Quantcast
Channel: HABARI MSETO BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

MKUU WA WILAYA MTWARA AFUNGUA WARSHA YA SIKU MBILI YA MASUALA YA MAAFA

$
0
0
Tathmini ya Viatarishi, Uwezekano wa Kuathirika na Uwezo wa Kukabiliana na Maafa (Risk Vulnerability and Capacity Assessment - RVCA) yafanyika Wilayani Mtwara


Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Bw. Wilman Ndile afungua Warsha ya Siku Mbili Wilayani Mtwara kuhusu“Mpango wa Kujikinga, Kukabiliana na Kuzuia athari za Maafa kwa Wilaya ya Mtwara leo tarehe 26 na 27 Septemba, 2014. 

Wakati wa ufunguzi huo Bw. Ndile alisema Mpango huu utasaidia sana pindi maafa yatakapotokea na kuwaomba washiriki wa warsha hiyo kutoka Manispaa na Halmashauri ya Wilaya hiyo kushiriki vema katika mafunzo na kuchangia masuala hayo ili kuweza kukamilisha mpango huo unaoratibiwa na Idara ya Uratibu wa Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu. 

Alisema “hatua hizi zimekuwa madhubutu na zitatusaidia sana sisi kama wadau wakubwa wa Maafa katika Halamshauri zetu na Manispaa kwa kuona uzito wa  suala la Maafa ni la kila mmoja na sio Ofisi ya Waziri Mkuu ambaye ni mratibu tu wa Maafa” alisisitiza Bw. Ndile. 

Imetolewa na Afisa Habari Ofisi ya Waziri Mkuu
26 Septemba, 2014, Mtwara

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19659

Trending Articles