Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

KAIRUKI HOSPITALI YAINGIZA MTAMBO MAALUMU WA UPASUAJI

$
0
0
NA MIKA NDABA

HOSPITALI ya Kumbukumbu ya Kairuki Mikocheni jijini Dar es Salaam, imeingiza mtambo maalumu wa kisasa kutoka Kampuni ya Ethicon ya Marekani utakaokuwa ukitumika katika upasuaji wa  kawaida na ule matobo.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Daktari Bingwa wa Upasuaji Dk. Muganyizi Kairuki alisema kuwa mtambo huo ni wa kwanza nchini na unatumia nishati ya sauti au mwangwi I ( ultrasound).

Alisema mtambo huo una uwezo  kubwa kiasi cha kuweza kukata mwili wa binadamu bila kupoteza hata chembe ya damu kwa mgonjwa.

"Mtambo huu wa gharama kubwa unafahamika kama Ultrasonic and Advanced Bipolar HARMONIC Generator, ambapo unaweza kufanya zaidi ya kazi nne kwa muda mmoja," alisema.

Akitaja kazi na umuhimu wa mtambo huo, Dk. Kairuki alisema unapunguza matumizi na mahitaji ya damu ambayo ni adimu kupatikana kwa wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji hospitalini .

Pili, upunguza athari zinazoweza kutokea kwa viungo vya jirani wakati wa upasuaji kama ilivyo kwa mitambo ya  zamani inayotumika sasa katiika hospitali nyingine.

"Pia inasaidia kurahisisha na kuharakisha upasuaji hivyo kupunguza muda wa upasuaji kwa jumla, pamoja na kuondoa kabisa matumizi ya nyuzi za kushonea viungo vya ndani wakati wa upasuaji"aliongeza Dk. Kairuki.
Mtambo maalumu wa kisasa kutoka Kampuni ya Ethicon ya  Marekani  utakaokuwa ukitumika katika upasuaji wa    kawaida na ule wa matobo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>