Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia (kulia) akipokea zawadi ya shati maalumu lililotolewa na wakazi wa jimbo la Vunjo kwa ajili ya kumpelekea aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji mstaafu, Joseph Warioba, pia walikabidhi kiasi cha shilingi 200,000 ikiwa ni nauli ya kumwezesha kufika jimboni humo kutoa elimu juu ya Katiba. (Picha na Dixon Busagaga)
Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassari akizungumza na wananchi katika jimbo la Vunjo,wakati wa mkutano wa hadhara ulioitishwa na Chama cha NCCR-Mageuzi kwa lengo la kuwashukuru kwa kuchagua wenyeviti wengi waliotokana na chama cha NCCR-Mageuzi,mkutano uliohutubiwa pia na Mbunge wa kuteuliwa na rais,James Mbatia.