Na Mwandishi Wetu
KITUO Cha Uwekezaji nchini (TIC) kimesema kinamiliki viwanja viwili na shamba moja nchini hivyo kama
kuna Kiwanja chenye hati ya TIC basi wao hawahusiki.
Hayo yamekuja siku chache baada ya waandishi wa habari kutaka kupata ufafanuzi wa kiwanja chenye namba
40118 kilichopo eneo la Wazo Hill Katika Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Akizungumza Waandishi wa habari mwanzoni mwa wiki hii kuhusu hati hiyo Ofisa Mipango Miji wa TIC
Elibarik Wilfred alisema kutokana na hati hiyo kwa jinsi ilivyo kisheria wao ndio wamiliki halali wa eneo hilo
lakini si kweli kuwa wao ndio wamiliki wa Kiwanja hicho hivyo hawahusiki nacho.
"Sisi hatumiliki hiki Kiwanja kwani TIC tunamiliki Viwanja viwili ambavyo ni hiki hapa Dar es Salaam ambapo zipo ofisi zetu na cha pili kipo Kimandoro Arusha lakini kingine si Kiwanja bali ni Shamba lililopo Mkulazi Kilombero mkoani Morogoro"alisema Wilfred.
Akizungumzia kuhusu kutumika kwa jina la TIC kumiliki Kiwanja hicho au Viwanja vingine bila wao kuhusika
wala kutambua alisema hilo ni jambo lingine.
Kiwanja hicho ambacho kinadaiwa kuwa ndio ambacho Mafundi Gereji wa Manispaa ya Kinondoni ndipo walipo
baada ya kupelekwa hapo na Manispaa hiyo baada ya kubomoa gereji zote bubu zilizoko katika Manispaa hiyo ili kuiweka katika hali ya usafi
Akizungumzia kuhusu hilo Diwani wa Kata ya Wazo John Murro alisema tayari pia nyaraka hizo zimemfikia
Meya wa Manispaa ya Kinondoni Yusuph Mwenda.
"Ni kweli Meya naye amezipata na amemwagiza ofisa wa Mipango Miji na Ofisa ardhi ili kujiridhisha
kuhusu TIC kumiliki Kiwanja hicho."alisema Morro
Baadhi ya watu waliotoa maoni yao kuhusu sakata hilo walisema inawezekana jina la TIC lilikuwa
linatumika ili watu wajipatie kula na familia zao huku wanyonge wakidhulumiwa
Walisema kumekuwa na tabia ya watu wenye fedha kutumia fedha zao kudhulumu haki za watu wengine sasa
kama TIC wamekana kumiliki Kiwanja hicho basi Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi waweke wazi nani ambaye analipia Kiwanja hicho ili akamatwe
"Kama kweli TIc wamekana kumiliki Kiwanja hicho basi wanaokilipia wakamatwe ili iwe fundisho kwa wengine wenye kudhulumu haki za wenzao ili kujinufaisha wao na familia zao"walisema watu hao.