Benki ya NMB imefadhili UMITASHUMTA kwenye manispaa ya Sumbawanga kwa kutoa vifaa vya michezo vyenye thamani ya shilingi milioni tisa. Lengo kuu la ufadhili huu ni kusaidiana na UMITASHUMTA katika kuibua na kuendeleza vipaji vya michezo kwa shule za msingi nchini Tanzania.
Meneja wa NMB Tawi la Sumbawanga, John Chinguku akimkabidhi Ofisa Elimu, Modesta Zambi sehemu ya vifaa vya michezo vitakavyotumika kwenye UMITASHUMTA manispaa ya Sumbawanga. Makabidhiano haya yalifanyika hivi karibuni kwenye manispaa hiyo.
Maofisa wa Benki ya NMB na maofisa wa Manispaa ya Sumbawanga wakisikiliza maelekezo kutoka kwa Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Sumbawanga, John Chinguku (tatu kulia) mara baada ya kukabidhi vifaa vya michezo.
Mipira iliyokabidhiwa.