Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

'MY BABY' YAFANYA KWELI KIDEONI

$
0
0

Na Elizabeth John
VIDEO ya ngoma inayokwenda kwa jina la ‘My Baby’ iliyoimbwa na nyota wa muziki nchini, Quick Rocka, Shaa na Marehemu Ngwea imeanza kufanya vizuri katika vituo mbalimbali vya televisheni hapa nchini.

Wimbo huo ni kati ya nyimbo zinazofanya vizuri katika tasnia ya muziki huo kutokana  na wasanii walioshirikiana katika kazi hiyo kukubalika katika soko la muziki na kujitahidi kutunga
 mashairi yaliyosimama.

Kwa mujibu wa Shaa, kazi hiyo wameisambaza wiki iliyopita katika vituo mbalimbali vya televisheni wakiwa na lengo la kuwapa raha mashabiki wa kazi zao.

“Kiukweli kazi hii imekubalika katika soko la muziki huu, tunawashukuru mashabiki wetu kwa kuipokea vizuri kazi hii ambayo wengi wanaipenda kutokana na kuwa na mashairi ya kuvutia,” alisema Shaa.

Wasanii hao walioimba kazi hiyo ni kati ya wasanii ambao wanafanya vizuri katika tasnia hiyo ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kutokana na kiwango chao kuwa juu.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>