NMB YAENDELEA KUZINDUA BUSINESS CLUB “SASA NI ZAMU YA KARATU”
Benki ya NMB imeendelea kuwa kinara katika kubuni na kuboresha huduma mbali mbali za kibenki, ili kuwawezesha wateja wake kupata unafuu na urahisi wa upatikanaji wa huduma za kibenki nchini Tanzania.
Katika kulizingatia hili, NMB imezidi kuzindua klabu maalum za wafanyabiashara maarufu kama NMB Business Club. Hadi sasa zaidi ya NMB Business Club 29 zimekwisha zinduliwa nchi nzima.
Kupitia NMB Business Club wajasiriamali wanaowezeshwa na benki ya NMB wamekua wakipata nafasi ya kujifunza jinsi ya kuandika michanganuo ya biashara zao na pia kuendelea kua vinara wa biashara.
Mhandisi Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Tulinumpoki Mwakalukwa akitoa shukrani zake kwa NMB mara baada ya kuzindua rasmi NMB Business Club wilaya ya Karatu. Kushoto ni Meneja wa NMB tawi la Karatu , Evarist Mtaro na Mkuu wa Kitengo cha wajasiriamali wadogo wadogo na wakati wa NMB, Filbert Mponzi.
Sehemu ya wanachama wa NMB Business Club wilaya ya Karatu wakifurahia uzinduzi wa NMB Business Club.
Mkuu wa Kitengo cha wajasiriamali wadogo wadogo na wakati wa NMB, Filbert Mponzi akimkabidhi mwenyekiti wa NMB Business Club, Paulith Jack mara baada ya kuibuka kidedea kwenye mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa NMB Business Club Karatu .