Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

SIR. GEORGE KAHAMA AMBARIKI MH. MEMBE KUWANIA URAIS WA TANZANIA

$
0
0
 Mwanasiasa mkongwe nchini, Sir. George Kahama akizungumza na wana CCM na wakazi wa Lindi katika Viwanja vya Ofisi ya CCM Mkoa jana, wakati Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (wa tatu kushoto waliokaa), alipotangaza nia ya kugombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu ujao wa Mwezi Oktoba, katika Viwanja vya Ofisi ya CCM Mkoa jana. Wengeni (kutoka kushoto) ni Katibu wa CCM Mkoa wa Lindi, Adelina Gefi na Mke wa Waziri Membe, mama Dorcas Membe.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kushoto), akimpongeza Mwanasiasa mkongwe nchini, Sir. George Kahama baada ya Mzee Kahama kuhutubia umati wa  wana CCM na wakazi wa Lindi katika Viwanja vya Ofisi ya CCM Mkoa jana, wakati Mheshimiwa Membe alipotangaza nia ya kugombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu ujao wa Mwezi Oktoba.
Mama Dorcas Membe mke wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe, akimpongeza Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Lindi, Mzee Ali Mtopa baada ya kuhutubia umati wa  wana CCM na wakazi wa Lindi katika Viwanja vya Ofisi ya CCM Mkoani humo jana, wakati Mheshimiwa Membe (katikati), alipotangaza nia ya kugombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu ujao wa Mwezi Oktoba.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>