili kuhakikisha lengo linakamiliaka Kampuni yake ya Fahamu imeamua kuandaa semina kwa wasanii mbalimbali zaidi ya 100, ambao wataongozwa na Msanii mkongwe Inspector Haorun aka babu,ambaye ndiye Mwenyekiti wa TEHAMA CLASS,na mwakilishi wa wasanii.
Semina hiyo inategemea kufanyika Mwezi huu jijini Dar es Salaam, ambapo itawajumuisha wasanii ,wanafunzi wa sekondari, pamoja na wa Vyuo Vikuu lengo la kuwa jumuisha katika semina ni kuona umuhimu wa kuweza kuwasaidia wadogo zao katika kuhakikisha wanakuwa watumiaji wa TEHAMA ambayo sasa ndiyo iliyobeba Teknolojia ya Habari na Mawasiliano,
Kwa upande wa serikali kupitia TAMISEMI, wamekuwa bega kwa bega kwa kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Fahamu Campany kwa ajili ya kutoa elimu hiyo kwa watoto wa shule za msigi nchini.