Washiriki wa Fainali za Mashindano ya urembo ya Redds Miss Tanzania 2014 kutoka mikoa mbalimbali nchini wataanza kambi rasmi ya mafunzo kwa kuingia kambini Jumamosi ya tarehe 13 Septemba 2014.
Washiriki hao 30 watapiga kambi katika Hotel ya JB Belmont iliyopo katikati ya jiji ya D’salaam ambapo mazoezi na mafunzo ya aina mbalimbali yatatolewa kwa muda wa wiki nne kabla ya Fainali za Taifa ambazo zimepangwa kufanyika mapema mwezi ujao.
Wakiwa kambini warembo hao watapewa semina kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu mashindano ya urembo, kusaini Mikataba n.k.
Kwa mujibu wa Ratiba ya Kambi iliyotolewa na Lino International Agency Limited, waandaji wa Mashindano ya urembo ya Miss Tanzania, washiriki hao watakuwa hotelini hapo kwa muda wa siku 3 tu, na baadaye kuanza ziara ya kutembelea Vivutio mbalimbali vya Utalii katika mikoa ya Morogoro, Tanga, Kilimanjaro, Manyara na Arusha.
Washiriki hao watarejea jijini D’salaam tarehe 28 Septemba 2014 na kufikia katika hotel ya Kijiji Beach Kigamboni na kuendelea na ratiba yao ya mafunzo kama ilivyopangwa na waandaji.
Orodha ya washiriki pamoja na mikoa wanayowakilisha imeambatanishwa.
Shindano la Redds Miss Tanzania linadhaminiwa na REDDS ORIGINAL.