Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akilihutubia Bunge la Tanzania na hatimae kulifunga. Kulia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anna Makinda. (Picha na Joseph Senga)
Spika wa Bunge Anne Makinda akimuongoza Rais Jakaya Kikwete kuingia katika ukumbi wa Bunge.
Rais Kikwete akitoka mara baada ya kulivunja Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Rais mstaafu, Ali Hassan Mwinyi na Rais mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa.
Wimbo wa taifa ukipigwa.

Rais Jakaya Kikwete, akionyesha mfano wa ufunguo mara baada ya kukabidhiwa wakati wa uzinduzi wa ukumbi mpya wa mikutano wa CCM uliopo mkoani Dodoma. (Picha na OMR)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akimkabidhi mfano wa ufunguo wa Ukumbi mpya wa mikutano wa CCM wa Dodoma Convention Centre, Katibu Mkuu wa CCM Bara, Abrahman Kinana, baada ya kuzindua rasmi ukumbi huo mjini Dodoma.Picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa Chama na Serikali baada ya uzinduzi huo.
Rais Jakaya Kikwete na baadhi ya Viongozi, wakitembelea kukagua ukumbi huo baada ya uzinduzi.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete, akizungumza wakati wa uzinduzi wa ukumbi mpya wa mikutano wa CCM wa Dodoma Convention Centre, uliopo mjini Dodoma.