Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi akizungumza wakati wa hafla ya kuwakabidhi beji waamuzi wapya wa FIFA kutoka Tanzania kwa mwaka 2015. Hafla hiyo imefanyika leo katika Ofisi za TFF zilizopo Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)
Mwamuzi wa Fifa, Sophia Ismail Mtongori akipokea beji yake ya Fifa kutoka kwa Rais wa TFF, Jamal Malinzi.
Mwamuzi wa Fifa, Jonesia Rukyaa akipokea nyenzo za kufanyika kazi wakati wa hafla ya kukabidhi beji za Fifa kwa waamuzi wa Fifa wa mwaka 2015. Jumla ya waamuzi 18 walikabidhiwa beji zao wakiwemo wanawake 7.
Baadhi ya waamuzi wa kimataifa wa Fifa kutoka Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kukabidhiwa beji zao na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi.
Mwamuzi Msaidizi wa Fifa, Hellen Nduma akipokea beji ya Fifa kutoka kwa Rais wa TFF, Jamal Malinzi
Mwamuzi wa Kimataifa, Jonesia Rukyaa akipokea beji ya Fifa kutoka kwa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi wakati wa hafla ya kukabidhi beji kwa waamuzi 18 wa Fifa wa mwaka 2015 kutoka Tanzania wakiwemo wanawake 7. Hafla hiyo ilifanyika katika Ofisi za TFF zilizopo katika uwanja wa Karume Ilala jijini Dar es Salaam.
Mwamuzi wa Fifa, Florentina Zabron Rukyaa akipokea beji ya Fifa kutoka kwa Rais wa Fifa, Jamal Malinzi wakati wa hafla ya kukabidhi beji kwa waamuzi wa Fifa wa mwaka 2015.
Mwamuzi wa Fifa, Mujuni Nkongo akitoa neno la shukrani.
Mwamuzi Msaidizi wa Fifa, Hellen Nduma akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wenzake baada ya waamuzi 18 kukabidhiwa beji za Fifa kutoka kwa Rais wa TFF, Jamal Malinzi.