Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Solly Mahlangu, Muhando, John Lisu waanza kujifua

$
0
0
NA MWANDISHI WETU

WAIMBAJI wanaotarajia kushambulia jukwaa la Tamasha la kuombea Amani wameanza rasmi kujifua ikiwa ni maandalizi ya tamasha hilo linalotarajia kuanza kutimua vumbi Oktoba 4 uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kabla ya kuhamia katika mikoa mingine 10

Wakizungumza na gazeti hili waimbaji hao, walisema kuwa wameanza kujifua kwa ajili ya Tamsha hilo ambalo linashirikisha waimbaji mbalimbali kutoka Afrika na Uingereza.

Waimbaji hao walisema kuwa kuwa kutokana na kwamba wataimba ‘live’, hivyo wamelazimika kuanza mazoezi mapema kwa ajili ya siku hiyo ambayo ni maalum kwa Taifa la Tanzania.

Mwimbaji Solly Mahlangu alizungumza na gaezeti hili kwa njia ya simu na kuthibitisha kuwa ameshaanza mazoezi japokuwa ni mzoefu wa kuimba ‘live’ lakini kutokana na umaalum wa tamasha hilo anaongeza zaidi vionjo ili kuendana na hadhi ya tamasha hilo.

Naye John Lisu alisema kuwa yeye ni kawaida yake kuimba live aliwataka watanzania kufika kwa wingi kuona uimbaji wa tofauti katika tamasha hilo huku akisisitiza kuwa kutakuwa na nyimbo maalumu za kuliombea taifa.

Malkia wa nyimbo za injili nchini, Rose Muhando alisema kuwa mazoezi kwake ni muhimu kwa kuwa kawaida yake ni kuwainua watanzania katika viti vyao ambako alisema kwa maandalizi anayoyafanya atafanya mambo tofauti na ilivyozoeleka katika maonesho mengine aliyowahi kuhudhuria.

Waimbaji wengine watakaokuwepo ni pamoja na  Sipho Makhabane, Glorius Celebrations ‘Kwetu Pazuri’, Ephraim Sekeleti , Solomon Mukubwa, Anastazia Mukabwa na Sara K.

Kwa upande wa waimbaji mahiri wa Tanzania, ni Boniface Mwaitege, Martha Mwaipaja, Beatrice Mwaipaja, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Joshua Mlelwa na Christopher Mwahangila. Chanzo Tanzania Daima.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659