Wachezaji wa timu ya Mtera wakiendelea kuumiliki mpira katikafainali ya Lukuvi Cup kata ya Migoli Mtera |
Mabingwa wa Lukuvi Cup timu ya Mtera wakimiliki mpita |
Mchezaji wa timu ya Home Boys akiwa chini baada ya mchezaji wa timu ya Mtera kuupiga kichwa mpira uliokuwa ukigombewa |
Waziri Nkamia akimkabidhi zawadi mchezaji wa timu ya MTERA |
waziri Nkamia akiwa na mchezaji bora wa timu ya mtera Bw.mzambia |
Waziri Nkamia akimkabidhi kombe kepteni wa Home Boys
Na Matukiodaima Blog
MTERA Shooting yaibuka mabingwa Lukuvi Cup 2014 kwa kata ya Migoli jimbo la Isimani baada ya kuifunga timu pinzani ya Home Boys kwa jumla ya magoli 4-1 katika mchezo wa fainali ulioshuhudiwa na mgeni rasmi naibu waziri wa habari ,vijana ,utamaduni na michezo Juma Nkamia.
Mchezo huo uliochezwa juzi katika uwanja wa Migoli Mtera uliokuwa na upinzani wa hali ya juu kwa timu zote kutokana na kushindwa kuonyeshana ubabe dakika 90 za mchezo kwa timu hizo kutoka sare ya goli 1-1 kabla ya kumsaka mshindi kwa mikwaju ya penati ambayo iliiwezesha timu ya Mtera Shooting kuigagadua (kuifunga) Home Boys kwa jumla ya magoli hayo 4-1 ambayo yaliiwezesha kutwaa kombe na kiteta cha pesa taslim kiasi cha Tsh milioni 1 kutoka kwa mbunge wa jimbo la Isimani Wiliam Lukuvi ambae ni waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera na uratibu wa bunge.
Kbala ya dakika 90 za mchezo kumalizika timu ya Mtera Shooting iliweza kuwanyanyua mashabiki wake baada ya kujipatia goli la kwanza dakika ya 86 kwa mkwaju wa penati goli lililowekwa nyavuni na Mtei Mlimbwa huku dakika ya 88 Frank Jackson aliweza kuisawazishia timu yake ya Home boys goli hilo hivyo timu hizo kutoka uwanjani dakika 90 kwa bila mbabe kujulikana.
Hali hiyo iliweza kupelekea mashabiki wa kila timu na wachezaji kupigwa na butwaa ya nani kutwaa kombe hilo kabla ya mwamuzi kutumia njia ya matuta kumpata mshindi ambae alitokana na ujuzi wa kugusa nyavu za mwenzake.
Akikabidhi zawadi kwa mshindi wa kwanza, wa pili na wa tatu, Naibu Waziri wa habari, vijana, utamaduni na michezo, Juma Nkamia,ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi, alisema kuwa vijana wengi Tanzania wanapenda michezo japo bado kuna tatizo kubwa kwa viongozi wa michezo hususani walimu wa timu kwa kutokuwa na mafunzo ya ualimu wa timu.
Mapema katibu wa mbunge Lukuvi ,Thom Malenga alisema kuwa lengo la mbunge Lukuvi kuanzisha mashindano hayo ni kuweza kuhamasisha michezo katika jimbo hilo na kuwafanya vijana kuepukana na matumizi ya madawa ya kulevya pamoja na mambo mengine ambayo yanaweza kuwasababishia kupata maambukizi ya VVU.
Mbali na hilo alisem akuwa kupitia michezo wananchi wanakuwa pamoja na kuondokana na masuala ya itikadi vya vyama wakati wa kufanya shughuli za kimaendeleo.
Pia alisema mbali ya mashindano hayo ya ngazi ya kata pia ameanzisha mashindano ya ngazi ya tarafa ambapo bingwa atazawadiwa Power tilla kwa ajili ya kuanzisha vikundi vya uzalishaji mali katika tarafa.
Waziri Nkamia akizungumza kabla ya kukabidhi zawadi kwa mshindi wa mashindano hayo alisema kuwa uamuzi uliofanywa na mbunge Lukuvi katika kuanzisha michezo ni uamuzi wa kupongezwa kwani mbali ya kutekeleza ilani ya CCM katika michezo bado amewawezesha vijana kupata fursa ya kuonyesha vipaji vyao ili kupata nafasi ya kuchezea timu kubwa zaidi .
Hivyo alisema katika mchezo huo kwa upande wake amependezwa na kiwango cha mchezo cha mchezaji wa timu ya Mtera pia alisema kuwa mbunge Lukuvi ametenga zaidi ya Tsh milioni 30 kwa ajili ya mashindano ya soka katika jimbo hilo la Isimani na yeye kama waziri mwenye dhamana ya michezo amependezwa zaidi na jitihada hizo
" Mimi katika kuunga mkono jitihada hizi za Lukuvi nawaahidi kuwa nitawasiliana na Lukuvi ili mabingwa wakacheze na timu yangu jimboni Kondoa mkoani Dodoma na mchezo mwingine waje wacheze hapa Mtera hapo vipi ".
Katika mashindano hayo NKamia alimkabidhi mshindi wa kwanza kombe na fedha taslimu shilingi milioni 1 huku mshindi wa pili akuikabidhiwa kombe na shilingi 500,000,mshindi wa tatu akipewa Tsh 250,000 na mchezaji bora kutoka timu ya Mtera akipewa Tsh 100,000