Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wake wa hadhara uliofanyika leo, Oktoba 9, 2014 kwenye Uwanja wa Mashujaa, mjini Mufindi akiwa katika ziara ya kukagua na kusimamia utekelezaji wa ilani ya Chama mkoani Iringa
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipokea saluti ya Vijana wa CCM alipowasili wilayani Mufindi mkoani Iringa
Kinana akisalimiana na Mbunge wa Mufindi Kusini Menradi Kigola wakati wa mapokezi hayo. Kulia Katibu wa CCM wilaya Mufindi Mtaturu.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiangalia namna mbao zinavyotayarishwa kwenye kiwanda cha mbao cha Emmanuel Investiment, kinachomilikiwa na Ndugu Charl Ayo, mjini Mafinga wilayani Mufindi mkoani Iringa
Katibu Mkuu wa CCM akikagua kiwanda hicho cha upasuaji mbao
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitazama mti uliopandwa na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kwenye Ofisi za Kampuni ya Sao Hill, wilayani Mufindi alipotembelea kampuni hiyo. Mto huo ulipandwa na Mwalimu Nyerere zaidi ya miaka 30 iliyopita.
Mti wa Mwalimu Nyerere ulivyostawi Sao Hill
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipanda mti wa kumbukumbu kwenye viwanja vya Kampuni ya Sao Hill
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akipanda mti wa kumbukumbu kwenye viwanja vya Ofisi za Kampuni ya Sao Hill, Mufindi
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Sao Hill wakimpokea Kinana alipotembelea kampuni hiyo
Image may be NSFW.
Clik here to view.
Clik here to view.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo kwenye mkutano mkuu wa CCM jimbo la Mafinga Kaskazini.
Image may be NSFW.
Clik here to view.
Clik here to view.

Baadhi Wajumbe waliohudhuria mkutano Mkuu wa CCM Jimbo la Mafinga Kaskazini
Viongozi wa Dini wakiwa kwenye mkutano mkuu wa CCM jimbo la Mufindi Kaskazini
Mwenyekiti wa Wazee Waasisi wa CCM wilaya ya Mufindi Mzee Raphael Ngogo akisoma risala ya Wazee kwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana
Wajumbe wakiimba nyimbo za kumkaribisha Kinana.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimiana na viongozi wa Dini wilaya ya Mufindi ambao walialikwa kwenye mkutano mkuu wa CCM Jimbo la Mufindi Kaskazini.
Mganga Mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Mufindi Dk.Boaz Mnenegwa akizungumza na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana wakati alipotembelea wodi ya kina mama hospitalini hapo.
Sehemu ya Wodi ya akina mama katika hospitali ya wilaya ya Mufindi.