Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

CCM WAMSHAMBULIA MDHAMINI CHADEMA

$
0
0
ABDALLAH NA SHEHE SEMTAWA

MJUMBE wa Bodi ya Wadhamini wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Muslim Hassanali, amedai kushambuliwa na katibu kata wa kata ya Kisutu kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM),Sauda Addey, baada ya mjumbe huyo kukataa kubandika kipeperushi cha wagombea wa nafasi ya uenyekiti wa serikali za mitaa kupitia CCM mbele ya eneo lake la biashara.

Hassanal anadai tukio hilo lilitokea juzi jumamosi saa tano asubuhi baada ya wafuasi wa CCM kubandika kipeperushi chao katika eneo lake la biashara lililopo mtaa wa Mali Kisutu jijini Dar esSalaam.

Kushambuliwa kwa Hassanal kumekuja ikiwa ni siku chache zimepita huku baadhi ya wafuasi wa vyama vya siasa katika maeneo mbali mbali nchini wakiwa wameshashambuliana na wengine kusabaishiwa vifo.

Akizungumzia namna alivyoshambuliwa Hassanal alisema baada ya kufika ofisini kwake alikuta kipeperushi hicho na alipouliza watu aliowakuta wakamuambia kuwa makarataisi hayo yamewekwa usiku na kwamba hawamjui aliyeweka.

“Kisheria lile ni eneo langu ninalolimiliki kibiashara hivyo yeyote anayetaka kulitumia ni lazima aonane na mimi nimpe ruhusa ama la sasa hawa CCM wamekuja kuweka pasipo ridhaa yangu na mimi siipendi CCM nikiona hata rangi zao nasikia kichefu chefu nikaona ngoja niziondoe”alisema Hassanal na kuongeza.

“Unajua ile ni sehemu ya biashara wanafika watu wa kila itikadi sasa kubandika picha kama zile zinaweza kuvuruga biashara zangu isitoshe kwa kulitambua hilo ndio maana nimeshindwa hata kubandika picha za wagombea wa Chadema ambacho ni chama changu”.

Alidai kuwa baada ya kuyaondoa  matangazo hayo viongozi wa Kata hiyo wa CCM wakiambatana na wafuasi  wao walimvamia na kumfanyia vurugu zilizosababisha uharibifu wa miwani yake ya macho, vifaa, nyaraka na upotevu wa baadhi ya vitu. 

Alisema kufuatia fujo hizo  alifika katika kituo cha Polisi Kisutu nao wakamueleza hawana mamlaka ya kushughulikia kesi za kisiasa hivyo alifikishe suala hilo kituo kikuu cha kati cha Polisi. 

Hassanali alisema baada yakushauliwa hivyo, aliamua kwenda kituo hicho lakini cha kusikitisha hakuweza kupata ushirikiano wa kutosha na alitakiwa kurudi kituoni hapo siku ya Jumatatu (jana), ambapo alifanya hivyo.

“Leo kama mnavyoniona hapa bado nasumbuliwa nataka kufungua jalada lakini bado wahusika wanazunguuka tu kwa kunieleza kuwa msimamizi wa shauri langu hajafika hata hivyo niliweza kuhojiwa na kuandika maelezo yangu,”alisema.

Wakili wa Hasanali  Fredrick Kihwelo, alikiri mteaja wake kufanyiwa vurugu na kwamba baada ya kufika polisi waliandika maelezo na kuambiwa uchunguzi unaendelea.

 “Pamoja na kukwama siku ya Jumamosi, leo (jana), tumekuja tena, tangu asubuhi tuko hapa na hatimaye tumefungua kesi ya jinai kimsingi suala hili litakuwa kwenye uchunguzi baada ya hapo litapelekwa kwa DPP ambaye ndio ataamua kama litapelekwa mahakamani.

Kwa upande wake katibu  Kata ya wa CCM kata ya Kisutu Sauda, alisema zoezi la kubandika picha za wagombea limefanyika jiji zima kisheria tangu miaka ya nyuma na hakutegemea katika eneo hilo kama angekuwepo mtanzania mwenye asili ya Asia asiwe mfuasi wa CCM.

 “Sisi hatukujua kama pale kuna mtu wa Chadema tena Muhindi kama tungejua tusingebandika kwani kwa zaidi ya mika 25 tumekuwa tukibandika,”alisema.Sauda.

 Kamanda wa Polisi mkoa wa Ilala Mery Nzuki alisema suala hilo bado liko kwa mkuu wa kituo kwa ajili ya uchunguzi na mara litakapokamilika litafikishwa kwake kwa hatua zaidi.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>