Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi dawa kwa mganga mkuu wa hospitali ya jimbo la Mpendae Dr. Omar Shaban Amran wakati alipokabidhi sehemu ya madawa kwa hospitali hiyo ambayo yametolewa na mbunge wa jimbo la Mpendae Mh. Salum Turki kiasi cha makontena ya dawa manne yenye thamani ya shilingi Bilioni Moja na pointi Nne yatakayosaidia katika hospitali zote za Zanzibar, Kinana akiongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi amemalizia ziara yake leo katika mkoa wa Mjini Magharibi wilaya ya Amani jimbo la Mpendae kabla ya kuendelea na ziara mikoa mingine ya Zanzibar. (Picha na Fullshangwe)
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kazi ya ukarabati wa barabara kwa kusambaza kifusi katika barabara inayounganisha hospitali ya Jimbo la Mpendae na Barabara kuu ya Mchina.
Umati wa watu waliohudhuria ukifuatilia mambo muhimu yaliyokuwa yakielezwa na Ndugu Abdulrahman Kinana hayupo pichani.