Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Msama Promotions yamshukuru Rais JK

$
0
0
NA FRANCIS DANDE

 MWENYEKITI wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la kuombea amani Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, Alex Msama  (pichani) amempongeza Rais Jakaya Kikwete kwa kukubali kuwa mgeni rasmi katika tukio hilo lenye umuhimu na uzito mkubwa kwa mustakabali wa taifa.

 Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Msama ambaye kupitia kampuni yake ya Msama Promotions ndiye amekuwa mwasisi wa matamasha ya muziki wa injili tangu mwaka 2000, alisema hatua ya Rais kikwete kukubakli mwaliko wao, kumewapa ari na nguvu zaidi. “Unajua Rais ni mtu mwenye majukumu mengi sana, hivyo hatua yetu ya kupeleka ombi la kumtaka awe mgeni wetu na kukubali, ni jambo la furaha sana kwetu kama Msama Promotions,” alisema Msama. 

 Msama alisema mbali ya Rais Kikwete kujumuika na watanzania katika tukio hilo la kuombea amani uchaguzi mkuu, pia kwake Tamasha hilo litakuwa na kumbukumbu kubwa kwake kabla ya kuondoka madarakani baada ya uchaguzi mkuu. 

 “Tunajua Rais Kikwete anakwenda kumaliza muda wake na kukabidhi madaraka kwa mwingine ajaye, hivyo kwa namna yoyote ile huenda likawa tukio la mwisho la aina hii akiwa ndani ya madaraka ya urais,” alisema Msama. 

 Alisema wapenzi, mashabiki na wapendwa katika kristo na wananchi kwa ujumla wana kila sababu ya kujitokeza kwa wingi katika tamasha la kesho Uwanja wa Taifa kuombea amani uchaguzi Mkuu. 

 Msama alisema wanapaswa kufanya hivyo sio tu kutokana na umuhimu wa tukio hilo kwa maslahi ya taifa, pia kumtia moyo Rais Kikwete ambaye amekuwa mdau mkubwa wa muziki wa injili kwani si nmara ya kwanza kukubali mwaliko wa Msama Promotions. Alisema alikwenda mbali na kusema hata mwaka 2011, Rais Kikwete alikubali kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Pasaka ambalo lilifanyika Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam, ikiwa ni kielelezo cha umoja na mshikamano kwa kitaifa. Msama alisema kwa mazingira hayo, wao Msama Promotions wana kila sababu ya kutoa shukrani kwa Rais Kikwete na kumpongeza kwa kuwa karibu na muziki wa injili, akisema amesaidi kuupa hadhi na heshima kubwa, hivyo kutimia kwa malengo mbalimbali.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>