Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

VIGOGO WATATU WALIOPATA MGAO WA FEDHA ZA ESCROW WAFIKISHWA MAHAKAMANI LEO

$
0
0
Meneja wa Msamaha wa Mamlaka ya Kodi na Mapato Tanzania (TRA),  Kyabukoba Mutabingwa (kulia), Mkurugenzi wa fedha Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Julius Angello pamoja na Mwanasheria Mwandamizi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Steven Urassa wakiingia katika chumba cha mahakama.
Mkurugenzi wa fedha Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Julius Angello akiwa chini ya ulinzi wa askari Polisi.
Mkurugenzi wa fedha Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Julius Angello akijifunika na suti yake kuficha sura yake wakati alipofika mahakamani.


Mkurugenzi wa fedha Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Julius Angello akijifunika na suti yake kuficha sura yake wakati alipofika mahakamani.
Watuhumiwa wakiwa chini ya ulinzi.
Mkurugenzi wa Fedha wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Julius Angello anadaiwa kupokea zaidi ya bilioni 1 kupitia akaunti namba 00120102646201 zikiwa ni sehemu ya fedha za Akaunti ya Tegeta Escrow.
Mkurugenzi wa Fedha wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Julius Angello anadaiwa kupokea zaidi ya bilioni 1 kupitia akaunti namba 00120102646201 zikiwa ni sehemu ya fedha za Akaunti ya Tegeta Escrow.
Mkurugenzi wa Fedha wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Julius Angello anadaiwa kupokea zaidi ya bilioni 1 kupitia akaunti namba 00120102646201 zikiwa ni sehemu ya fedha za Akaunti ya Tegeta Escrow.
Mkurugenzi wa Fedha wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Julius Angello anadaiwa kupokea zaidi ya bilioni 1 kupitia akaunti namba 00120102646201 zikiwa ni sehemu ya fedha za Akaunti ya Tegeta Escrow.
Mkurugenzi wa Fedha wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Julius Angello anadaiwa kupokea zaidi ya bilioni 1 kupitia akaunti namba 00120102646201 zikiwa ni sehemu ya fedha za Akaunti ya Tegeta Escrow.
Mkurugenzi wa Fedha wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Julius Angello akitoka mahakamani.
Mwanasheria Mwandamizi wa (Tanesco),  Steven Urassa anakabiliwa na shitaka moja la kupokea zaidi ya sh. milioni mia moja kupitia namba 00120102658101 zikiwa sehemu ya Akaunti ya Tegeta Esrcow.

Na Mwandishi Wetu

VIGOGO wengine watatu wamepanisha kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu wakikabilia na mashitaka ya kujipatia fedha kwa njia rushwa kutoka kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow.


Vigogo waliopandishwa kizimbani leo katika mahakama hiyo ni Meneja wa Mamlaka ya Kodi Tanzania (TRA),  Kyabukoba Mutabingwa, Mkurugenzi wa fedha Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Julius Angello pamoja na Mwanasheria Mwandamizi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco),Steven Urassa.

Mshitakiwa wa kwanza katika sakata hilo, ambaye ni Mkurugenzi wa BoT, Angello alisomewa shitaka lake na Wakili wa Serikali Leornda Swai akishirikiana na Max Ari mbele ya Hakimu Mkazi Devotha Kisoka, huku upande wa utetezi ukiwakilishwa na Wakili Jamuhuri  Jonson.

Wakili Swai alieleza kwamba mshitakiwa anakabiliwa na shitaka moja la kula rushwa Februari 6, 2014 katika benki ya Mkombozi wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, ambapo alijipatia kiasi cha fedha zaidi ya bilioni 1 kupitia namba 00120102646201 zikiwa ni sehemu ya fedha za Akaunti ya Tegeta Escrow.

Alieleza kwamba, mshitakiwa alijipatia fedhab hizo ikiwa ni tuzo kwa kusaidia malipo yaliyofanyika kwenye Akaunti hiyo ya Tegeta baada ya kuwepo kwa makubaliano baina na Kampuni ya IPTL, ikiwa kinyume na matakwa ya mwajiri wake.

Swai alieleza kwamba upelelezi wa shauri hilo umekamilika, pia shitaka hilo halihitaji kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP).Pia aliiomba mahakama izuie matumizi ya fedha hizo kutokana na fedha hizo zina kesi mhakamani hapo.

Hata hivyo upande wa utetezi kupitia wakili wake Jonson ulimuomba hakimu atoe dhamana kulingana na shitaka lenywe kwani mshitakiwa bado ni Mkurugenzi, pia kosa hilo alikugundulika kwa siku moja.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Kisoka alimuuliza mshitakiwa kuhusu shitaka hilo, lakini mshitakiwa alikana mashitaka.

Hata hivyo alitoa masharti ya dhamana kwa mshitakiwa huyo kutoa kiasi cha Sh milioni 80 taslimu au hati yenye thamani ya fedha hizo, pamoja na wadhamini wawili ambao wanatakiwa kuwa na bondi ya Milioni 50 kwa kila mmoja.

Hakimu Kisoka alisema kwamba kwa kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na mtuhumiwa kashindwa kutekeleza masharti ya dhamana anarudishwa rumande hadi Januari 27, mwaka huu kwa ajili ya kukamilisha dhmana yake na usikilizwaji wa awali.

Pia mshitakiwa wa pili kupandishwa kizimbani ni Mwanasheria Mwandamizi wa (Tanesco), Urassa mbele ya Hakimu Mkazi Janeth Kaluyenda, ambapo upande wa Jamhuri uliwakilishwa na wakili Swai, huku upande wa utetezi ukiwakilishwa na Jopo la Mawakili watatu likiongozwa na Jamhuri Jonson, Francis Kugesha na Peter Kibatala.

Wakili Swai alieleza kwamba, mshitakiwa anakabiliwa na shitaka moja la kupokea rushwa mnamo Februari  14, mwaka jana katika Benki ya Mkombozi Tawi la St. Joseph lililopo Ilala, ambapo kiasi hicho alichopokea ni zaidi ya milioni mia moja kupitia namba 00120102658101 zikiwa sehemu ya Akaunti ya Tegeta Esrcow ambazo alizipokea kutoka kwa Rugemalira.

Alidai kwamba Urassa alizipokea fedha hizo ikiowa kama tuzo ya kuiwakirisha Tanesco kama Shirika la uzarishaji umeme nchini mbele ya Mahakama ikiwa kinyume na matakwa ya mwajiri wake.Swai aliongeza kwamba upelelezi wa shauri hiolo umekamilika, pia anaiomba Mahakama izuie matumizi ya fedha hizo.

Baada ya kusomewa mashitaka yake, Hakimu Kaluyenda alimuuliza mshitakiwa kama anakubaliana na kosa hilo, lakini alikanusha.

Ili kupata dhamana Hakimu Kaluyenda alimtaka mshitakiwa alipe fedha taslimu za Milioni 81 au hati yenye thamani ya fedha hizo, pamoja nawadhamini wawili, mmoja awe mtumishi wa umma, pia wawe na vitambulisho pamoja na barua za ofisi wanazofanyia kazi.
 
Baada ya mshitakiwa kukamilisha baadhi ya vipengele vya dhamana, Hakimu Kaluyenda alimuachia kwa dhmana mshitakiwa huyo, pamoja na kuahirisha kesi hiyo hadi Februari 11, mwaka huu kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali.

Hata hivyo mtuhumiwa wa tatu katika sakata hilo, ambaye ni Meneja wa Msamaha wa (TRA), Mutabingwa alisomewa mashitaka yake na wakili Swai mbele ya Hakimu Kaluyenda.

Wakili Swai alidai kwamba mshitakiwa anakabiliwa na makosa manne ya kutoa na kupokea rushwa, ambapo kosa la kwanza la kupokea rushwa alilifanya Januari 17, 2014 katika Benki ya Mkombozi, kiasi cha zaidi ya Bilioni moja kupitia namba za akaunti 0011020613801 zikiwa ni sehemu ya Akaunti ya Tegeta Esrcow kutoka kwa Rugemalira.

Alieleza kwamba mshitakiwa alizipokea fedha hizo ikiwa ni tuzo ya kuiwakilisha TRA pamoja na Kampuni ya VIP ikiwa kinyume na matakwa ya mwajiri wake.

Shitaka la pili linalomkabili Mutabingwa, inadaiwa kwamba Julai 15, mwaka jana kupitia Benki hiyo ya Mkombozi alipokea rushwa ya zaidi milioni mia moja kupitia akaunti namba ya benki 00110202613801 zikiwa sehemu ya Akaunti ya Tegeta ambazo alizipokea kutoka kwa Rugemalira zikiwa kama tuzo ya kuiwakilisha TRA na Kampuni ya VIP.

Pia shitaka la tatu, inadai kwamba Agosti 26, 2014 kupitia benki hiyo hiyo, Mutabingwa alipokea tena rushwa ya zaidi milioni mia moja kupitia Akaunti hiyo hiyo ya benki zikiwa sehemu ya Akaunti ya Tegeta Esrow kutoka kwa Rugemalirab kama muwakilishi wa TRA na Kampuni ya VIP.

Hata hivyo katika shitaka la nne, Swai alieleza kwamba Novemba 14, 2014 kupitia Benki hiyo hiyo ya Mkombozi iliyopo Ilala mshitakiwa alipokea zaidi ya Milioni mia moja kupitia namba zile zile za akaunti yake kutoka kwa Rugemalira ikiwa kama tuzo ya kuiwakilisha TRA na Kampuni ya VIP.

Baada ya kusoma mashitaka hayo, Swai aliiomba Mahakama izuie matumizi ya fedha hizo hadi keszi hiyo itakapoisha, pia sheria izingatiwe katika utoaji wa dhamana.

Hata hivyo Hakimu Kaluyenda alimuuliza mshitakiwa kama anakubaliana na mashitaka hayo, lakini alikanusha.Pia mshitakiwa alitakiwa kutoa fedha taslimu Bilioni 1, pamoja na wadhamini watatu, wawili wakiwa watumishi wa umma pamoja na bondi ya Sh.milioni 340 kwa kila mmoja.

Baada ya kutoa masharti hayo, Hakimu Kaluyenda aliahirisha kesi hiyop hadi Januari 29, mwaka huu kutokana na mtuhumiwa kushindwa kukamilisha masharti ya dhamana na mshitakiwa huyo alirudishwa rumande.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>