Na Hosea Joseph, Kaliua
MGOMBEA ubunge wa jimbo la Kaliua, Tabora, (CCM), Profesa Juma Kapuya amefichua mjadala uliokuwa ukiendeshwa na wapinzani wake juu ya matumizi ya fedha za mfuko wa jimbo katika uongozi wake.
Akizungumza na wananchi wakati akiomba kura Kata ya Kamusekwa, alibainisha kuwa yeye sio fisadi kwakuwa kila jambo liko wazi juu ya matumizi ya fedha hizo.
Alisema wapinzani wake wamekuwa wakiwapotosha wananchi kuwa anatumia fedha za mfuko huo jambo ambalo linaweza kuondoa imani nakuibua mgogoro usio na tija kinyume na ukweli ulivyo.
"Fedha za mfuko wa jimbo hapewi mbunge kwani zinatumwa Halmashauri milioni 70 kwa mwaka na matumizi yake hufanyiwa ukaguzi yakinifu na mara nyingi nimepongezwa sana kwa kuzisimamia kwa maendeleo ya Halmashauri na kupata hati safi" alisema Kapuya.
Aidha, Kapuya aliwaomba wakazi hao wamchague na chama kwaujumla kwakuwa amekuwa akitumia fedha za mshahara na misaada ya rafiki zake kuwasaidia wananchi katika mahitaji mbali mbali na hata katika shughuli za maendeleo.
Pia Kapuya alitangaza irani ya chama chake na kuahidi yaliyomo mengi ni yakuwasaidia wananchi wa jimbo lake hasa katika suala la miundombinu ya barabara na reli ya Kaliua Mpanda hadi Karema kwa kiwango cha kimataifa.
"Nawaahidi sitawaangusha kwani mkimchagua Magufuli kwakishindo hatutapatashida kwa lolote maana nimtekelezaji na mfatiliaji makini katika kila kazi inayomhusu" alisema Kapuya.
Kapuya alitumia fursa hiyo kumnadi mgombea udiwani wa chama
chake wa Kata ya Kamsekwa, Athumani Saidi ili achaguliwe na
kukamilisha utatu wa uongozi unaoendana bila kuchanganya.