Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

ANSAF YAKUTANA NA WADAU WA KILIMO

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi isiyo ya Kiserikali inayojihusisha na masuala ya kilimo (Ansaf), Audax Rukonge akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano uliowakutanisha wajasilimali mbalimbali kupitia kilimo katika Hotel ya Serena jijini Dar es Salaam hivi karibuni. (Picha na Francis Dande)

Na Mwandishi Wetu

MSICHANA mwenye umri wa miaka 19 Anna Malongo amekuwa kivutio kikubwa, katika mkutano wa wajasiliamali wadogowadogo ulioratibiwa na Taasisi isiyo ya Kiserikali inayojihusisha na masuala ya kilimo (Ansaf), baada ya kutoa ushuhuda wa maisha yake kupitia utaalamu wa kutengeneza viatu vya ngozi.

Anna aliyasema hayo katika mkutano huo uliowakutanisha wajasilimali mbalimbali kupitia kilimo katika Hotel ya Serena Jijini Dar es Salaam, kuwa yeye anaishi kwa kupitia utengenezaji wa viatu vya ngozi huku akiwataka wasichana kama yeye kujiamini na kujiajili kuliko kuilalamikia Serikali kila kukicha.

Alisema, yeye licha ya kukumbana na changamoto mbalimbali hasa za umeme na maji katika kijiji chao cha Chilolo Mkoani Dodoma, lakini anapigana kadri awezavyo kuhakikisha anajikwamua na kuyamudu maisha yake, kwani licha ya kumaliza kidato cha nne hakupata fursa ya kuendelea kusoma hivyo kupitia mikono yake anatafuta ada ili ajiendeleze.

“Mimi kusema kweli nina historia kubwa mno katika ujasiliamali huu, nanunua ngozi ya mbuzi sh 3000 ya ngombe sh 8000 na natoa hata viatu vya sh 70,000 hivyo nawaomba wasichana wenzangu hasa wa vijijini kama mimi wasikimbilie kuwa wafanyakazi wa ndani wajitume na kufanya kilimo kinalipa jamani,”alisema Anna.

Mbali na Anna wajasiliamali wengine waliotoa ushuhuda wa maisha yao kuwa bora kupitia kilimo ni Michael Tarimo anayejihusisha na ukulima wa mboga mboga ambapo kupitia kampuni yake ya Home Veg-Tanzania anasafirisha bidhaa zake nchi kama Uholanzi, Ujerumani na nyinginezo.

Akizungumzia mkutano huo wa siku tatu, Mkurugenzi Mtendaji wa (Ansaf) Audax Rukonge alisema, lengo la kufanya mkutano huo, ni kuwakutanisha wajasiliamali ambao wameona matunda yake na wale ambao wanatamani kuingia ila wamejawa na hofu.

“Sisi Ansaf tunaimani kubwa kuwa kilimo ndio uti wa mgogo wa mtanzania, na hapa leo tumewaleta zaidi ya wajasiliamali 18 ambao wamenufahika na kilimo, tunaimani kupitia wao vijana wengine watapata fursa ya kuchangamkia kilimo,”alisema Rukonge na kuongeza kuwa wanatambua wakulima wanachangamoto mbalimbali ila wao kwa kushirikiana na Serikali wanajitahidi kuzitatua.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>